Mwabukusi: Mbeya Sio Jiji ni Mkusanyiko wa Vijiji Vikubwa. Haina Miundombinu na Mzunguko wa Pesa ni Mdogo

Kwani hakuna miradi? Hakuna Barabara kuu na za mitaani zinazoendelea na Ujenzi? πŸ‘‡πŸ‘‡View attachment 3643950

Stendi kuu ,masoko ,Viwanja vya mpira vya kisasa no vyote vinajengwa.
Mbeya ina deserve miradi mingi zaidi. Hivi umeona Dar sasahivi? Kila sehemu ni ujenzi wa barabara, nyingine zinakuwa renewed, wanaweka hadi sidewalks Dsm, angalia video za Bertin

Mbeya ndio ilipaswa iwe hivyo. Naongelea ndani ya jiji. Ilipaswa kuwe na ujenzi massive wa mtandao wa lami kila kona ya jiji na barabara zilizochoka ziwe renewed, na waweke sidewalks na proper drainage system kama Dar, nimeona maeneo mengi ambayo recently wameweka closed drainage system, miradi kama hiyi na hapa Mbeya inahitajika

Halafu upande wa mazingira inabidi waanze upandaji wa miti, yani urbanisation inavyoongezeka Mbeya watu wanakata miti hovyo sana. Jiji litapoteza status ya Green City
 
Hiyo hadhi ya kupewa miradi mingi kama Dar au Dom hawana.

Mwanza wanalia daily sembuse Mbeya? Wewe hujui nafasi ya Dar,Dom na Arusha hapa Tanzania?

Mbeya itapewa miradi ila sio kama ya Dar ndio maana imepewa Stendi Mpya ya kisasa,Soko jipya,uwanja wa ndege Mpya,na upanuzi wa Barabara kuu na za mitaani.
 
Hii ndio sababu watu hawaipendi CCM. Wote huwa mnafikiria kama wewe
Umeshasema Mbeya ni mkoa wa 3 kwa uchumi Tz, sasa kwa nini hawastahili hiyo miradi? Tena Mbeya ndio inahitaji hiyo miradi kwa kiasi kikubwa, Mbeya inahitaji barabara nzuri, proper drainage system na sidewalks hata itasaidia kupunguza vumbi
Na barabara zinatumika sana so inapaswa ziwe katika hali nzuri

Kama maendeleo yenyewe ndio ya kupendelea maeneo machache ya nchi basi ni heri tu serikali ya majimbo. Watu wamechoka
 
mkataa kwao ni mtumwa πŸ’
 
Kama hujui sababu harafu unajiita msomi wewe Bado ni mjinga.

Mfumo wa centralized economy unategemea matakwa ya Kisiasa badala ya kuangalia vigezo.

Hata Mwanza ni namba 2 Kwa Uchumi lakini hakuna miradi yeyote ya maana Kwa sababu ya mfumo wa governance ulivyo maana unategemea hisani ya mwanasiasa ila sio hadhi stahiki.
 
Na huu ndio ujinga. Unajaribu ku justify ukosefu wa miundombinu bora Mbeya kwa kusema hata Mwanza hawana. Kwa nini Mwanza hawana hiyo miundombinu in the first place?
Mwanza kukosa hiyo miundombinu pia ni makosa makubwa sana. Serikali yoyote yenye akili timamu ingeelewa kuwa Mwanza na Mbeya zinahitaji miundombinu bora zaidi ili kuchochea ukuaji wa uchumi na uwekezaji
Pia street lights ni janga kubwa sana Mbeya. Miji yote miwili inastahili miundombinu bora.
Wala hakuna sababu ya kisomi kuhalalisha uhaba wa miundombinu kwenye hiyo miji
 
Nakupa sababu bado huelewi ,haya wewe unataka miundombinu sijui miradi ipelekwe Kwa utaratibu upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…