Sheria ni sheria hata kama ni sheria mbaya. Uchaguzi huu unaendeshwa kwa mujibu wa sheria zetu hadi hapo sheria itakaposema vinginevyo. Kelele zinazosikika za akina MWABUKUSI na wengine ni kelele za kutaka watu wapindishe sheria ili kuwaridhisha watu wasioipenda sheria husika. Katiba hii ni katiba ya 1977 wakati wa Nyerere; haikutungwa na Samia na wenzake. Mwabukusi anataka Rais samia apore na kupoka madaraka ya wananchi ya kuandika katiba yao ili kuwaridhisha kikundi cha watu wachache; hii hatutaikubali. Katiba ni mali ya watanzania wote, hivyo kama kuna shida kwenye katiba tuhusishwe wote tulione hilo tatizo na tukubaliane kuwa ni tatizo kweli au ni mtizamo tu wa watu.
kama Rais samia atakubali kuichakachua katiba kwa maoni ya wachache atakuwa hafai hata kuongoza tarafa. Katiba hii ipo tangu 1977 hakuna haraka, tutafute muda tuiangalie wote.
chadema ni watanzania, lakini watanzania sio chadema. Katiba haina kukaa mezani, bali inatekelezwa.
Kama sheria zinatungwa bungeni basi wabobezi wa sheria wengi nendeni bungeni kupitia chama chochote hata ikibidi CCM ili mkatuletee sheria nzuri lakini sio kuhamasisha Rais avunje sheria kuwaridhisha chadema na watu wengine.
Ukishindwa kumshinda ungana nae.