Mwabukusi: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeng'olewa Meno

Mwabukusi: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imeng'olewa Meno

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini imeshindwa kuwa huru na kutekeleza wajibu wake kikamilifu.

"Tume ya Haki za Binadamu kwa kweli haina meno. Imeng'olewa meno, sasa tunaipa kuwa itafune, haitaweza."

Akizungumza katika mahojiano yaliyorushwa Septemba 19, 2026 na Nijuze, Wakili Mwabukusi ameeleza kuwa tume hiyo haina meno na imekuwa ikipoteza mwelekeo hata inapopaswa kuchunguza matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki nchini.

Mwabukusi amebainisha kuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili tume hiyo ni pamoja na ukosefu wa uhuru wa kisheria na kifedha, kwani inalazimika kuomba msaada wa wanasheria kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali inapotaka kufungua mashtaka. Amsisitiza kuwa hali hiyo inainyima tume uwezo wa kutenda kazi kama chombo huru kinachojitegemea na chenye meno ya kisheria.
 
Back
Top Bottom