Mwabukusi: Tunapoteza nguvu kushughulika na upinzani kuliko Ripoti ya CAG

Mwabukusi: Tunapoteza nguvu kushughulika na upinzani kuliko Ripoti ya CAG

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa kauli nzito kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), akidai kuwa ripoti hiyo imeendelea kuwa "kumbukumbu ya kila mwaka" isiyo na matokeo ya kisheria kwa wabadhirifu wa mali za umma.

Akizungumza na televisheni ya mtandao ya Saut Digital, Mwabukusi ameeleza kusikitishwa kwake na namna serikali na vyombo vya dola vinavyoshindwa kutumia robo tu ya nguvu inayotumika kwenye siasa kudhibiti ubadhirifu unaofichuliwa na CAG.

“Kwa hiyo tukiweza kutuma huo ujumbe kwa kutumia vyombo vyetu kama TAKUKURU, ofisi ya CAG mwenyewe na ofisi ya DPP huku ndiko tulikotakiwa tuweke mkazo sio huku tunakokimbizana na kina CHADEMA,, huku mara umekamata Tundu Lissu, sijui umemkamata nani...vitu vidogovidogo visivyokuwa na maana tunapoteza muda mrefu…robo tu ya nguvu tunayopeleka kwenye siasa kukimbizana na vyama vya kweli vya upinzani tukaiwekeza huku kwenye kusimamia rasilimali, kuna fedha nyingi sana zinaweza zikaokolewa, na zikaenda kusaidia kwenye ujenzi wa miradi na huduma za jamii”, ameeleza Mwabukusi.

Mwabukusi amebainisha kuwa CAG anafanya kazi kubwa ya kugundua mapungufu, lakini inapofika wakati wa kutoa mapendekezo, ofisi hiyo inakosa nguvu ya kisheria ya kusimamia utekelezaji. Amependekeza maboresho ya vifungu vya sheria ili kumwezesha CAG kupendekeza hatua za kisheria moja kwa moja.

“Mimi nilikuwa nadhani kuhusu CAG, tuboreshe kifungu cha kumwezesha kuchukua hatua au kupendekeza hatua za kisheria kwa sababu nilikuwa nasikiliza mapendekezo ya CAG, ukweli amegundua mambo makubwa lakini kila akifika kwenye mapendekezo alikuwa anabutua, alikuwa alikuwa anapaisha, nilikuwa naona mapendekezo yake, yalikuwa hayashabihiani na ule udhaifu aliokuwa akiugundua. Kwahiyo hapo ndio sehemu yenye udhaifu, namna ya kuchukua na kuifanyia kazi ili kumfanya mtu aogope kwamba kuchukua fedha ya umma au kufanya ubadhirifu wa mali ya umma ni jambo la hatari sana, mtu asilizoee”, amependekeza Mwabukusi.

Wakili huyo msomi amesema kwa sasa Bunge haliwezi kutegemewa katika kusimamia uwajibikaji kwani "lilishakataa" wajibu huo na badala yake linaishia kumdhibiti CAG anaponyooshea kidole udhaifu wao. Aidha, ameelezea kudhoofika kwa vyama vya siasa, akidai kuwa CCM ya sasa haina uwezo wa kuikemea serikali kama zamani, huku vyama makini vya upinzani kama CHADEMA (Bara) na ACT Wazalendo (Zanzibar) vikiwa vimebanwa kufanya harakati zao.

Mwabukusi amesisitiza kuwa taifa linapita kwenye mkwamo mkubwa ambao suluhisho lake ni Katiba Mpya na marekebisho ya sheria yatakayozipa uhuru wa kikatiba, kisheria, na kibajeti taasisi kama ofisi ya CAG, DPP, na Tume ya Haki za Binadamu.

Ameenda mbali zaidi na kupendekeza kuundwa kwa Tume ya Ukweli, Haki, na Uwajibikaji ili wananchi wajadili jinsi taifa lilivyofika hapa na kutafuta majawabu ya hasira zilizopo mioyoni mwa watu.

Mwabukusi ameonya kuwa bila kuchukua hatua sasa, taifa halitafikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa kutokana na nakisi kubwa ya fedha zinazopotea. Amesisitiza kuwa uzembe huu unaporomosha uchumi na kushusha maadili ya utumishi wa umma.
 
Screenshot_20260401-130445~2.png
 
Nguvu iliyotumika kuwauwa wanaodaiwa wandamanaji hapo tarehe 30 ilikuwa kubwa mno kuliko inayotumika kupambana na majangili ya ccm.
Unamfyatulia risasi mtu akiwa dukani, unamwita mfanya vurugu.
Yule jambazi wa wizara Fulani unataka atajwe tu Ili ajisikie Aibu yaani
 
Back
Top Bottom