Mwabukusi: Watanzania waambie waandamane kwa ajili ya Simba au Yanga, wataandamana hata uchi

Mwabukusi: Watanzania waambie waandamane kwa ajili ya Simba au Yanga, wataandamana hata uchi

Kwa kifupi Watanzania tulio wengi hatuna 'critical thinking' (hatuwezi kuhoji kwa nini mambo yafanyike kama yanavyofanyika na si tofauti). Kwa vile hatuna utamaduni wa kujihoji, tupo tupo tu bora liende, Kila mtu na shughuli zake.
Ni kama hapo mwandishi kashindwa kumhoji Mwabukusi anayejifanya ana critical thinking kuwa kwa nini hakuandamana maandamano ya Chadema jana?
Mwandishi alikosa kuhoji critical questions

Na Mwabukusi aliongea tu hewa ananyooshea tu vidole watanzania kuwa wajinga utafikiri yeye sio mtanzania yeye mbona hakushiriki maandamano ya Chadema? Na Chadema ndio waliomsaidia kupata uraisi wa Tanganyika Law Society kupitia Tundu Lisu makamu mwenyekiti wa Chadema ambaye pia alimshukuru waziwazi

Tundu Lisu tusaidie kwa nini huyo mtu wako Mwabukusi uliyemfanyia kampeni kuwa Raisi wa Tanganyika Law Society akashinda hakushiriki hayo maandamano ya Chadema

Lisu tupe jibu
 
Huu nao ni Wendawazimu kulinganisha yasiyoendana.Hao watakaoandamana kwa Simba au Yanga ni Mashabiki wa timu husika sio lazima wahusike na mambo mengine.Kama wanahitajika umati kama huo ni jukumu la Wahusika kuhamasisha ili nao wafikie huko na sio kutamani Wahusika wa mambo mengine.Huenda Mashabiki wa Simba na Yanga ni Watu milioni 7 tu, bado kuna zaidi ya Watanzania milioni 30 au 40 wa kufuatilia mambo mengine.Sasa inashangaza kushindwa kwako kuhamasisha muwatupie lawama wanaocheza vema upande wao?Vipi kama mliokuwa mkipingana nao (serikali) ndio wamefanikiwa dhidi ya hamasa ya kuandamana,bado utawalaumu Mashabiki wa Simba na Yanga? Kwani wakiitisha hay maandamano ya Simba na Yanga pia kutakuwa na vitisho vya Mamlaka?
 
Watanzania waambie njooni muandamane Simba ameleta kombe, wataandamana hata uchi kwenda uwanja wa Taifa. Wanazingatia sana mamboa ambayo si ya msingi.

Kwenye culture yetu tuliamini kuwa mambo yote magumu magumu ni ya viongozi. Hali hii itaendele na itakuwepo kwa muda mrefu kwasababu kwanza hatujabadili mfumo wetu wa elimu na sasa hivi tumeubemenda, tumeutikisa zaidi.

Ile free thinking huipati sawasawa ndiyo maana utakuta watoto wa siku hizi Ukimona anapiga kelele ni boom, yaani kama ndege.

Soma:
atuache kila mtu na starehe yake yeye aandamane tu ndio hobby yake
 
Watanzania waambie njooni muandamane Simba ameleta kombe, wataandamana hata uchi kwenda uwanja wa Taifa. Wanazingatia sana mamboa ambayo si ya msingi.

Kwenye culture yetu tuliamini kuwa mambo yote magumu magumu ni ya viongozi. Hali hii itaendele na itakuwepo kwa muda mrefu kwasababu kwanza hatujabadili mfumo wetu wa elimu na sasa hivi tumeubemenda, tumeutikisa zaidi.

Ile free thinking huipati sawasawa ndiyo maana utakuta watoto wa siku hizi Ukimona anapiga kelele ni boom, yaani kama ndege.

Soma:
Mwambusi akumbushwe kuwa hata mahakama hatuna tuna shina la CCM
 
Ni kama hapo mwandishi kashindwa kumhoji Mwabukusi anayejifanya ana critical thinking kuwa kwa nini hakuandamana maandamano ya Chadema jana?
Mwandishi alikosa kuhoji critical questions

Na Mwabukusi aliongea tu hewa ananyooshea tu vidole watanzania kuwa wajinga utafikiri yeye sio mtanzania yeye mbona hakushiriki maandamano ya Chadema? Na Chadema ndio waliomsaidia kupata uraisi wa Tanganyika Law Society kupitia Tundu Lisu makamu mwenyekiti wa Chadema ambaye pia alimshukuru waziwazi

Tundu Lisu tusaidie kwa nini huyo mtu wako Mwabukusi uliyemfanyia kampeni kuwa Raisi wa Tanganyika Law Society akashinda hakushiriki hayo maandamano ya Chadema

Lisu tupe jibu
wewe unapima ujasiri wa Mwabukusi kwa maandamano ya jana? labda km akili yako ni ndogo km ya sisimizi unaweza uliza kwa nini hukumuona jana..
 
Watanzani wataandamana kama mifumo yao ya kujipatia kipato itaathiriwa.

Ni wabinafsi sana na hawana hulka ya kujali wengine.

Mtu kama haimhusu basi hajali.
Leo umeongea point iliyojitosheleza kwa 100%. Umemuelezea mtanzania kwa utoshelevu kwa kutumia maneno machache tu. Watanzania huwa hatujali yanayowafika wengine hadi yatufike wenyewe, na tulivyo wajinga yakishatufika huwa tunataka kila mtu aguswe na kujali.

Hii tabia ya ubinafsi hata ndugu zangu kadhaa kila siku nagombana nao, yaani walishapotezwa na propaganda za sisiem, sasa hata utekaji ushamiri vipi wao ni kuwashutumu wapinzani kuwa wanataka kuleta vurugu, mara kupindua nchi nk huku wakiikingia kifua serikali na kuamini 'kifo ni kifo' kama mama yao wa hiari anavyowaaminisha. Nami huwaambia kuwa 'mnadhani hayawahusu kwakuwa mnayasikia kwa wengine, siku yakiwahusu itakuwa too late'. Ajabu ni wasomi wote!

Nchi hii bado tuna safari ndefu sana. Wale wanaosema mwafrika bado yupo kwenye transition kutoka mnyama kuelekea binadamu kidizaini huwa nawaelewa.
 
Back
Top Bottom