Mwabukusi: Waziri hana Mamlaka ya kufuta Kijiji na asili ya Watu wa Ngorongoro

Unajua Tanzania ni mwananchama wa mikataba mbalimbali ya kimataifa juu ya haki za watu na binadamu?

Haki ya kuwatambua indigenous people ipo kwenye mkataba wa kimataifa na Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizosaini mkataba huo kwa maana watu wanaotokea maeneo yao ya asili wasiondolewe bali watengenezewe mazingira yanayoendana na eneo husika.

Kuna kesi ya Kenya dhidi ya jamii ndogo ya watu walioishi miaka mingi kwenye pori kabla serikali haijatangaza kuwa hifadhi ya taifa.

Walipowaondoa wakaenda mahakama za ndani wakashinda baadae serikali ya Kenya ikasuasua kutekeleza kikamilifu hukumu hivyo jamii ile wakaenda mahakama ya Afrika wakashinda kesi na Serikali ya Kenya iliamuriwa kuwarejesha kwenye makazi yao ya asili na kuwalipa fidia juu.
 
magolo utayaweza nayo hujiona maarabu, wakati yanaitwaga magolo, " hiyo golo akili haina"
“Hatua ya kufuta vijiji na vitongoji ni hatua inayoenda mbali sana. Maana yake ni kwamba wananchi wahusika hawatakuwa na serikali zao za mitaa vijijini na vitongojini. Hii ni kinyume cha ibara ya 145 na 146 ya Katiba ambayo inazungumzia Madaraka ya Umma na kuweka Serikali za Mitaa. Kuwa na madaraka ngazi ya vijiji ni mosi, kuimarisha demokrasia ngazi za chini; pili kuwezesha wananchi waishio vijijini kushiriki katika utawala ambayo ni haki yao kwa mujibu wa ibara 21(1); na tatu, waishio katika eneo hilo kupata haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika Halmashauri zao kama wananchi wenzao waishio katika maeneo mengine. Kwa kuwa vijiji vimefutwa wananchi hao watakosa haki hizo. Kwa maneno mengine wamekuwa disenfranchised (Kuporwa haki). Jamani tunaelekea wapi? Nini lengo la kufanya hivyo? Je tuelewe vipi? Tuambiwe waziwazi kama jamii ya Kimaasai waishio Ngorongoro ni wananchi au wakimbizi wa ndani? Prof. Shivji

Maneno ya Mhadhiri Mwandamizi Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Profesa wa Sheria Profesa Issa Shivji kupitia mtandao wake wa X.
 

Naona wewe huna uelewa wowote juu ya sheria za Nchi yako
Rais ana mamlaka kisheria kubadilisha matumizi ya ardhi kwa maslahi ya umma, na walio adhirika kupewa maeneo mbadala ya kuendesha maisha yao. Ikumbwe kuwa, Ngorongoro ndio lango la watalii (roho ya utalii) ambao ndio unapatia Nchi fedha za kigeni hivyo hapa kinacho angaliwa ni maslahi ya umma sio maslahi ya Wamasai pekee.

Kuhusu watu kuhamishwa; watu walihamishwa sana kupisha mbuga za wanyama la sivyo, hao wanyama wangekuwa wamekwisha, Lakini pia kuhamishwa sio jambo geni, vijiji vya ujamaa watu walihamishwa nk nk nk
Mwisho: wamasai waliachwa tu kwa sababu walionekana kwa kipindi hicho hawakuwa na madhara na mazingira pamoja na wanyama waliokuwepo kama sio hicho kigezo wangekuwa wamehamishwa...

Hata hivi sasa kuna miradi mikubwa ya kimkakati yenye maslahi kwa umma inafanyika na watu wanahamishwa makazi yao na kufidiwa; sijui kwa nini kwa wamasai ionekane tofauti
NAFIKIRI KINACHOLETA UKAKASI KWENYE HUU MJADALA NI TAFSIRI INAYOPOTOSHWA

Hivi inawezekanaje Serikali, iamue kuwa eneo flani liwekwe mipaka na kuitwa kata x, wakati huo huo mseme kwamba Serikali haina mamlaka ya kufuta kata x iliyo ianzisha yenyewe?

Mimi sio mwana sheria ila ni mtazamo tu!
 
Kwenye hili wewe na Mwambukusi wako ni novices na you will be defeated again. Tafuta hii hukumu hapa
 
Umechanganya masuala mawili tofauti. Sheria zetu zinasema ardhi ni mali ya Serikali na wananchi wanaimiliki kwa njia ya sheria ya vijiji au sheria ya ardhi.

Serikali inauwezo kubadili matumizi ya ardhi kwa namna inavyoona inafaa
 
Kwenye hili wewe na Mwambukusi wako ni novices na you will be defeated again. Tafuta hii hukumu hapa
View attachment 3074987
Pamoja na kukutambua wewe sasa unaposimamia, nakushukuru kwa hizi jitihada za kuleta taarifa.

muhimu juu ya swala hili.

Lakini sikubaliani nawe kuhusu hitimisho lako hilo kwa sababu nyingi tu.
Nami nisinge furahishwa kuona hao watu wa nje ndio wakiwa kichocheo cha kututafutia haki sisi wenyewe.
 
Ni ngumu sana kuwabeba watanzania, wanaotegemea kuwa mtu mmoja ndio atawaletea mabadiliko halaf wao wanakuwa busy na umbea, uchawa, uzinzi… huyo mtu mmoja akianguka wanambebesha lawama
Hapana. Usiwahukumu waTanzania kwa vile huwaelewi vizuri.

WaTanzania hawahitaji "kubebwa" na yeyote. Hili ndilo kosa kubwa mnalochanganya wengi.

WaTanzania wenyewe wataleta mabadiliko watakapo pata uongozi wanao uamini. Hawahitaji kusukumwa na mtu yeyote.

Ukipatikana uongozi wanao uamini kuongoza jitihada zao, hutahitaji kuwakumbusha wajibu wao.
 
Umechanganya masuala mawili tofauti. Sheria zetu zinasema ardhi ni mali ya Serikali na wananchi wanaimiliki kwa njia ya sheria ya vijiji au sheria ya ardhi.

Serikali inauwezo kubadili matumizi ya ardhi kwa namna inavyoona inafaa
Pia umesahau kwamba katiba ndiyo sheria mama ambapo sheria zingine zote lazima zitungwe within a scope of constitution.

Ni haki ya kikatiba kila mtu kumiliki mali ikiwemo ardhi. Hivyo huwezi kubadili tu matumizi ya ardhi kwa utashi wako bali kwa kuzingatia sheria za nchi na zile za kimataifa ambazo nchi imeridhia.
 
Ukweli hili ndilo linahitajika kueleweka vizuri na kila upande, badala ya serikali kuburuza tu watu kwa vile inashikilia mamlaka.
 
Hapana. Usiwahukumu waTanzania kwa vile huwaelewi vizuri.
WaTanzania wenyewe wataleta mabadiliko watakapo pata uongozi wanao uamini. Hawahitaji kusukumwa na mtu yeyote.
No mabadaliko hayategemei uongozi, yanaetegemea umoja walionao. Uprising unayo iona currently haina chama cha siasa ndani yake, but ni wananchi waliochoka wakashikamana kupeleka hoja zao, hawakuhitaji kiongozi

Wabongo umoja 0, udhubutu 0, even kujali mambo ya muhimu 0, halaf wanataka aje kiongozi ndio waamke? Seriously
 
No mabadaliko hayategemei uongozi, yanaetegemea umoja walionao.
Huu "umoja" utapatikana vipi kama hauongozwi? Sijasema pawe na chama cha siasa ndicho kiongoze hayo mageuzi.
Wabongo umoja 0, udhubutu 0, even kujali mambo ya muhimu 0, halaf wanataka aje kiongozi ndio waamke? Seriously
Very wrong conclusion.
Ninapata taabu sana kuutumia huu mfano, kwa vile sikupenda baadhi ya mambo yake yaliyo tokea - Magufuli pamoja na ukichaa wake ule waTanzania walielewa sana baadhi ya mambo aliyo yasimamia. Ukisema "hawakujali mambo ya muhimu" katika yale ya muhimu aliyokuwa akiyafanya, sitakubaliana na wewe kamwe.
Huo ni mfano mmoja tu.
 
Is why napinga dependency mpaka atokee mtu ndio watu nao watokee. Akianguka nao wanarudi nyuma
Case study magufuli

Nchi zingine wanawezaje? Umoja wao wanatengenezaje without too much dependecy on kiongozi?

Current case study, bangladesh, walipoteza watu wengi kwneye vuguvugu lao, but still they continue, hawakurudi nyuma.
 
I can assure you, hakuna nchi ya watu wasio tegemea uongozi kati yao ili kufanya mambo yao.
BTW: uwe mwangalifu hapa. Usitegemee hata siku moja wananchi wa nchi yoyote, "wote", au hata asili mia 60 ya watu hao kuwa pamoja kuleta mabadiliko.

Hizi huwa ni jitihada za makundi ya watu wachache ndani ya nchi, wengine hufuata tu, na wasiokubali daima watakuwepo.

Kwa hiyo tusiwalaumu waTanzania wote kwa ujumla wao, we only need to have a few dedicated groups to bring about change; and these need leadership.
 
Current case study, bangladesh, walipoteza watu wengi kwneye vuguvugu lao, but still they continue, hawakurudi nyuma.
WaTanzania waliwezaje kwenda vitani na kumwondoa Nduli! Wewe unadhani hapakuwepo na waTanzania walio poteza maisha yao huko vitani?

Sasa jiulize, ilikuwa kuwaje wakajitoa mhanga huo wa vita.
What's different? Leadership matters.
 
WaTanzania waliwezaje kwenda vitani na kumwondoa Nduli! Wewe unadhani hapakuwepo na waTanzania walio poteza maisha yao huko vitani?

Sasa jiulize, ilikuwa kuwaje wakajitoa mhanga huo wa vita.
What's different?
mfano wake hauna comparison inayolingana. We were at war, now hatuko at war. Hizi ni nyakati mbili tofauti, zisizo na mazingira yaliyofanana

Vijana wa bangladesh wamewezaje kuiforce goverment yao kuachana na upendeleo wa ajira? Walikuwa na kiongozi No? Wameoigana vita?
Vijana wa kenya wamewezaje ku force serikal kuwasikiliza matakwa yao? Kulikuwa na kiongozi specific ? Walienda vitani?

Hizi ni live example, kinachohitajika ni common interest among wananchi, udhubutu, umoja period
So far umoja hawana, udhubutu hawana, na hayo mambo wanakuwa nayo kwenye mambo ya kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…