Naomba nikuelezee mambo yanayojiri Ngorongoro ili usije kuwa unapotoshwa, na kuanza kuilaumu Serikali kimakosa:-
1. Watu wanaishi Ngorongoro bila kuwa na huduma muhimu za jamii, hususani shule, hospitali, na nyumba za kuweza kuishi binadamu wa karne hii.
2. Watu wanakufa kwa kuliwa na wanyama wakali, ie simba nk, nilishuhudia mabaki ya watoto waliokuwa wanatoka kuchunga mifugo wakavamiwa na kuliwa na simba, mtoto mmoja akawahi kukimbia akapanda mti. Huyo mtoto anasishi na trauma mpaka leo
3. Robo tatu ya watu wanaoishi Ngorongoro hawamiliki mfugo hata mmoja, mifugo iliyomu humo ni ya watu wengine tofauti kabisa ambao wamepeleka mifugo yao humo kwa ajili ya malisho, na kuwapa watu wanaoishi humo kazi ya kuitunza mifugo hiyo, na ndiyo wanao-fund hayo maandamano ya wamasai kwaajili ya interest zao.
4. Kuna baadhi ya jirani zetu wanasafirisha nyama ya kondoo uarabuni, sasa kwa kukosa maeneo ya malisho nchini mwao, wameamua kuwapa wamasai wanaoishi huko kwao mkataba wa kuwanoneshea mifugo hiyo kwenye bonde la Ngorongoro na kwa kuwa koo za wamasai zimesambaa across boundary wamewaruhusu wenzao kuleta hiyo mifugo, ili waweze kutimiza mikataba waliyokubaliana na watu wa uarabuni wa kuwapelekea nyama. Ndiyo maana usishangae kuwaona jirani zetu wakijadali hoja ya Ngorongoro mpaka kwenye bunge lao.
Sasa serikali imefanyaje kutatua tatizo hilo.
5.Serikali iliamua kutenga budget na kuwajengea nyumba ya vyumba vitatu ya matofali ya block, mkoani Tanga, eneo la Msomera, na kuwapa maeneo ya malisho, na mtaji, watu wote waliokubali kuondoka ngorongoro na kuhamia msomera. Lakini ushangae kwamba watu hawataki kutoka pamoja na kupewa nyumba bure yenye eneo la ekari mbili na nusu, pamoja na ekari zingine tano za shamba la kulima pamoja na ardhi nyingine ambayo ni communal land kwa ajili ya malisho.
6.Bado still kila kaya inayohamia Msomera inalipwa mtaji wa shilingi milioni kumi ili iweze kununua mifugo yao mwenyewe.
7. Lakini pia, ukumbuke eneo la Ngorongoro sio eneo la Wamasai peke yao kama wanavyotaka kuwaaminisha watu, wenyeji wa asili pale Ngorongoro ni kabila la Wahadzabe, Wadatoga na Wamasai, lakini haya makabila mengine hayana shida yoyote ya kuhamia Tanga.
Sasa baada ya serikali kuyafanya hayo yote, utakuwa mtu wa namna gani, kuanza kuandika mabango kumchafua Rais na Serikali yake, kama itakuwa sio kwamba watu hawa wana agenda nyingine under the carpet