Uovu na waovu, hawaachwi kusemwa milele. Hitler bado anaishi? Stallin bado anaishi? Id Amin bafo anaishi? Je, hawasemwi?
Ukiwazuia watu kusema ukiwa hai kwa sababu una madaraka ya kuamrisha maharamia yaliyopo kwenye vyombo vya ulimzi na usalama kuwaua au kuwazima watu wasiseme uovu wako, au kukukosoa chochote, maana yake unawaambia wakuseme au ukiwa nje ya madaraka au ukiwa umekufa.
Dikteta marehemu aliwaziba midomo kwa utawala wa mkono wa chuma, hakuna ambaye angemsema au kumkosoa halafu akawa na uhakika wa kubakia salama. Sahizi wanapokuwa huru, ni lazima wamseme, na ni haki yao.
Lakini pia ni jambo jema kuusema uovu tena na tena ili iwe funzo kwa walio hai. Na ndiyo sababu tunaenda kwenye nyumva za kuabudu kila wiki, na wengine kila siku, na nyakati zote hizo, shetani anaendelea kusemwa, na maovu yanaendelea kusemwa na kukemewa.