Ndugu nadhan huo ulikuwa ndo utapeli wa kipind hicho Dar,na mimi nilitapeliwa kwa namna hiyo mwaka 1992 bado nikiwa hata darasa la kwanza sijaanza,mimi nilitumwa na mama,kipindi hiko mzee yupo Arusha.
Nilitumwa na mama dukan nakumbuka nilipewa elf kumi ile ya blue,ile nmetoka kununua kitu cha kwanza ilikuwa nyama natoka buchani niende kwenye kununua vitu vingine nikiwa nimeshikilia chenji,kuna jamaa akaniita akaniamba wewe si una baba yako yupo arusha,nikamjibu ndiyo akaniambia kuna mzigo kanipa niulete kwenu kwa vile nimekuona ngoja nikupe uende nao,na mimi kwavile nilikuwa bado mdogo nikamwamini kwel anamjua mzee.
Basi bana akaniambia lete hizo hela na ile nyama ili anishikie ili nisije kuangusha then akaniambia niende umbali wa mita 300 kuwa kuna mwembe kuna mtu utamkuta atakupa huo mzigo then uje hapa uchukue vitu vyako uendelee na manunuzi mengine ya vitu vilivyobaki.
Nimeenda mpka kwenye ule mwembe sioni mtu,kuulizia watu pemben wanasema hawaelew kinachoendelea,ile kurudi mpka sehemu nilipomwacha jamaa sikumkuta,jamaa alishayeya
Kurudi hom na kilio kumwambia maza haelew,aliyeniokoa nisipate bakora za maza ni bibi aliyekuwa katutembelea,ila jamaa nilikuja kumuona tena.miaka ya 2000 nikiwa sekondari