Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
Mkuu, umekosea sana kuwaita binadamu wenzio MBWA
 
Daaah, zamani ilikuwa ni shiiiida mkuu
shida tupu, shule zilikuwa chache mno hivyo ili uchaguliwe yakupasa ufanye vizuri kweli, tena hususana masomo mazuri kama hisabati na sayansi kwa ujumla wake, ni mazuri na ni matamu ,sio magumu
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya secondary ya serikali. Wachache waliobahatika walijulikana kata/tarafa nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

TABORA BOYS SECONDARY SCHOOL
View attachment 1661676

Juzi kuna mtoto wa jirani yangu alinifuata akaniambia brother ninaomba uniangalizie matokeo yangu ya darasa la saba. Mimi bila hiyana na smartphone yangu hii nikaingia katika website ya necta nikamuangalizia fresh tu. Dogo bwana alipata C flat masomo yoooote.

Nikajua ndio basi tena. Baada ya selection ya shule kutoka nikasikia huyu dogo amepangiwa shule moja ya kata mwendo kama wa dakika 20 kutoka hapa tunapokaa, ndio nikajisemea kimoyomoyo hakika dunia imebadilika kwa kasi sana.

Yaaani mtu anapata C flat bado anaenda secondary? Ninakumbuka dada yangu aliyeniachia ziwa, sasa hivi ni engineer, yeye ni moja kati ya wanafunzi 4 waliofaulu kwenda secondary shule ya serikali. Kumbuka enzi hizo kuchaguliwa tulikuwa tunaita kufaulu.

Yaaani wewe ukichaguliwa unaonekana umefaulu na wale ambao hawakuchaguliwa wanaonekana wamefeli ingawa kiuhalisia hawakuwa wamefeli ila shule zilikuwa ni chache mnoooo kiasi kwamba ni ngumu ku-accomodate wanafunzi wooote waliofaulu.

View attachment 1661678

Dada yangu alifaulu wakati huo baba anafanya kazi Wilaya ya ******* Mkoa wa Mbeya. Watu walifurahi familia nzima, lilipikwa pilau kana kwamba kuna sherehe ya kipaimara. Ndugu waliokuwa wanaishi karibu walikuja kumpa pongezi dada utadhani labda amejifungua mtoto.

Dada alikuwa maarufu sana kwa maana akiwa anaenda shuleni basi ni yeye tu ndiye aliyekua anaonekana asubuhi amevaa sare wakati huo wenzake aliomaliza nao darasa la saba bado wamelala au wameenda shambani.

Mgeni aliyekuwa hapafahamu nyumbani akiwa anaulizia kwa mama fulani wenyeji wanaanza kudadisi kwa kuambiana "au yule mama mjaluo ambaye mwanae anasoma secondary". Kwenda secodary ya serikali ilikuwa ni umaarufu kama dereva kwa maana enzi zile hakuna gari ya automatic transmission.

Gari zote ni manual na anayeweza kuendesha ni mzee mmoja au wawili tu mtaa mzima. Wanafunzi wa secondary walikuwa maarufu kama madereva kutokana na uchache wao.

View attachment 1661682

Matokeo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa sana kwa maana matokeo na selection zilikuwa zinakuja kwa pamoja tofauti na sasa hivi ambapo matokeo yanaanza kutoka na mwanafunzi au mzazi wake anaingia katika internet kisha baada ya mwezi mmoja mbele ndio selection inatangazwa.

Je, wewe ni mmoja ya wanafunzi wachache waliobahatika miaka ya 1990?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Aisee umenikumbusha Mbali Mkuu
Nakumbuka miaka hiyo ya 1996
Mwezi wa 12 mara paapa jina Langu limetoka Gazetini
Kichwa cha habari majina ya waliochaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu!
Daaa acha Kabisa maana Ilikuwa kila siku naenda Kuangalia Magazeti ola,Siku hiyo Jumamosi asubuhi!
Jina hili hapa nipo na bro wangu aisee ailikuwa Furaha ajabu acha tuu!
Imeisha hiyooo[emoji851]
 
Hiyo iko poa kama ulivyo wasilisha.

Wakongwe hua wanasema hayo yote.

Kwa sisi ambao tuko bado shule kama tunavyo ingia sekondari sana ilichaguliwa shule ya serikali kawaida ila waliopo shule binafsi ndio wanajiona wao ndio wao
Siku hizi secondary bwerere sana mpaka raha
 
Tulipasua vibaya saana....nakumbuka wilaya nzima tulikiwa 15 tu tulijulikana!! Moshi Tech, Bihawana, Msalato, Weruweru; Tabora Boyz / Girls....

Wakati huo elimu under Mwalimu ilikuwa na hadhi...ukiwa form one ukirudi likizo kwenye msiba kijijini basi unakaa na wazee wa heshima eee wazee wastaafu na walimu na watumishi wa Serikali kama katibu kata / tarafa; Mratibu wa Elimu etc
Safi sana mkuu...
 
WAHENGA TU: Kuna mzee mmoja alisoma secondary miaka ya 1970s. Yeye binafsi aliwahi kuniambia kwamba enzi hizo waliokuwa wanasoma shule za secondary za serikali walikuwa wanaheshimika sana ukilinganisha na wale waliokuwa wanasoma shule za secondary za binafsi tofauti na hivi sasa ambapo wanafunzi wa private ndio wanaheshimika.

Je, kauli hii ina ukweli wowote ndani yake?
Kabisa nasikia walikua wanaweza kuchaguliwa watu kumi tu wilaya nzima mzee wangu alisoma tabora boys na kumaliza mwaka 1979
 
Back
Top Bottom