Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
Mkuu, umekosea sana kuwaita binadamu wenzio MBWA
 
Daaah, zamani ilikuwa ni shiiiida mkuu
shida tupu, shule zilikuwa chache mno hivyo ili uchaguliwe yakupasa ufanye vizuri kweli, tena hususana masomo mazuri kama hisabati na sayansi kwa ujumla wake, ni mazuri na ni matamu ,sio magumu
 

Aisee umenikumbusha Mbali Mkuu
Nakumbuka miaka hiyo ya 1996
Mwezi wa 12 mara paapa jina Langu limetoka Gazetini
Kichwa cha habari majina ya waliochaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu!
Daaa acha Kabisa maana Ilikuwa kila siku naenda Kuangalia Magazeti ola,Siku hiyo Jumamosi asubuhi!
Jina hili hapa nipo na bro wangu aisee ailikuwa Furaha ajabu acha tuu!
Imeisha hiyooo[emoji851]
 
Hiyo iko poa kama ulivyo wasilisha.

Wakongwe hua wanasema hayo yote.

Kwa sisi ambao tuko bado shule kama tunavyo ingia sekondari sana ilichaguliwa shule ya serikali kawaida ila waliopo shule binafsi ndio wanajiona wao ndio wao
Siku hizi secondary bwerere sana mpaka raha
 
Safi sana mkuu...
 
Kabisa nasikia walikua wanaweza kuchaguliwa watu kumi tu wilaya nzima mzee wangu alisoma tabora boys na kumaliza mwaka 1979
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…