Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Hata iyo c flat kabebwa tu. Matoto ya sikuizi yanamakiza secondary hata hayajui kusoma na kuandika mengine
 
Natafhimini ya ufaulu miaka hiyo unaulizwa shule yenu mwaka Jana imefaulisha wangapi unajibu 20 na we we unashika wa ngapi unajibu kumi bora utafauli ila ukijibu 40 utafeli
 
Safi Sana, naona ulikuwa njema sana Boss, hongera zako

Watano mkoa mzima sio mchezo mkuu. Na hapo ni Dar tu mkoa wa serikali, vp hiyo mikoa mingine? Si unakuta anatoka mmoja tu wa kwenda huko Mzumbe?
Hahah DsM ndio walikuwa wanatoka wengi mikoa mingine mmoja au wawili au hakuna.

Harafu wanafunzi wote mnafahamiana mpk wale wa shule zingine na mikoa mingine maana kila mtu anatoka ameongoza kijiji au wilaya au mkoa.
Unakuta mtu yupo Mzumbe form 4 lakini anawajua wanafunzi wote wa form 4 Ilboru au Tabora huko noma sana wee hacha tu.

Ushindani ulikuwa wa hali ya juu watu special school ukimaliza bila kuwa kichaa shukuru Mungu tu maana unalogwa na kijiji kizima😂😂😂😂
 
Ni kweli
 
Unakuta sanduku la posta hilo moja linatumiwa na watu kibao mpaka ndugu yake na rafiki yako wa kazini...
Simu enzi hizo zilikuwa zile za posta na simu,zile za mezani ikiita mnakimbilia atakae wahi kulipokea,na ukipokea lazima uanze kwa kusema Halooo,shikamoo,nani mwenzangu,sasa ole wako uulize we nani? Utagombezwa mpaka ujute.
WHEN LIFE WAS LIFE.
 
Juzi kuna. Denti nimeonana nae ni mtoto wa jirani yangu nikamuuliza kuhusu matokeo akanijibu wamefauli darasa zima kasoro mmoja nikasema kazi ipo

Hahahaha! Eti kazi ipo, labda mitihani ya siku hizi ni mtelezo.
 
Mwaka gani hiyo mkuu?me 2003 ndiyo nimeanza form 1 hapo arusha secondary school nikitokea Naura primary school.Enzi hizo Arusha kuna shule tano tu za secondary ambazo ni Arusha sec,Arusha day,Kaloleni,Sinoni na Ilboru(hii ilikuwa ya vipaji maalumu)
2003 nipo chuo dogo ,Arusha sec ya headmaster Don king, ilboru nilipafaidi A level kipindi hicho Arusha sec hamna Advance
 
Sera za Elimu zinabadirika.
Kwa sasa "elimu ya msingi" ni mpaka kidato cha nne.
 
Hao Jamaa walio soma enzi hizo waliofanikiwa kujuinga olevel walikua vichwa sana
 
Ni kweli, wakati ule tuliokuwa tunasoma shule za serikali tuliheshimika Sana wale waliokuwa wanasoma shule za binafsi walihesabika kuwa walifeli ndo maana wakaenda kusoma private.
 
Ndio mimi ni mmoja wao. Kati ya wanafunzi 90 tuliomaliza shule ya msingi Magereza Moshi tulichaguliwa wawili (2) tuu kwenda Form I Mawenzi Secondary School.

Najivunia sana elimu ya wakati ule kwani sijabebana na lundo la vitabu wala kuchoshwa na Tuition; walimu walijuma na kutupa NOTES na majaribio yaliyotuwezesha kuwa mahiri.

Elimu ya sasa hivi mtoto wa CLASS II anaandikia vitabu zaidi ya nane, daftari la Class work na Homework anakuwa na mzigo uliozidi umri wake; sijui hawa walimu huwa wanaokotwa wapi maana badala ya kuwapa watoto notes na homework, watoto wanatumia vitabu kama ndio notes.
 
Aisee, kwenye huu uzi kila mtu anasema alifaulu.
Jf raha sana, ukianzisha mada ya magari basi kila mtu atasema analo.
Mkuu member wengi wa JF Wana angalau elimu ya secondary.
Usifikiri wana ongopa.
 
Nilipomaliza darasa la saba, mkoa mzima (yaani na wilaya zake zote) kulikuwa na nafasi 10 tu za kwenda Umenyeni...
 
Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
Vipi wee mbna umeandila kwa jazba sana? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…