Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Kwahiyo kufaulu wachache na kufaulu wengi kipi bora?. Yani kipi bora wachache waelimike au jamii nzima ielimike?. Acheni husda ngoja maisha yawanyooshe
Enzi zetu hakukuwa na kufaulu ilikuwa kuchaguliwa maana shule zilikuwa chache hata hivyo elimu ya wakati ule hiwezi kulinganisha na sasa.Sasa hivi kijana anamaliza form four lakini hawezi hata kuandika "official letter" hata kwa kiswahili elimu imekuwa majanga.
 
Mkuu Infantry Soldier Unaelezea Kufaulu Kutoka Shule ya Msingi? Au Sekondary?
Mi Nakumbuka “Nilipofaulu” Kutoka Shule ya Msingi kwenda Pugu 1995,Na Jina Likatoka Gazetini…Alooo ilikuwa furaha sanaaa,Sababu Unaonja Furaha kwa maravya Kwanza unaona Ufaulu,Ila Kutoka O level kwenda A level tayari imeshazoeleka
Ila Shule ya Msingi ndio kwanza unaenda kuingia Sekondari duuuu,
Halafu Pia Kipindi Kile Eti ukimalaiza Chuo Kikuu unawaza kwenda Eti wanaita “Mlimani”
Ndio watu wanajua umeenda Chuo Kikuu…
Ila sasa hivi Aahh Kwenda Chuo kikuu,Mzumbe,Udom,SUA,TIA nk nk.
Cha Msingi umepata Degree ukatafute ajira,Pia Sasa hivi hawaangalii eti Chuo kikuu umesoma wapi!
Cha Msingi umeweza Itetea Elimu yako kwenye Enterview? Na Katika Kazi husika?
Marahaba Infantry Soldier ingawa Leo hujaamkia wakubwa zako kama ilivyo kaqaida yako emoji3516][emoji2368][emoji3166]
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya secondary ya serikali. Wachache waliobahatika walijulikana kata/tarafa nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

TABORA BOYS SECONDARY SCHOOL
View attachment 1661676

Juzi kuna mtoto wa jirani yangu alinifuata akaniambia brother ninaomba uniangalizie matokeo yangu ya darasa la saba. Mimi bila hiyana na smartphone yangu hii nikaingia katika website ya necta nikamuangalizia fresh tu. Dogo bwana alipata C flat masomo yoooote.

Nikajua ndio basi tena. Baada ya selection ya shule kutoka nikasikia huyu dogo amepangiwa shule moja ya kata mwendo kama wa dakika 20 kutoka hapa tunapokaa, ndio nikajisemea kimoyomoyo hakika dunia imebadilika kwa kasi sana.

Yaaani mtu anapata C flat bado anaenda secondary? Ninakumbuka dada yangu aliyeniachia ziwa, sasa hivi ni engineer, yeye ni moja kati ya wanafunzi 4 waliofaulu kwenda secondary shule ya serikali. Kumbuka enzi hizo kuchaguliwa tulikuwa tunaita kufaulu.

Yaaani wewe ukichaguliwa unaonekana umefaulu na wale ambao hawakuchaguliwa wanaonekana wamefeli ingawa kiuhalisia hawakuwa wamefeli ila shule zilikuwa ni chache mnoooo kiasi kwamba ni ngumu ku-accomodate wanafunzi wooote waliofaulu.

View attachment 1661678

Dada yangu alifaulu wakati huo baba anafanya kazi Wilaya ya ******* Mkoa wa Mbeya. Watu walifurahi familia nzima, lilipikwa pilau kana kwamba kuna sherehe ya kipaimara. Ndugu waliokuwa wanaishi karibu walikuja kumpa pongezi dada utadhani labda amejifungua mtoto.

Dada alikuwa maarufu sana kwa maana akiwa anaenda shuleni basi ni yeye tu ndiye aliyekua anaonekana asubuhi amevaa sare wakati huo wenzake aliomaliza nao darasa la saba bado wamelala au wameenda shambani.

Mgeni aliyekuwa hapafahamu nyumbani akiwa anaulizia kwa mama fulani wenyeji wanaanza kudadisi kwa kuambiana "au yule mama mjaluo ambaye mwanae anasoma secondary". Kwenda secodary ya serikali ilikuwa ni umaarufu kama dereva kwa maana enzi zile hakuna gari ya automatic transmission.

Gari zote ni manual na anayeweza kuendesha ni mzee mmoja au wawili tu mtaa mzima. Wanafunzi wa secondary walikuwa maarufu kama madereva kutokana na uchache wao.

View attachment 1661682

Matokeo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa sana kwa maana matokeo na selection zilikuwa zinakuja kwa pamoja tofauti na sasa hivi ambapo matokeo yanaanza kutoka na mwanafunzi au mzazi wake anaingia katika internet kisha baada ya mwezi mmoja mbele ndio selection inatangazwa.

Je, wewe ni mmoja ya wanafunzi wachache waliobahatika miaka ya 1990?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
wenye credit wengi walibaki kitaa wenye BCC arts waliouna moto, ccc flat ndio hwakuona nuru yoyote, hesabu ilikamua watu, one of the kings of 99 R.I.P Mwalimu Nyerere, what a lovely year it was. Kaka zetu wao walifutiwa matokeo na kurudia january ya 99, na tukaisolve respect tu paper la hesabu la 96, msiulize kila mtu ashinde mechi zake,
 
Ukweli ni kuwa hapo zamani watu wengi wamekosa nafasi ya kusoma secondary school sio kwa sababu ya kutofaulu bali sababu ya uchache wa shule za sekondari.

Unakuta wilaya nzima kuna shule moja ya sekondari halafu shule za msingi zaidi ya120.Ilikuwa jambo la kawaida kukuta shule yote haijatoa hata mwanafunzi mmoja wa kujiunga kidato cha kwanza.

Kwa kweli aliyeleta shule za kata alifanya jambo la maana sana pamoja na changamoto zake. Kujivunia ule uzamani ambao uliwanyima wenzetu nafasi za kusoma na sababu kubwa ikiwa ni ukosefu wa shule za sekondari unakuwa sio uzalendo
[emoji16][emoji16][emoji16]
 
WAHENGA TU: Kuna mzee mmoja alisoma secondary miaka ya 1970s. Yeye binafsi aliwahi kuniambia kwamba enzi hizo waliokuwa wanasoma shule za secondary za serikali walikuwa wanaheshimika sana ukilinganisha na wale waliokuwa wanasoma shule za secondary za binafsi tofauti na hivi sasa ambapo wanafunzi wa private ndio wanaheshimika.

Je, kauli hii ina ukweli wowote ndani yake?
Hadi miaka ya 2002 Hali hiyo ilikuwepo.

Binafsi nilifaulu peke yangu Jimbo Zima la Mbozi Magharibi sasa Wilaya ya Momba kwenda shule ya bweni
 
Uchache wa Sekondari enzi hizo ndio lilisababisha hilo zengwe

Upatikanaji wa kitu kikiwa kidogo na mahitaji ni mengi kinapanda thamani
 
Back
Top Bottom