Baada ya kumaliza kidato sikupata chuo. Migodi mikubwa ndio ilikuwa imeanza kufunguliwa nchini.
Mimi nikaona isiwe tabu nikaenda Kakola mkoani Kahama kusotea kazi. Kazi zilikuwa ngumu sana kupatikana. Kama huna konection unasotea huku ukiishi kwa kuvunja magoti wanaotinga.
Nilivyooona Mambo magumu ikabidi niende Geita. Hapo mambo hayakuenda vizuri. Japokuwa niliitwa kufanya interview lakini nilifeli screen test.Waliowahi kusotea watanielewa.
Nikawa nakaa geto na jamaa zangu, tulisoma nao O level
Mmoja alikuwa anatinga na ishu zake binafsi..
Siku mmoja kuna jamaa alikuwa anasotea pamoja na mimi akaniambia ni msindikize kuchukua mizigo yake. Nikawa nimemsaidia kubeba briefcase yake nikawa nimetangulia kutoka maeneo ya Bomani kuelekea jirani na uwanja wa mpira wa Kahangalala. Ghafla nikavamiwa na watu wakanikata mkononi mara mbili akaja jamaa mmoja baadae nilikuja kumjua kuwa anaitwa Rama. Akajaribu kunisaidia nae wakamkata mkononi. Wakapora ile briefcase. Ilikuwa na vyeti vya jamaa vyenye level ya Ftc.
Mpaka leo sijatoboa mambo magumu nauza Kangala tu. Nimetafakari maisha ni Safari ndefu
Mwaka 2004 nilikula pasaka nikiwa ninamajeraha makubwa sana.