Mwaka 2023 Waziri Ummy amepigwa attacks za kimyakimya sana

Yaani watu kusema wajawazito wanajifungulia chini, hakuna madawa hospitalini inakuwa hujuma. Ndugu hebu mkatibiwe hosp za Serikali huko muone. Mkitibiwa private huko mnahisi hakuna shida. Hizo hoja zinajibiwa kisiasa tu.
 
Soma bro ata mwongozo wa mpya wa NHIF utaelewa kuwa sio msimamizi mzuri wa WIZARA,wanufaika wa bima wataumia sana japo wanachangia pakubwa,bias Kwa watoa huduma wanatengwa wa serikali kuu na serikali za mitaa japo kiwango Cha elimu Kiko sawa,siasa za matibabu kule Kwa wajawazito na wazee japo hazitekelezeki,vituo vya afya vingi visivyo na watoa huduma,,tuachie hapo kiujumla ni msanii
 
Tatizo alikuwa na kiburi pamoja na kutaarifiwa baadhi ya matatizo na wananchi wenye nia njema yeye ama anakaa kimya au anafanya mashambulizi ya maneno yakionesha taarifa alizopewa ni za uongo.

Kiburi huwa kina mwisho wake. Angeiga mtindo wa waziri wa jinsia, watoto na makundi maalum oangepeta sana lakini kutokana na namna walivyokuwa wanadhani wanatoka jamii ya Tanga asingepata ajali ya kisiasa. Kwanza Tanga mjini hawamtaki kabisa ni bora angerudi tu alipokuwa mwanzo kule Korogwe maana huko ndiko alikoibuliwa na JPM hadi kuwa waziri.
 
Tanga Mjini hawamtaki kwanini ?
 
Vipi kuhusu ufisadi na kifeli kwa NHIF ni uongo au ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…