Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 2,858
- 5,123
Mwaka juzi niliona maiti ya mwanaume ikiwa imesimama nyuma ya muuza chakula kwenye mgahawa fulani.
Ilikuwa ni mgahawa mmoja huko Tanga nilikuwa nimeenda kula. Rafiki yangu alinishauri kula hiyo sehemu kwa sababu chakula chao ni kitamu sana.
Kwa kuwa hoteli niliyokuwa nimefikia ilikuwa karibu na huo mgahawa alinishauri nipite hiyo sehemu nikaonje chakula chao. Nikamwambia nitafanya hivyo. Jioni nilienda kuona hiyo sehemu ilivyo na pia ili nile chakula cha usiku.
Nilipo ingia tu kwenye ule mgahawa, nilihisi hisia za ajabu na uwepo wa kitu kisicho cha kawaida. Ilikuwa ni kama nimeingia makaburini. Nilihisi hivyo bila kujua kwa nini.
Nilika kwenye kiti, mhudumu akaja kuchukua oda yangu. Nilimwambia ninachotaka, kisha akaondoka.
Nilipokuwa nasubiri chakula changu, niliangalia kwa makini macho yangu ya kiroho yakafunguka.
Niliona maiti ya mwanaume ikiwa imesimama nyuma ya mwanamke aliyekuwa anapakua chakula. Huyo Mwanaume alikuwa na madoa ya ajabu kwenye nguo zake na alama isiyo ya kawaida mdomoni. Ilikuwa ni maiti halisi. Kwa sura yake, ilikuwa kama anaoza taratibu.
Huyo mwanamke alichota chakula na kumwambia muhudumu atafute sijui kitu fulani, yule binti akawa bize na kile kitu yule ma a akaamua kunihudumia mwenyewe.
Aliponikaribia, roho ya yule mwanaume ilimfuata. Hapo nilijua kuna tatizo na kwamba alikuwa anafuatwa na roho ya mtu aliyekufa.
Nilimwita pembeni na kumuuliza kama anajua kuna mwanaume anayemfuata nyuma. Kutokana na uso wake, nilijua alikuwa anajua, lakini hakutaka kuongea. Alikana kujua ninachomaanisha, na mimi sikumlazimisha aendelee kuongea.
Sikuweza kula kile chakula tena. Dr dogoli kinyamkela nililipa chakula na kuondoka bila kula. Baadaye nilimuuliza rafiki yangu maswali kuhusu yule mwanamke wa ule mgahawa.
Aliniambia kuwa mume wa yule mwanamke l alikuwa amefariki miaka mitatu iliyopita. Ingawa baadhi ya watu waliomjua huyu mwanake na mume wake walihisi kwamba alimwua mumewe waje mwenyewe, na akaulaumu kifo hicho kwa watu wasiojulikana waliodaiwa kumchoma kisu kifuani hadi kufa.
Nilitabasamu.
Baada ya maelezo yake, nilielewa kwa nini mzimu wa marehemu mume wake ulikuwa unamfuata kila mahali, na nikatambua kwa nini alikuwa anaogopa kuzungumza. Alikuwa anehusika moja kwa moja na kifo cha mume wake na alikuwa anateseka kimya kimya kwa sababu ya mateso ya hiyo roho.
Nilijua ilikuwa ni suala la muda tu apate ukichaa, akiri, au atafute msaada. Nilikuja Tanga mwaka huu kwa safari ya kikazi nikakuta ule mgahawa umefungwa. Niliambiwa yule mwanamke alijinyonga.
Ningemsaidia kwa namna fulani, endapo tu angefunguka na kusema ukweli. Ningeweza kumsaidia kabisa. Jina langu ni xxxx , nina uwezo adimu wa kuhisi, kuona, na kuwasiliana na viumbe wa ajabu bila kupata madhara yoyote.