Mwaka wa 9, Sijawahi kumuona mtu mwingine akitumia JamiiForums

Mwaka wa 9, Sijawahi kumuona mtu mwingine akitumia JamiiForums

Jf ukiuliziq watu ni kama hakuna wanachokijua ila wengi wanaitumia
 
Fake ID zinasaidia sana mimi humu kuna ndugu wengi na hatujuani, kuna diwani mmoja wa CCM nilinasa ID yake ye yupo jukwaa la mahusiano tu siasa hayupo
Humu waliokuwa jukwaa la siasa wala sio wanasiasa, wanasiasa wenyewe wako MMU hawataki stress washajitafuta wamejipata 🤣🤣🤣 Countrywide njoo umuone diwani anashinda MMU
 
Soon ntabadilisha ID mana mambo yangu yote yatakuwa hadharani...mana kwa kusema watu na utajiri nilionao wata niua bure mtaani
Badili kma mimi tu
Nitahakikisha hi id siwasiani na mtu ng’ooo
 
Ni mwaka wa ku 9 tangu Nilipoanza kuutumia huu mtandao lakini sijawahi kukutana na mdau wa mtandao huu.

Leo nimejaribu kuwauliza colleagues Kama wanaufahamu, wote walikiri kuufahamu lakini wakasema hawautumii.

Nikajiuliza iwapo ni kweli au wanaficha privacy zao. Je, uliwahi kumuona mtu live akitumia JamiiForums?
Umewahi kuwaona majini?Ndiyo members wa JF!Ngumu kuwaona mpaka waweke utambulisho wao wa kweli au waamue tu uwafahamu.
 
Mwaka wa saba huu natumia JF. Kuna watu kama watatu nimewaona wanatumia JF.

Wawili niliwaona kwenye daladala, wengine wanne nafahamiana nao kabisa mmoja hadi Id yangu anaijua.

Ila nilichogundua watumiaji wengi wa JF hawako comfortable kabisa kujulikana wanatumia huu mtandao. Maana kati ya hao jamaa ninaowafahamu, mmoja tu ndiye aliyenitajia ID yake. Wengine walificha kabisa. Na huyo aliyenitajia ID yake siku hizi haifanyi kazi iko dormant, na alikuwa anauponda kwamba ni mtandao wa wazee hauna vibe.

Mwisho, salamu kwako wewe dada, juzi kati hapa ulikuwa kwenye daladala Mwanza, ya kutoka town kwenda Kisesa mida ya jioni ulikaa na sister wako fulani mweupe. Niliona simu yako inaingiza notification za JF.

Wewe dada ni mgeni ndio kwanza siku hiyo umetoka kwenu Dodoma, ukawa unaponda eti Mwanza ni pabaya halafu Dodoma na Arusha ni pazuri. Hivi hiyo Dodoma unayoisifia kwamba ni nzuri kuliko Mwanza ndio hii hii ninayoijua mie, ambayo haifiki hata nusu ya ukubwa na uzuri wa Mwanza au nyingine?

Njoo dm nikutembeze nikuonyeshe uzuri wa Mwanza, kama bado upo.
 
Back
Top Bottom