Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Kwanza hakuna sehemu yeyote Duniani ambako kila mtu anaweza kujiajiri,Ili uzalishaji afanye nani Sasa?
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ we ni mwalimu!?
Inawezekana katika kuleta hii mada nikawa nimewatoa matongo tongo watu wengine, kwa hiyo nakuwa kama nimefundisha.
Mtu yeyote anayetoa wazo la kujenga, huyo ni mwalimu wa kuzaliwa/kipaji.
 
Kwa sisi waTz weusi hawa ni 99%
Watu wengi wana Illusion kwenye suala la kujiajiri na mwisho wa siku waanzisha tuvitu tudogo tudogo ambavyo sio sustainable.

Biashara nyingi sana za kujiajiri nilizoziona hapa Tanzania kwetu ni za kiulanguzi na sio za uzalishaji na hazina sustainability.

mfano watu waliojiajiri maduka ya nguo Kariakoo mwaka 2024, yaani internet inakuwa lakini bado wao hawajaona hili.

Kingine huwezi kufanikiwa kwenye biashara kama huwezi hukufanikiwa kwenye ajira, kama huna nidhamu, matumizi ya mabaya ya pesa usikurupuke kujiajiri
 
Kujiajillri inahitaji Uthubutu kwa kuwa njia yake sio rahisi na matokeo yake ni ya mda mrefu.

Binadamu hatufafanani, Suala la Uthubutu sio la kila mtu, Dunia yote inafahamu hilo.
Ni kweli matokeo ya kujiajiri ni ya muda mrefu, na wengi tunashindwa kwa kutaka matokeo ya muda mfupi
 
Hata biashara hatuwezi kufanya wote kwa namna yeyote ile, hata tukifanya watu wengi watafeli.

Walioajiriwa kupitia mishahara ,posho ndio wanaongeza mzunguko wa pesa mitaani kwa wafanyabiashara.
Na waliojiajiri walikuwa wanawaza hivi kweli?
 
Biashara nyingi sana za kujiajiri nilizoziona hapa Tanzania kwetu ni za kiulanguzi na sio za uzalishaji na hazina sustainability.
Ni kweli kutegemea biashara ya ulanguzi katika kujiajiri ni ngumu; ila kwa yule aliyewekeza kwenye mashine/mitambo ya uzalishaji huyu ni rahisi kujiajiri kwa sababu anatengeneza na kuuza.
Lakini wapo watu wenye hiyo mitaji, kwa nini hawafanyi; tatizo ni nini, elimu au uwoga?​
 
Unaruhusiwa kutoa maoni yako, kwa nini hatujiajiri huku mtaji ukiwa si tatizo?
Kujiajiri kiukweli ni kuajiriwa na wateja wako!! Wateja ni wafalme!! Utalaziomika kuwasikiliza na kuteleleza wanayotaka!! Kiuhalisia ni kwamba kujiajiri ni kuajiriwa na wateja!! Wateja ndo mabosi na waajiri wako!! You are not free!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…