Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Kinachoamuwa maisha yetu ni maono ya mtu. Huwezi kujiajiri ukubwani kama hujawahi kuwaza kufanya hivyo ukiwa katika umri wa chini ya miaka 20.
Kama hujui unachotaka, hutapata unachokitafuta.
Niliamuwa kuacha kazi na kujiajiri ili kutimiza maono yangu toka nikiwa mtoto. Nilichukia sana maisha ya umaskini na njia pekee niliona itanisaidia ni kujiajiri tu.
Nilipita kwenye ajira ili nione jinsi system inavyofanya kazi.
Mwajiriwa mwenye kipato kizuri kwa asilimia kubwa lazima awe ameiba
 
Shida kubwa ni Elimu yetu inatulaza usingizi sana, yaani Mtu unatumia miaka mingi kuwaza namna ya ku-score A's tu katika masomo, ukirudi likizo tusheni, nyumbani homework ya masomo ya darasani. habari za ujasiliamali hujishughulishi nazo.

Na hayo masomo bora hata yawe yanalenga ktk ubunifu, kupata pesa na kutengeneza faida kupitia hiyo pesa, kukuza uchumi unakuta ni nadharia fulani za kukaririshana tu basi mtu anazidi kuwa mgeni na mazingira halisi.

Kwangu Mimi shida kubwa ni mifumo yetu ya elimu inalaza watu usingizi.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
Hao wanaojiajiri wamesomea wapi?
Ukweli watu wengi hawana maono toka utotoni bali tunakimbazana kwa kusoma kozi ambazo ni rahisi kuajiriwa.
Tuna system mbovu kutoka kwenye familia zetu.
 
Hao wanaojiajiri wamesomea wapi?
Ukweli watu wengi hawana maono toka utotoni bali tunakimbazana kwa kusoma kozi ambazo ni rahisi kuajiriwa.
Tuna system mbovu kutoka kwenye familia zetu.
Uko sahihi, kwa sababu familia zilizotoka kwenye biashara na kupata elimu uwa wanajikita pia kwenye biashara
 
Levels mzee, kuna vibarua, wafanyakazi na waajiriwa.

Ukiwa kwenye makundi mawili ya kwanza hayo ni vizuri ukapambana kujiajiri tu.

1.Vibarua hawana mikataba rasmi hawa boss akinuna akasema usije ujue ni mateso bila chuki. Mara nyingi vipato vyao havitoboi laki 3 kwa mwezi mzima. Hamna muda maalum wa kutoka kazini ila saa 12 asubuhi lazma uwepo eneo la kazi 😂😂😂 na mazingira ya kazi ni magumu.

2. Wafanyakazi hawa hawana tofauti sana na vibarua isipokuwa muda wa kuripoti wengi huwa saa 2 asubuhi na kutoka saa 11 jioni na wanaenda hadi siku ya Jumamosi. Kipato chao range ni laki 5 mpaka 2M kwa waliobahatika kupata ofisi nzuri. Hawa sifa yao kuu ni kudaiwa kila kona mikopo mikopo tu alimradi. Wapo wanajitutumua na vimikebe vya mtumba toka japani na kujiona wamewin sana ila hamna kitu wanatubu sana kitaa.😂

3. Wenye ajira, kiukweli ukiskia kijana amepata ajira jua tu kwamba amefanikiwa kuukimbia umaskini kwa ghafla mno kama mwanga wa radi. Hawa wengi unakuta wako kwenye Taasisi nyeti kama TCRA, TPDC, Mifuko ya hifadhi ya jamii ambako level ya mshahara si chini ya 4M kwa kuanzia tu na safari nyingi zenye per diem mlima na dili nyingi za mkwanja mrefu, hali kadhalika makampuni makubwa ya binafsi kama GGM au Barrick Gold ambako watu wanalamba 8 figures za madafu. Hawa ofisini huwa ni saa 3 mpaka saa 9 wanafunga siku😀 na benefits zote hupewa kuanzia bima kubwa ya familia, transport, communication na hata schoolfees za watoto. Hawa waajiriwa wengi ndio husukuma vyuma vya kibabe kwa 0kms na ndo juzi kwenye speech mzee wetu Jenerali ulimwengu aliwagusia kama huna disposable income walau ya 5M kwa mwezi usijitwishe gari litakutesa.

Kwahio tujichekeche tu ndugu zangu. Maswala ya kujiajiri yana mantiki kwa vibarua na wafanyakazi. Walioko kwenye level ya ajira wanaweza ku make it in life easily kuliko hata wanao hustle kupambana na kero za TRA,OSHA,FIRE, Manispaa na wengineo wengi.

I couldn't agree more.
 
Kwamba watu wote kwenye economy hii wawe self employed, mfano Mbeya yote wawe wakulima, no need of teachers, doctors, nurses, engineers etc, tambua kuwa services are intangible goods are included in measuring national income, hata hizo capitalist countries still there's a large number of people who are employed in different sectors of the economy [emoji3]
 
Kwamba watu wote kwenye economy hii wawe self employed, mfano Mbeya yote wawe wakulima, no need of teachers, doctors, nurses, engineers etc, tambua kuwa services are intangible goods are included in measuring national income, hata hizo capitalist countries still there's a large number of people who are employed in different sectors of the economy [emoji3]
Unatusaidiaje katika kujenga kiwanda cha sukari, kuchimba mafuta n.k?
 
Leo nimetoka intervierw,ya kufundisha tu nimekutana na mtu anaexperince ya 8 years mmh nikasema kweli life kitaa sio
Inawezekana alikopata elimu, walikula ada zake badala ya kumjengea uwezo wa kujiajiri
 
Wee fala nini unajua utamu wa kuajiriwa tena serikalini..?
No pressure full job security na uhakika wa mshahara na allowance za hapa na pale...
Kujiajiri ni kipaji kama ilivyo football au mziki
 
Tunaamini elimu tunayoipata huko vyuoni na mashuleni, inatupa uhuru wa kufanya maamuzi sahihi katika uzalishaji mali pamoja na kujitegemea.

Tulitegemea ujuzi na elimu ulioipata huko duniani n.k iwe chachu ya wewe kujijenga na kuanzisha na kumiliki kampuni, taasisi, au kiwanda ili pia iweze kutoa ajira kwa wengine.

Mtaji kwako sio tatizo, kwa sababu umeshaajiriwa kwa miaka mingi na una sifa zote za kukopa; Swali, kwanini unashindwa kujiajiri?

Tatizo ni nini?​
Wote tukijiajiri nani ataajiriwa?
 
Back
Top Bottom