Mwaka wa nne huu naishi Mbeya, Wanyakyusa nawapa maua yenu japo mna mapungufu machache

Mwaka wa nne huu naishi Mbeya, Wanyakyusa nawapa maua yenu japo mna mapungufu machache

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kwanza kabisa ieleweke mkoa wa Mbeya kuna makabila mengine kama wasafwa, wandali, wamalila, n.k. Ila wageni wengi huwa tumekariri wanyakyusa sababu ndio main tribe kwa kigezo cha umaarufu, mifano mingine Ruvuma main tribe ni wangoni ila kuna wamatengo, Mara main tribe ni Wakurya ila kuna wajita, Njombe main tribe ni wakinga ila kuna wabena, n.k.

Wanyakyusa kwa haraka haraka naweza kusema ndio kabila linaloongoza kwa wasomi wengi, viongozi, watu kwenye system, n.k. Kwa Tanzania ukiigawanya mara mbili ile mikoa ya chini.

Inshort wanyakyusa kwa uzoefu wangu ni watu wakarimu zaidi tena kwa vitendo na hakuna maneno ama kutangazwa ukishasaidiwa.

Nimeshakwenda ofisi flani nikiwa mgeni wa mifumo ila kuna mbaba wa kinyaki alinisaidia a to z utadhani mimi mtoto wake, nilishangaa sana.

Suala la msosi wa wanyakyusa wala si taabu, utakula vizuri tu labda wasipike ubwabwa wapike ndizi

Ni wacha Mungu hasa kwa upande wa wanawake, Mbeya ni mkoa unaoongoza kwa makanisa mengi mitaa ya Nzovwe kunaitwa Nigeria sababu kuna nyomi la makanisa, wingi huu umeweza kuwafanya wanyakyusa kuwa mstari wa mbele kutoa waimba gospel na wachungaji wengi katika ngazi ya taifa (japo kuna wimbi kubwa limenza kutanda la wachungaji matapeli wanaonenepea sadaka).

Wanyakyusa wanathamini sana elimu kwa lengo mtoto aje apate ajira, Mbeya ni sehemu ya pili hapa Tanzania kwa kuwa na vyuo vingi nyuma ya Dsm. Ni Kabila la nne kwa wasomi nyuma ya wahaya, wachaga na wasukuma (kuna wasukuma milioni 16 wana asilimia ndogo ya wasomi ndani ya jamii yao lakini hio asilimia ni idadi kubwa kitaifa)

MAPUNGUFU YAO...

Rundo la ndugu.. Kwa kawaida ndugu inabidi wawe wale mliozaliwa nao na wale wa upande wa wazazi kina mjomba, shangazi, ma mdogo, ba mkubwa, Pamoja na watoto wao, kwa wanyaki wamevuka, hata mjukuu wa mke wa pili wa bamdogo wa babu bado ni ndugu, ubaya wa hapa ndugu wa mbali huweza kushawishika kuingia kwenye mambo ambayo sitayaelezea ila watu wa huko wanayajua,

Ukabila - kwenye fursa / nafasi za kazi huwa hawawezi kuficha udaifu wao wa ukabila / tribalism, mnyakyusa akishika madaraka mfano umeneja au cheo cha kuajiri, kigezo kizito kwake ni kuwa kabila moja kisha vingine vitafuata, ukichanganya na kuwa na ndugu wengi ni janga.

Wanawake kujali zaidi ndugu kuliko mme, huna sauti mbele ya ndugu zake, inaweza kuelekweka kwa ndugu wa damu lakini kinachokera ni hadi wale ndugu wa mbali kina mjukuu wa bamdogo wa babu, jambo la ndugu kwanza wewe wa pili.

Ubabe kwa baadhi ya wanawake ni tatizo, na hasa ukizingatia wengi wana miili ile oiginal ya kibantu yenye afya ukiwa legelege usije ukajaribu kutumia violence, utaaibika !! Wao wanataka muwe sawa na hii inaleta taabu wao kumnyenyekea mume, wao hujisifu kwa kuchanganya ni msimamo au kukataa kuendeshwa ila ni ubabe na kiburi.

Kwenye nyumba mama ndie mwenye sauti - hii ni kawaida sana kwenda nyumba yenye mama mnyakyusa uki observe utagundua mama ndie kashikilia usujkani ama kuna usawa kwenye utawala wa nyumba.

Wengi wana uwezo mdogo kusimamia biashara sababu ya kuingiza undugu usio na mipaka kwenye biashara, mtu ukifanikiwa kidogo tu kwenye biashara ndugu huanza kukuelemea na nilichogundua wana uoga wa kuwawajibisha ndugu kwa hofu ya kusemwa na ndugu wengine. Ndio maana wengi hupendelea ajira ambazo serikali huwalipa mshahara, Ni wazi hata ukienda Mbeya biashara kubwa zimeshikiliwa zaido na wageni hasa wakinga.

Ni hayo tu lakini kwa ujumla wanyakyusa wapo juu.
 
Kuna kabila la Wasukuma...

Hili kabila tulifungwa kamba Sana, huwezi kubali mpka ufike unyantuzuni ndio utakubali...., kwa mda mfupi tuu ila sina hamu na wale watu.

Najua ndio mnaongoza kwa kua wengi humu mtaniandama, na mlivyo wachawi mnatamani muitoe hii ID kafara.

Ukabila upo sehemu nyingi ila hawa wamezidi, Wanapenda kunyenyekewa, roho mbaya.

Potelea kote, lawama hapewi mbuzi.
 
Kuna kabila la Wasukuma...

Hili kabila tulifungwa kamba Sana, huwezi kubali mpka ufike unyantuzuni ndio utakubali...., kwa mda mfupi tuu ila sina hamu na wale watu.

Najua ndio mnaongoza kwa kua wengi humu mtaniandama, na mlivyo wachawi mnatamani muitoe hii ID kafara.

Ukabila upo sehemu nyingi ila hawa wamezidi, Wanapenda kunyenyekewa.

Potelea kote, lawama hapewi mbuzi.
Nakuunga bro! Niliona mnyatunzu bro hawa watu sio poa kabisa aisee kilichotokea mungu anajua zaidi
 
Bora Siku hizi wamepunguza kuomboleza Msiba.

Miaka ya Nyuma ilikuwa Wanyakyusa wanakaa Siku 40 wakiomboleza Msiba.

Ilifikia kipindi Serikali ikaingilia kati maana ilikuwa inaathiri Uchumi wao.

Huwezi ukakaa Siku 40 Ukilia Msiba bila kwenda kwenye shughuli zako za Kiuchumi
 
Nitajie wasanii Wakubwa 5 wanaotoka Mbeya ukiachana na Rayvany?????
Gospel karibu 80 percent

Legends wa bongo fleva kuna AY, MiKE TEE, Caz T, Enika, kwa kizazi cha sasa kuna kina Ray Vanny.

Producers legends wa bongo fleva kuna Roy wa g-recordz na amba wa Iringa wasanii kibao wa dsm wanafunga safari kutengeneza hits.
 
Point ya msingi hujaigusa kabisa je kuna madem wazuri? Kwa umri wanguu huu hilo ni jambo la muhimu kujua
 
Point ya msingi hujaigusa kabisa je kuna madem wazuri? Kwa umri wanguu huu hilo ni jambo la muhimu kujua
Wazuri mkuu, shepu za kibantu pro utazipata kwa wanyakyusa wa Rungwe, kama weupe ndio ugonjwa wako wapo wanyaki wa Kyela.

Ukinasa kwenye penzi la mnyaki ni ngumu sana kuchomoka, ndugu wanaweza kudhani umerogwa
 
Back
Top Bottom