Kwanza kabisa ieleweke mkoa wa Mbeya kuna makabila mengine kama wasafwa, wandali, wamalila, n.k. Ila wageni wengi huwa tumekariri wanyakyusa sababu ndio main tribe, karibu kila mkoa una main tribe wageni hawajui sub tribes, Ruvuma main tribe ni wangoni ila kuna wamatengo, Mara main tribe ni Wakurya ila kuna wakwaya, Njombe main tribe wakinga ila kuna wawanji, n.k.
Wanyakyusa kwa haraka haraka naweza kusema ndio kabila linaloongoza kwa wasomi wengi, viongozi, watu kwenye system, n.k. Kwa Tanzania yote ya kusini ukiigawanya vipande viwili ukiondoa dsm.
Inshort wanyakyusa kwa uzoefu wangu ni watu wakarimu zaidi tena kwa vitendo na hakuna maneno ama kutangazwa ukishasaidiwa.
Nimeshakwenda ofisi flani nikiwa mgeni wa mifumo ila kuna mbaba wa kinyaki alinisaidia a to z utadhani mimi mtoto wake, nilishangaa sana.
Suala la msosi wa wanyakyusa wala si taabu, utakula vizuri tu labda wasipike ubwabwa wapike ndizi
Ni wacha Mungu hasa kwa upande wa wanawake, sehemu kama mitaa ya Nzovwe kunaitwa Nigeria sababu kuna nyomi la makanisa, wingi huu umeweza kuwafanya wanyakyusa kuwa mstari wa mbele kutoa wachungaji wengi na waimba gospel katika ngazi ya taifa.
Nikiwa mwizi kichapo kikinizidia ntakimbilia kwa wanyakyusa at least ntapata dozi ya kati kisha nipelekwe polisi, nikizubaa naweza kukatwa mapanga
Wanyakyusa wanathamini sana elimu kwa lengo mtoto aje apate ajira, Mbeya ni sehemu ya pili haoa Tanzania kwa kuwa na vyuo vingi.
MAPUNGUFU YAO...
Pamoja na hayo mapungufu yapo na hayo ni:
Rundo la ndugu.. Kwa kawaida ndugu inabidi wawe wale mliozaliwa nao na wale wa upande wa wazazi kina mjomba, shangazi, ma mdogo, ba mkubwa, n.k. Pamoja na watoto wao Ila wanyaki wamevuka, hata mjukuu wa mke wa pili wa bamdogo wa babu ni ndugu,
Ukabila - Wanyakyusa kwanza wengine msubiri, Kwenye fursa / nafasi za kazi mnyakyusa akishika madaraka ni kawaida kujaza wanyakyusa wengine, ukichanganya na kuwa na ndugu wengi ni shida hio, mlolongo ni mrefu sana.
Wanawake kujali zaidi ndugu kuliko mme, huna sauti mbele ya mwanamke linapokuja suala la ndugu zake hata awe mjukuu wa bamdogo wa babu.
Ubabe kwa wanawake, mtu anaweza kuwa na mapungufu bila yeye kujua, wengi huchanganya ubabe na msimamo, ni vitu viwili tofauti.
Ni hayo tu lakini kwa ujumla wanyakyusa wapo juu.