Mwakinyo anasulubiwa na watesi wake

Mwakinyo anasulubiwa na watesi wake

Sijui kwa Nini nawachukia sana vibaka, kwangu Mimi Bora jambazi kuliko kibaka/mwizi. Yule dogo kwa maelezo yake tu inaonesho ni kibaka mzoefu na bila shaka mwakinyo alimkamata akiwa anaiba.
Wewe unaweza kuokota nazi shambani kwa mtu? Tena nazi 6?

Watanzania tumejaa unafiki mtupu, Leo hii nani anaweza kumkamata mwizi nyumbani kwake na akamuacha bila hata kumgusa? Nani asiejua ukatiri wa Hawa vibaka wakikutaiti? Raha yenu mlitaka msikie mwakinyo amevamiwa na vibaka wamemjuruhi kwa visu na mapanga ndio mfurahi?...!! Eeeh maana mngepata story ya kuondokea kwamba bondia Gani anapigwa na vibaka'!! Wanafiki wakubwa nyie....!!

Mwakinyo anakesi nyingi tu za kuibiwa vitu vyake hapo nyumbani kwake na ametoa taarifa mara kadhaa polisi na hata kwa mwenyekiti wa mtaa wake, amelalamika mara kadhaa kuibiwa betry za gari,vifaa vyake mazoezi na tairi za magari ,Tv n.k . Sasa nyie mnao mtetea kibaka mwenzenu ambae amekiri kuiba. punguzeni chuki kwa mwakinyo!! Hakuna mtu Tanzania hii ambae anaweza kumkamata mwizi wa mali zake alafu akamuacha hivi hivi hakunaaaa!!!!
 
Itakuwa kweli mkuu maana kwa level ambayo alikuwa amefika mwakinyo sio wa kurudi kijijini na kukaa katika maghofu

Unaweza tazama kipindi cha Showbizz cha zamaradi jamaa anaishi katika maghofu na anagombania nazi
Kwa hiyo mnamroga awe zezeta mumnyonye mtakavyo?
 
Big
Na unapokua maarufu au mtu mwenye mafanikio makubwa ktk jamii sifa yako moja ni kujua watu wanakuwinda na watu wwng hawakupendi na wanakutaftia sababu za kukushusha
Sasa ni jukumu lako km mtu maarufu kujikinga na kua makini na watu wa aina iyo

Na ndo maana inashauriwa watu waarufu wawe na vijana wa kaz na kazi zao ndo km izo kupiga watu ata kesi ikitokea watashikwa vijana ila mwakinyo kawa mshamba anaenda kupiga yeye wenyewe badala ya kuachia vijana
Bigup sana mkuu natamani siku mwakinyo apate ushauri wako huu. Inshort Ukiwa na uwezo usiende kuishi katikati ya maskini, hata kama ukiwa unapita na gari unashusha vioo na kuwasalimia ufikili watakupenda, hata kama upite Kila nyumba na kuwapa misaada usifikili watakupenda, always raha ya maskini ni kuona unafanana nae tofauti na hapo unajidanganya tu. Tuupige vita umaskini kwa nguvu zote.
 
I advice Mwakinyo when this stupid case is over, he should seek for nationality in other countries...in Europe maybe
Ulaya hawataki kina Hassani na mudi, labda akomae na Irani, Iraq, Saudi na Yemeni pia sio mbaya
 
Mwakinyo kinachokuponza ni misimamo Yako na lifestyle Yako. Nchi hii kama huimbi mama mama mama! Ama Mama mitano Tena tegemea hata ukiua panya chumbani kwako inaweza kuwa kesi trust me!!

Msiwaone watu maarufu wanajichetua mkafikili hawana akili, wanazo sana. Kinachowafanya wajichetue ni kujihakikisha ulinzi kwa mambo ya kijinga jinga kama hayo.
Kuliko kuwa neutral Bora uchague upande ujulikane kabisaaaa
 
Na unapokua maarufu au mtu mwenye mafanikio makubwa ktk jamii sifa yako moja ni kujua watu wanakuwinda na watu wwng hawakupendi na wanakutaftia sababu za kukushusha
Sasa ni jukumu lako km mtu maarufu kujikinga na kua makini na watu wa aina iyo

Na ndo maana inashauriwa watu waarufu wawe na vijana wa kaz na kazi zao ndo km izo kupiga watu ata kesi ikitokea watashikwa vijana ila mwakinyo kawa mshamba anaenda kupiga yeye wenyewe badala ya kuachia vijana
Hakuna mtu anamchukia mtu hata kimoja ,Mwakinyo anapata support kubwa kwa ndugu zake ..Mengi watu hwaongei ila kama kuna mtu amekaa naye kitaa kimoja wanajua , Mwakinyo anajua kupigana na mkorofi haswa hata mtu awe mkubwa atapambana naye .

Hao wadigo ndiyo walipanda kuja kumsapot huku Dar , hao hao walipata ajali akafa jamaa mmoja anaitwa kiba junior kwa jina la umaarufu ...Hawawezi kumchukia katu ni kujishtukia ,kama unabishi njoo Tanga umkejeli Mwakinyo uone watu watakavyokushambulia .

Jamaa anapendwa zaidi ila ni mkorofi by nature japo kesi imekaa upande mmoja , mwaka jana kesi ya kumvamia yule dogo wa mafia boxing ilizimwa maana angepotea kabisa na baadhi walioandika walifuta, nakuambia hivi kama ulikuwa hujui ..Ni kesi kubwa zaidi ilibidi niseme ili uelewe ..

Mwakinyo sio wa kwanza kwenye mafanikio Tanga hata kwenye career ya boxing wako wengi sana .
 
Sijui kwa Nini nawachukia sana vibaka, kwangu Mimi Bora jambazi kuliko kibaka/mwizi. Yule dogo kwa maelezo yake tu inaonesho ni kibaka mzoefu na bila shaka mwakinyo alimkamata akiwa anaiba.
Wewe unaweza kuokota nazi shambani kwa mtu? Tena nazi 6?

Watanzania tumejaa unafiki mtupu, Leo hii nani anaweza kumkamata mwizi nyumbani kwake na akamuacha bila hata kumgusa? Nani asiejua ukatiri wa Hawa vibaka wakikutaiti? Raha yenu mlitaka msikie mwakinyo amevamiwa na vibaka wamemjuruhi kwa visu na mapanga ndio mfurahi?...!! Eeeh maana mngepata story ya kuondokea kwamba bondia Gani anapigwa na vibaka'!! Wanafiki wakubwa nyie....!!

Mwakinyo anakesi nyingi tu za kuibiwa vitu vyake hapo nyumbani kwake na ametoa taarifa mara kadhaa polisi na hata kwa mwenyekiti wa mtaa wake, amelalamika mara kadhaa kuibiwa betry za gari,vifaa vyake mazoezi na tairi za magari ,Tv n.k . Sasa nyie mnao mtetea kibaka mwenzenu ambae amekiri kuiba. punguzeni chuki kwa mwakinyo!! Hakuna mtu Tanzania hii ambae anaweza kumkamata mwizi wa mali zake alafu akamuacha hivi hivi hakunaaaa!!!!
Kamsaidie sasa mkuu.
 
Mwakinyo hapo anapoishi amepanga,hiyo nyumba ni ya mwanamke mmoja, nyumbani kwao Mwakinyo ni Makorora.Kupiga watu Mwakinyo hajaanza leo,hata huko kwao Makorora anatembeza kichapo kwa watu huku akilindwa kwa sababu ya jina lake
Oya gwangala Geita na Tanga mbona mbali sana
 
Simtetei Mwakinyo ukweli ni kwamba hauwezi kufungiwa kwenye banda la mbwa aina ya Rottweiler wakushambulie alafu utoke hai ufanye na interview.
 
Itakuwa kweli mkuu maana kwa level ambayo alikuwa amefika mwakinyo sio wa kurudi kijijini na kukaa katika maghofu

Unaweza tazama kipindi cha Showbizz cha zamaradi jamaa anaishi katika maghofu na anagombania nazi
Kwenye lile gofu kuna utulivu na amani kuliko palm village ambapo view banda la mpesa na bodaboda.
 
Back
Top Bottom