Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Eti naye ni Dr.....aiseee...ukweli gani atakaoutoa SAA hiz...wakat aliuficha ukweli kipindi kile....anatafuta kiki za kupuuz kabisa....okay najua anataka aseme uongo ili awasafishie watu flan njia 2020....
 
Siasa majitaka
 
Ufisadi wa jpm unaojaribu kutuaminisha hapa ni porojo ambazo ukiambiwa uthibitishe hutaweza, lakini kwa lowasa ni tofauti.......kamati teule ya bunge ilimwaga ushahidi wote ya ufisadi wake!
 
It's obvious ...Mwakyembe hawezi kufanya lolote ....kama Waziri aliyekuwepo katimuliwa kwa kuunda tu tume mnategemea huyu achukue hatua gani kama si upinzani kukosa mbinu ya namna ya kumlazimisha mamlaka ya uteuzi kuchukua hatua ....unaibuaje hoja kama hii kwa mgongo wa issue ya aibu kama Richmond ambayo sasa inaleta ukakasi hata huko Chadema? ....
 
Fukua makaburi kijana
 
Chadema ina ushahidi wa ufisadi wa Lowassa
 
Ni kweli hakuhojiwa hata ujio wake ukawa pia hakuhojiwa ila tumwache mzee apumzike mbona aliyekula nae kapumzika!
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
Wanyakyusa ni kati ya watu wakweli sana, huyu Mwakyembe sijui ni wa aina gani! Ati naye ana Ph.D Kweli mtu akiingia siasa ukoo umtenge kwanza, siku akiacha siasa arejeshwe kwenye ukoo.Kumbe siasa inaendeshwa kwa unafiki na uongo.
 
Namshangaa sana Waziri Mwakyembe eti hakumhoji Mh.Lowassa Kwa kuwa ushahidi dhidi yake ulikamilika.Kama ndio hivyo mbina Ushahidi dhidi ya Paulo Makonda nao ulikamilika? Bw.Mwakyembe wewe ni mwana Sheria kumhoji mtuhumiwa ni haki kisheria kutomhoji Mh.Lowassa ulikosea huo ndio ukweli je kwanini suala la Makonda unataka ahojiwe? Mbona nao ulikamilika? Kumbuka watanzania hatudanganyiki tumesoma kama we we Sheria tunaijua mkuu
 
Ushahidi dhidi ya Lowasa ulikamilika ndiyo maana alitimuliwa kwenye Uwaziri Mkuu. Makonda bado Rc Mkoa wa Dsm, huoni tofauti hiyo?
 
Kwa hiyo kama kuna ufisadi mahali na serikali inaujua, na wahusika inawajua mpaka isubiri upinzani ulete hoja ndo ishughulikie? Kwa maana hiyo Mwakyembe anatwambia serikali haina uchungu na fedha za nchi hii na kama kuna mwenye uchungu ajitokeze? Sioni alichowatega CHADEMA zaidi ya yeye kujionyesha alivyo dhaifu katika Maamuzi kiasi cha kusubiri wenzie waanzishe jambo ndo adandie. Kwani tumesahau kwamba yeye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya Bunge iliyochunguza suala hili na kuhitimisha kwa kusema angeweka wazi ukweli wote nchi ingetikisika? Kwa maana hiyo ukweli bado anao, na naamini akiuweka wazi sasa hivi haitatikisika maana walioko madarakani ni wengine japo chama ni kilekile. Au bado nchi itatikisika kwa vile mhusika si mmoja tu toka ndani ya chama hicho? Tunakumbuka pia wakati wa kampeni aliahidi kumuumbua Lowasa kwa kuweka wazi ushiriki wake kwenye Richmond lakini mpaka kampeni zinaisha hakusema lolote zaidi ya yale aliyosema February, 2008 bungeni, au anataka tuamini kampeni bado zinaendelea na sasa yuko tayari kuhtimisha kampeni? Mwakyembe ukweli wa suala hili unaujua wote na wewe ndo wa kuuweka wazi vinginevyo ukae kimya maana burden of proof ya jambo hili iko kwako na si mtu mwingine maana wewe ndo tulikulipa hela yetu utuletee ukweli wote lakini ukasema umeweka nusu na kibakiza akiba. Basi tunaomba utumalizie nusu uliyobakiza vinginevyo tutaendelea kukudài UKWELI wetu uliobakiza.
 
Hivi huyu mzee alimaliza dozi ya kutoa sumu mwililini?
naona kabisa ambavyo sumu inazid kuathiri ubongo wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…