Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Yani Tiss iburuzwe mahakamani
Hapo ndio zito anapowapiga upofu. Tuseme anatumwa na TISS, je anayoongea ni SAHIHI au sio sahihi?Vipi kama hao TISS wanayomwambia ni kweli mfano kutembea na mke wa marehem, je huoni kuna ttz?
 
Serikali nayo mbona INAFUNGIA TU GAZETI KWANINI ISIENDE MAHAKAMANI?
Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
 
Magazeti ambayo huwa yanafungiwa na serikali, ni nani ambaye huwa ameenda mahakamani? Wendawazimu mtupu!
Wanaenda wahusika. Serikali haiwez wala haiwajibiki kwa vyovyote vile na habari binafsi za Mtu. Kama unadharirishwa ni wewe kwenda mahakaman na kudai HAKI na sio serikali iende mahakaman kusema Zito anadharirishwa. Huyo zito ndio aende mahakaman
 
Amesahau mwenzie aliyepiga marufuku Tundu Lissu asiombewe na yeye akapata ajali akaomba aombewe...Malipo ni hapa hapa maana watanzania walijua kumjibu
ipo siku atakuja kupotea yeye.alafu na sisi tutakaa kimya.
 
Yale magazei yaliyowahi kufungiwa walalamikaji ambao ni serikali walikwenda Mahakama ipi kulalamika kisha ikatoka hukumu ya kuyafungia???
Fuatilia, kuna taratibu za kutoa malalamiko. Na magazeti mengi unayoona yalifungwa yalitangulizwa barua za onyo. Idara husika ilifuata taratibu. Serikali haiwajibiki kwa vyovyote vile na habari binafsi za Mtu. Zito sio serikali kwamba msemaji wa serikali atolee maelezo,Huyo zito aende mamlaka husika.
 
Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
Kwanini serekali huyafungia magazeti kwa kigezo cha kukiuka taratibu za uandishi, kwanini nayo isiyapeleke mahakamani??
 
Umesema haki ipo mahakamani bwana.
 
Kwanini serekali huyafungia magazeti kwa kigezo cha kukiuka taratibu za uandishi, kwanini nayo isiyapeleke mahakamani??
Umeshasema yamekiuka taratibu na serikali ina mamlaka ya kuyafungia magazeti pale yanapokiuka taratibu. Sasa kwa Zito Gazeti limekiuka taratibu gani?Hayo malalamiko kampelekea nani?Au huko tweeter na fb ndio Serikali iliko?
 
Haya yanayofanyika kwa sasa yana lengo la kuwatoa watanzania katika report ya CAG...
 
Mbona magazeti mengine huwa anayafungia? Kwanini hao waliokashifiwa na hayo magazeti asiwashauri wakadai haki mahakamani?
 
Huyu mzee kuna wakati aliugua sana, sijui aliwekewa ' sumu'! Raia tuliungana kumuombea! Kumbe tungeacha tu mana na mimi naona lilikuwa swala dhaifu! Ila hawa ccm Mungu anawaona na malipo ni hapa hapa duniani! Yule mkubwa wa Sudan za hizi ananyea ndoo!
 
Huyu Dr wa hovyo kabisa angekua alinifundisha ningerudisha degree yao
 
sasa mbona wenyewe wanayafungia magazeti yanayowakosoa kwa nini wasiyapeleke mahakamani
 
Umeshasema yamekiuka taratibu na serikali ina mamlaka ya kuyafungia magazeti pale yanapokiuka taratibu. Sasa kwa Zito Gazeti limekiuka taratibu gani?Hayo malalamiko kampelekea nani?Au huko tweeter na fb ndio Serikali iliko?
Serekali ndo inayosema kuwa yamekiuka taratibu wa habari kama zito anavyo tuhumu pia.
Umshauri Zitto aende mahakamani kitu ambacho ni kizuri ingawa linapokuja swala la serekali kuyatuhumu magazeti hayo hutaki iende mahakamani kutafuta haki. Nilo likataa hapa ni serekali kuwa mlalamikaji na kisha kuwa hakimu. Hivi umeshafikiria kama Zitto angekuwa na mamlaka ya kulalamika na kuhukumu hilo gazeti angelifanyaje???
 
Eeeeh mwakyembe ni mwanasheria huyu sio????hivi anajielewa kweli?
 
Lakini bado usajili wa magazeti yote uko chini ya Wizara yake, kwani anapendezwa na aina ya uandishi wa hili gazeti? Je, angekuwa ameandikwa kiongozi yeyote wa Serikali angesema hayo ama lingefungiwa?
Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
 
Narudia tena Misuli, mahakama za huku Afrika huwa hazitoi haki iwapo unafanyiwa ufedhuli na watawala. Hilo gazeti ni la mtawala analitumia kama sehemu ya kuwachafua washindani wake. Kwa mfano Membe kaamua kwenda mahakamani, huko ataishia kupotezewa muda na hatashinda chochote, na hata ikitokea akashinda hakuna utekelezaji wowote wa hiyo hukumu utafanyika na hilo gazeti litaendelea kumchafua yeye na yoyote anayemsumbua mtawala. Huu ni upumbavu wa muafrika anapokuwa na madaraka. Ww tetea, jenga hoja lakini huna jipya kwa sababu haya yanayofanywa na hilo gazeti ni upuuzi wa viongozi wa kiafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…