Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online
Haya tumeelewa na Ben Saa8 je?
 
Jes
Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
Kesi ya ngedere ipekekwe kwa nyani patamu hapo....
 
...watu wasiendelee kufuatilia waliopotea..... Serikali itaendelea kudhibiti watoa maoni...!!!
Nadhani serikali ingeweka juhudi kusaka na kuwatambua watekaji...
Watoa maoni si watu hatari kama wale wanaoteka
....wanawajua ndo maana twaambiwa hakuna kuuliza!
 
Nimejikuta nasikitika kwa Waziri mwenye dhamana kufananisha uhai wa mtu na hoja ya neno dhaifu.....
 
Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online
Double standard!
 
Leo Mhe. Waziri wa Habari na Utamaduni katika kuhitimisha bajeti ya Wizara yake ametamka kuwa waoona kuwa wametukanwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani. Katika nchi iliyo na Utawala bora maneno kama yale hayakutakiwa kutamkwa na Mhe. Waziri. Ukurasa wa kwanza wa toleo la gazeti la Tanzanite yale maneno hayakutakiwa kuandikwa na binafsi gazeti hili linatakiwa likemewe. Sisi sote ni Watanzania. Tuheshimiane wote.
 
Wao wakikashifiwa na magazeti hayo hayo mbona hawaendi mahakamani wanakimbilia kulifungia gazeti badala ya kwenda huko mahakamani wanakojua kuna haki.
 
Inaonekana ile sumu aliyomwagiwa na mamvi bado ipo kichwani huyu mwakiembe hayuko sawa.
 
Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online
Ama kweli madaraka hulevya
 
Yeye mwakyembe alibabuka mwili mzima akwa anapita makanisani na marehemu sitta kuomba aombewe alikuwa anapita atatangaza kapewa sumu yote akitetea uhai wake, alifiwa na mkewe akalia kama mtoto kwenye jeneza la mkewe yote hii alijua thamani ya uhai wa mwanadamu, leo anasema marufuku kuulizia Azory, watu wasijitie upunguani kuna maisha baada ya haya ya dunia Mungu yupo.
 
Nadhani bado Ana kitu kinachomsumbua katika akili yake.... Ni Dr ambae anatuona sie wanyonge hatuna maana kuulizwa tukipotea...? Hawa watu wamejipa U-Mungu mtu Sana.
 
Ninyi mawaziri hayo majibu mepesi mnayo toa kwa watanzania yatakuja kuwagharimu ni swala la muda tu.
 
Tunahitaj kufanya juhud sana kama Taifa maana kadri muda unavyozid.Ndivyo tunavyojua watesi wetu wanavyotuwazia.Inavyoonesha wanatuona wapumbavu sana.Ni heri wangetuona wajinga maana ujinga unaisha lakin wao wanatuona kama maiti hivi.
 
Back
Top Bottom