TANZIA Mwalimu Alex Kashasha, mchambuzi nguli wa Soka afariki dunia

TANZIA Mwalimu Alex Kashasha, mchambuzi nguli wa Soka afariki dunia

Tanzia: Mchambuzi nguli wa soka Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha amefariki dunia leo Agosti 19, 2021 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Kairuki mkoani Dar es Salaam.
 
Mchambuzi nguri wa soka hapa Tanzania mwalimu Alex Treojenusi kashasha amefariki dunia mchana huu katika hospital ya kairuki jijini dar es salaam alipo kuwa anakatwa matibabu

Mwalimu kashasha alikuwa mwalimu wa michezo katika vyuo mbalimbali na baadae akawa mchambuzi wa soka katika television ya taifa .

Mwalimu kashasha alikuwa anaunguruma katika kipindi Cha michezo Cha TBCFM

Kwa wale wanasoka watakuwa wanamtambua mwamba huyu wa kuchambua soka kwa weledi wa hali ya juu

R.I.P mwalimu wa michezo

USSRView attachment 1898153
Daaaa.huyu jamaa alikuwa ni nguli wa uchambuzi wa michezo.halafu ile art yake ya uchambuzi ilinivuta hata kusikiliza hiyo TBC .
 
Huyu mzee alikuwa mtaalamu kabisa kwenye kuchambua masuala ya Kandanda..kwa mara ya kwanza nilimsikia akichambua TBC mwaka 2014 kombe la dunia.. R.I.P mzee kashasha
 
Back
Top Bottom