TANZIA Mwalimu auawa na Mwalimu mwenzake shuleni

TANZIA Mwalimu auawa na Mwalimu mwenzake shuleni

Geita. Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha (pichani) kwa kumchoma na kisu akiwa darasani.

mwalimu-pic.jpg

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza.

“Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo,” amesema Kamanda Jongo.

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea.

“Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea mwalimu amekamatwa na amekiri na sababu anadai aliona walimu wenyeji wanamchukia na wamemtenga na ndio sababu ya kutengeneza nia ya kutenda tukio hilo,” amesema.

Credit: Mwananchi
 
siungi mkono mauaji
ila ubaguzi una uma sana
unakuta watu wa kabila moja wanakaa wanakutenga kila unacho fanya unaonekana unakosea na wanatengeneza kila namna ya kukuferisha

vita ya madaraka kwa vijana, tamaa ya vyeo itawamaliza
 
Mtihani wa darasa la kwanza..🤔🤔

uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea. 🤔🤔

Hatari sana, watoto wanafundishwa na watu wa ajabu ajabu.. matokeo tunazalisha watu wa ajabu ajabu.. walimu walikuwa enzi za mwalimu
 
Siungi mkono kitendo hicho but for the one who have gone through segregation can understand how it feels
 
Geita. Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha (pichani) kwa kumchoma na kisu akiwa darasani.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza.
“Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo,” amesema Kamanda
Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi baina ya walimu hao ambao walikuwa wanagombea uongozi kwenye kitengo cha elimu ya kujitegemea.
“Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea mwalimu amekamatwa na amekiri na sababu anadai aliona walimu wenyeji wanamchukia na wamemtenga na ndio sababu ya kutengeneza nia ya kumuua huyo mwalimu menzake.
 
Back
Top Bottom