Nililitegemea hili kutoka kwako, kwamba wewe ni wale waumini ambao hufanya tafakari ya Biblia kwa kusoma maneno kama yalivyo bila kuzingatia mambo kadhaa kama muktadha uliotumika kuandika, akina nani walikua walengwa, wakati gani etc.
Lakini pia wewe ni wale waumini ambao huchagua maneno ya kuyachukua na kuyaacha kwenye Biblia, wale waumini ambao wanasemaga hili hatulitaki ila hili twendeni nalo.
Mfano mzuri tu ninyi wasabato mnaamini katika kutokutumia kilevi, lakini kwenye Biblia mnayotumia kuna mistari kadhaa inayoonyesha kwamba kileo ni kitu kizuri tu hakina tatizo tunaweza kunywa, ok..mbona huwa hamtumii hiyo mistari kunywa vileo? The answer is simple tu hapa chini;
Brainwash mliyoipata kwa mama yenu Hellen G White, kwamba kwenye Biblia tukazie haya mawili, Siku ya jumamosi ndiyo siku ya kuabudu, kutokula nguruwe. Ila sisi hatuna tatizo na nyie...mna haki ya kuamini chochote, wala hatutawaita majina ya kuudhi, mna haki kabisa
Hivi tukirudi katika mistari uliyoweka hapo juu tukaamua kutafasiri kila kitu kama kilivyo hapo unaweza leta majibu yenye mashiko?
Mfano mdogo tu, hayo magari ya vita atakayokuja nayo Bwana ni yapi? Ni magari gani hayo? Sasa hivi yapo wapi?, Kwahiyo atakuja kufanya vita? Kupigana na akina nani na hayo magari ya vita? Si tunaamini Bwana ni Mungu mwenye uweza sana kiasi akiamua kutuangamiza wote kwa neno lake tu anaweza? Sasa kwanini aje kufanya vita kwa kutumia magari...kufanya vita na viumbe aliowaumba yeye mwenyewe?
Ukielewa muktadha wangu hapo juu utaelewa kwamba Biblia haitafasiriwi hivi hivi tu kama unavyoamua wewe ama ilivyoandikwa, it is much more than that bro.