Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Serikali haifanyi mambo kwa pupa ila kwa strategies ndio maana iliamua kuchukua soft measures ili kutozua taharuki lakini haka kajamaa kakawa myopic kwa kukatalia mamlaka ya uteuzi.Huyu jamaa ameidhalilisha sana serikali kwa kujifanya nunda
Sasa kama hataki UCHAWA watamlazimisha mkuu? Kwani kuwa chawa lazima?
 
Basi tujiulize kwanini hataki kurudi Temeke ambako ndio ajira yake iliko kwani CWT Kuna nini mpaka anang'ang'ania? Akaimbe cheichei na watoto ndio wito na ajira yake iliko
Mkuu hebu rudia kusoma uzi umejieleza vizuri kwanini serikali wanamchukia Maganga. Ni kwa sababu anakuwa mgumu wa kuwaruhusu kuingia CWT kujitoea pesa za uchaguzi ndani ya chama na uchaguzi mkuu 2025. Wanataka wamfukuze kazi halafu wampachike kibaraka wao ili waendelee kuchota fedha za CWT bila shida. Umeelewa sasa?

Wewe unadhani kwanini serikali wanapenda kuingilia mambo ya CWT kuliko chama kingine chochote cha wafanyakazi? Ni kwa sababu kule kuna fedha nyingi za bwerere wanazoweza kuchota wakati wowote wakipenda. Tupo pamoja?
 
Aondolewe huyo mwana kulitafuta mwana kulipata, kwanini akatae kurudi Temeke sasa Kama kweli hakuhitaji uteuzi wa Raisi mbona anang'ang'ania CWT???
Hajang'ang'ania bali amegomea vyote....uDC na kurejea kazini. Wewe unatakaje?
 
Mkuu ubarikiwe,msaada kidogo,je naruhusiwa kukaa bila chama chochote kisheria!? Au nikijitoa lazima niwe na chama mbadala
 
Mkuu ubarikiwe,msaada kidogo,je naruhusiwa kukaa bila chama chochote kisheria!? Au nikijitoa lazima niwe na chama mbadala
Mkuu unaruhusiwa kabisa bila shida yoyote. Watumishi wengi hawajajiunga na chama chochote wanakula bata kwenda mbele. Kujiunga na chama ni hiyari sio lazima mkuu. Jitoe haraka halafu ulete mrejesho hapa.
 
Serikali inamuajiri vipi katibu wa CWT? Hayo mamlaka ya kumuongezea muda yanatokea wapi?
 
Mkuu unaruhusiwa kabisa bila shida yoyote. Watumishi wengi hawajajiunga na chama chochote wanakula bata kwenda mbele. Kujiunga na chama ni hiyari sio lazima mkuu. Jitoe haraka halafu ulete mrejesho hapa.
Asante mkuu,ubarikiwe ,
 
Hivi kujiunga huko CWT ni automatic, au hadi ujaze fomu kama vyama vingine? kama ni by default hiyo ni hujuma kwa walimu kwa sababu hivyo ni vyama vya hiari.
Sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 7 ya mwaka 2004 inapiga marufuku kukata mshahara wa mtumishi pasipo ridhaa ya mwajiriwa anayoitoa kwa mwajiri wake kwa kujaza fomu iitwayo Tuf 15 na kutuma maombi ya kujiunga kwenye chama cha wafanyakazi. Ila kwa bahati mbaya siwitiii wakishirikiana na maafisa utumishi kwa makusudi wameamua kwa makusudi kuikanyaga sheria halali kwakuingiza makato kwenye check number za walimu pasipo indorsement za wenye mishahara hasa kwa walimu walioanza kazi kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma .Hivi hao Cwt kiburi cha kudharau sheria hiyo halali ya nchi mpaka sasa watendaji wake wamediriki mpaka kukataa teuzi toka kwa mh Rais wanakipata wapi?
 
Aliajiriwa kama Mwalimu


Tatizo wengi mnatumia makamasi badala ya akili
 
Mwajiri ana haki ya kukuita kazini. Mnamjaza tuu huyu Jamaa.
 
Iandike wakati ndio huu labda itamsaidia huyo
 
Kama kuna watu wanadhani huyo Maganga alikataa uteuzi wa kuwa mkuu wa wilaya kwa sababu ana uchungu sana na walimu watakuwa wanakosea sana ukweli ni kwamba jamaa alifanya ulinganifu wa maslahi atakayopata akiwa mkuu wa wilaya na akiwa huko Cwt ambako pesa za walimu watu wanalipana posho na mishahara kama hizo hela hazina mwenyewe na ukaguzi wa CAG 2017/2018 ulithibitisha hivyo
 
Na ndicho anatakita hataki kazi hivyo asilazimishwe
 
Mtaje tu huyo Mkubwa fulani..
 
Let's assume kwamba huyo Maganga amezuia serikali isichote pesa huko Cwt kwa maelezo yako.Je hizo hela za walimu zimekuwa safe kiasi gani na lini ? Mbona bado kuna malalamiko kibao kwamba huko Cwt hela za walimu zinatafunwa ovyo ni kama hazina mwenyewe na ripoti ya CAG ya mwaka 2017/2018 ilithibitisha hivyo na mwaka huo huyo Maganga alikuwa kiongozi huko Cwt .Niombe mama Samia akiona inafaa atume tena CAG aone ni kwa namna gani hela za walimu wetu zinakuwa monitored tangu ukaguzi wa mwisho enzi za Magu
 
Kwani habari zake zilitolewa na serikali au mtu tuu? ilikiwa tangazo la serikali namba ngapi? Huyo kakataa udc vile amezowea Kula pesa za walimu hovyo bila kufanya kazi yoyote!! Arudi huko akafundishe watoto yanini analazimisha kazi CWT? Akwendreee Hana jipya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…