Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake

Watumishi wangapi wanasimamishwa kazi au kufukuzwa kazi kila siku hatujawahi ona "Tangazo kwa Umma"?

Kuna kitu hakiko sawa dhidi ya huyu Mwalimu. Hizi nguvu zote za kumchafua in public ni obvious jamaa kawashinda, so wanatafuta public sympathy
 
Mkurugenzi ni kama hawa watanzania wengi walio humu, wanamuona jamaa ni mjinga kwa kutokuwa mtu wa ndiyo mzee. Mamlaka zinamsulubu isivyo halali na watanzania wamekaa wanamcheka kuwa alibugi, halafu wakimaliza kucheka wanasema wanataka katiba mpya.

Yaani kifupi ni kuwa shule watu wamesomea ujinga. Ni wanafiki mwanzo mwisho.
 
Huyo Mkurugenzi amekosa Weledi katika kazi, Barua za namna hiyo huwa ni siri, sasa anautangazia umma ili iweje?
 
Kunawatanzania leo tungekuwa tunatawaliwa na mkoloni - Nyerere asinge tukomboa.
 
Huyo Mkurugenzi amekosa Weledi katika kazi, Barua za namna hiyo huwa ni siri, sasa anautangazia umma ili iweje?
Si bado katibu cwt

Ova
Ukikosa sifa ya kuwa Mwalimu moja kwa moja unakosa sifa ya kuwa Kiongozi wa CWT.
 
Huyu mbwiga kuna file lake mwezi februari litakuwa takukuru na ataanza msoto wa mahakamani
 
Hakuna rangi ataacha kuona ni suala la muda tu na atafungwa kwa kesi ya wizi hapo CWT.

Huo uteuzi alioukataa ilikuwa ni mbinu ya kuwatoa viongozi wote hapo CWT na baadae wangetenguliwa uDC na kustaafishwa kwa manufaa ya umma km ilivyotokea kwa DC wa Tabora Bwana Komanya!
 
Wanamualika kwenye siasa. Ngoja aje awasumbue huko.
Ogopa sana watu wanaojiamini. Siasa inayotumika inaweza kumfanya awe na nguvu zaidi kuliko sasa.
Labda wamfunge kwa tuhuma za wizi wa fedha za cwt.
Abdul Nondo walimfukuza chuo kikuu akageuka kuwa mwiba kwa ccm, naye huyu asije kuwa mwiba utao wachoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…