Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake

kweli kuna watu wanaweza shindana na serikali, safi sana, ukijua sheria na ukijua haki zako hutakiwi kuogopa mamlaka, sasa badala ya kumfuta kazi wanaruka ruka tu, mtu kamgomea mpaka raisi, muacheni tu afanye mambo yake, kama shule ina upungufu wa walimu ajirini mwingine mbona wanaohitaji ajira wako wengi, huyu maganga ashakuwa legend mwacheni apambane na majukumu yake kunako cwt
 
Mshahara wa DC ni 4M,inawezekana huko kwenye Ukatibu anapata zaidi ya hiyo hata ungekuwa wewe lazima ungekataa.
Alitakiwa kusoma alama za nyakati. Wakati anapewa UDC ilikuwa imeshapangwa kuwa hatakiwi tena kule CWT. Sasa kagomea U DC na kule CWT kaondolewa.
 
Bado ni mwalimu, amesimamishwa tu ila hajafukuzwa
Hata akifukuzwa Kazi bado ataendelea kuwa Mwalimu kama Mtumishi, lakini atakosa sifa kwa kuwa atakuwa amefukuzwa Kazi.

Kwa kosa analotuhumiwa nalo adhabu yake ni "KUFUKUZWA KAZI BILA UTUMISHI" na hawezi kutoboa labda awahi kwenda kwenye Tume ya Usuruhishi na Upatanishi "CMA" la sivyo kinachofuata ni KUFUKUZWA KAZI BILA UTUMISHI.
 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, ndugu Elihuruma Mabelya anapenda kuufahamisha Umma kuwa, Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) ambayo ndiyo mamlaka ya nidhamu ya Walimu, imemsimamisha kazi Mwalimu Maganga Moses Japhet aliyekuwa Mwalimu wa shule ya Msingi Tandika iliyopo kata ya Tandika, tangu leo, Desemba 05,2023.
Mwalimu wa Primary anawatoa jasho tusubiri wakianza wa sekondari na vyuo
 
Kimsingi hawa viongozi wetu wa TSC na huyu Mkurugenzi wanatumika na Deus, Serikali wasichokijua ni kwamba Deus anawachezea mchezo mbaya na furaha ya Deus ni Kuona Mwamba huyo anatoka katika hiyo Nafasi.. SERIKALI INATUMIKA VIBAYA
Hakuna Chombo kibovu kama TSC, sehemu kubwa huwa wanatumika tu, hawapo pale kwa ajili ya kutetea Walimu hata kidogo.
 
Huyo Mkurugenzi amekosa Weledi katika kazi, Barua za namna hiyo huwa ni siri, sasa anautangazia umma ili iweje?

Ukikosa sifa ya kuwa Mwalimu moja kwa moja unakosa sifa ya kuwa Kiongozi wa CWT.
Kwahiyo wale waajiriwa wa kudumu pale cwt wote ni walimu?
 
Kwa Kanuni za Kiutumishi za CWT, Katibu Mkuu anatakiwa kuwa Mwalimu aliye kazini ila anayefanya kazi CWT kwa kuazimwa kwa muda maalum. Kwa kitendo cha kusimamishwa, automatically, anakuwa amesimama pia kuwa Katibu Mkuu wa CWT. Na nafikiri wamemsimamisha muda huu ili "ASIWEPO JUKWAANI" kwenye Maadhimisho ya Siku wa Mwalimu yatakayofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Manispaa ya Ilemela tarehe 13/12/2023.
Basi katiba yao ndio kifungo, waondoe hicho kipengele ili katibu awe independently sio lazima awe mwalimu muajiriwa lkn angalau awe amesomea taaluma ya ualimu
 
Hata akifukuzwa Kazi bado ataendelea kuwa Mwalimu kama Mtumishi, lakini atakosa sifa kwa kuwa atakuwa amefukuzwa Kazi.

Kwa kosa analotuhumiwa nalo adhabu yake ni "KUFUKUZWA KAZI BILA UTUMISHI" na hawezi kutoboa labda awahi kwenda kwenye Tume ya Usuruhishi na Upatanishi "CMA" la sivyo kinachofuata ni KUFUKUZWA KAZI BILA UTUMISHI.
BAsi akifukuzwa kazi bila utumishi maana yake utumishi bado anabaki nao lkn kazi ya ualimu ndio wameichukua basi cwt wamrudishie ukatibu wake kwakuwa anayo sifa ya utumishi kwakuwa hawajampora utumishi wake
 
Maganga alikataa kuwa kama CWT wengine , hata watanzania wasio watumishi wa umma wanajua vyama vya wafanyakazi na vyama vya kitaaluma kwa Tanzania ni geresha tu ni matawi ya CCM.

Ukiangalia tija ya hivyo vyama kupigania maslahi ya watumishi wanaowawakilisha ni sifuri.

Inabidi vifumuliwe viundwe upya.
 
katika nchi zinazoongoza kwa watu wajinga wajinga na tunaongozwa na watu wengi wao walio wajinga wajinga bhs tanzania ni moja wapo unaeza fika kipind hata huwez jivunia kuwa mtanzania kwa mambo yanayoendelea
 
Back
Top Bottom