Mwalimu Mkuu aliyepewa fedha za TAKUKURU Afariki Dunia, yadaiwa amekunywa kimiminika chenye sumu

Huyu mwalimu vipi huyu, watu tunadaiwa mamilioni na tunakomaa angejua. Tunadaiwa na serekali, upande mmoja TRA wametuma reminder miksa vitisho hadi wamekaa kimya achilia mbali madeni ya bank 2 tofauti ambapo inayodai kidogo ni milioni 67 na Riba zinapanda tu Kila siku lakini ndio kwanzaaaaaaaaa tunakaa bar Tena kaunta kwa raha zote
We jamaa bhana 😂😂🤣 Kwa moyo huo utaishi miaka mingi sana halafu utakufa Kwa kung'atwa na mbu tu.
 
Sio rahisi kuamini kua kajiua
Ukute kajiua kweli, na ukute hiyo pesa anayo wala hakuila....shida ni kuwa alichelewa kutengeneza hilo bango.

Msione Mwenge unapita mtaani huwa kuna rabsha nyingi kwenye maandalizi....Mwalimu alitakiwa kujisimamia na kujitetea, Hao TAKUKURU walishindwa nini kulitengeneza Hilo bango wenyewe walipeleke shuleni?

Kingine ni kuwa wakuu wa shule jitahidini kuishi vizuri na subordinates wenu, wengi mna ukoloni na mahusiano mabaya, Yani mnawachukulia subordinates Kama wanafunzi vile....Hapo ukute Mkurugenzi katishia kumtoa ukuu Kwa kuwaharibia shughuli ya Mwenge, yeye kaona bora ajiue, Yani afe na ukuu wake🤣
 
Huyu mwalimu vipi huyu, watu tunadaiwa mamilioni na tunakomaa angejua. Tunadaiwa na serekali, upande mmoja TRA wametuma reminder miksa vitisho hadi wamekaa kimya achilia mbali madeni ya bank 2 tofauti ambapo inayodai kidogo ni milioni 67 na Riba zinapanda tu Kila siku lakini ndio kwanzaaaaaaaaa tunakaa bar Tena kaunta kwa raha zote
Naye alikuwa bar akipata hiyo raha.
 
Mm nadaiwa mil 60 na nmb .tra 14mil watu binafsi si chini ya 100 na bado badae ntakuwa Juliana kwa raha zangu
huna habari ndio kwanza unanenepa kama nguruwe yaani[emoji23][emoji23][emoji23].

kudaiwa sio kesi ya ubakaji.
 
Mnamo tarehe 14.09.2023 majira ya saa 1:30 asubuhi huko katika nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari Mtanila iliyopo Kijiji cha Igangwe Wilaya ya Chunya, Mkuu wa Shule hiyo aliyefahamika kwa jina la MAGWIRA NKUTA [41] alifariki dunia baada ya kunywa kimiminika kinachodhaniwa ni sumu.

Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo kwani inadaiwa kuwa kabla ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru, marehemu alikabidhiwa fedha na ofisi ya TAKUKURU kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kibao cha “KLABU YA TAKUKURU RAFIKI SHULENI” lakini pamoja na kutumiwa fedha hizo hakuweza kutengeneza kibao hicho hadi Mwenge wa Uhuru ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wa Klabu hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi walioibiwa mali mbalimbali kufika kituo cha Polisi Rujewa, Mbeya Mjini na Chunya kwa ajili ya utambuzi wa mali zao. Aidha, linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wakamatwe na kuchukulia hatua za kisheria.
Dah huu mtiririka wa habari ni wa aina yake
 
Ilikuwa shilingi ngapi? Kama fundi alizila alishindwa kuweka zake ili baada ya tukio amalizane na fundi?
 
Kwani hata angeambiwa alipe elfu hamsini atainyea Wapi, labda mpaka mshahara ila kama ni katikati ya mwezi hakuna ticha mwenye hela hiyo
Sidhani kama anaweza kuikosa hata kwa kukopa kwa mwalimu wa tutution wa mathe😂😂😂 au basi kumfukuza mwanafunzi kwa kuongea kilugha na kumpa adhabu ya kuja na elfu hamsini ya kununua vitabu vya kiingereza.
 
Back
Top Bottom