Mwalimu Mkuu aliyepewa fedha za TAKUKURU Afariki Dunia, yadaiwa amekunywa kimiminika chenye sumu

Mwalimu Mkuu aliyepewa fedha za TAKUKURU Afariki Dunia, yadaiwa amekunywa kimiminika chenye sumu

Kuna watu wanaiba mamilioni ya serikali wapo na hawafanywi kitu, uoga ni mbaya sana.
Kuna fisadi moja la ccm liliwahi kuniambia nisiogope kutoa rushwa kwani serikali ni dude kubwa na halina mqenyewe...ccm kumbafu sana
 
Kweli nchi hii inavituko! Mwalimu kala hela ya kibao ambayo hata iweje haiwezi kuzidi laki anajiua, lakini hawa wapo wanadunda na pengine wanatukashifu kwa dharau kabisa;
efe2af1cad09483d9b6d90dfa0818d64_379078763_1464927630934104_5929163713653261950_n.jpg
 
Ni wazi hakujiua kwa sababu za hicho kibao, wachunguze kwa kina sababu za kweli ni zipi. Au kama wanazijuwa waseme ukweli tu.
 
Kuna kitu Kiko nyuma ya pazia! Mwl huwa ni mtu asiekosa solution kwa tatizo lolote!
Mi nadhani Huyu ticha hajanywa mwenyewe kwa hiari itakuwa kanywesha! Au alikuwa na shida ingine kubwa kaunganisha!
 
Kuna wakati maisha yanakupiga, usidharau mahangaiko ya wengine.
Huenda kiasi kilichopelekea yeye kujitoa uhai kwako wewe ni kidogo lakini kwake kwa wakati huo mpaka anachukua uamuzi wa kujitoa uhai sio jambo jepesi.
Mungu atupe mioyo ya ujasiri na imani tupitiapo magumu, na mwalimu apumzike kwa amani.
Note; Siungi mkono kujiua!
Nifah
💛💛💛💛💚💚💚💚
 
Mnamo tarehe 14.09.2023 majira ya saa 1:30 asubuhi huko katika nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari Mtanila iliyopo Kijiji cha Igangwe Wilaya ya Chunya, Mkuu wa Shule hiyo aliyefahamika kwa jina la MAGWIRA NKUTA [41] alifariki dunia baada ya kunywa kimiminika kinachodhaniwa ni sumu.

Chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo kwani inadaiwa kuwa kabla ya ujio wa mbio za mwenge wa uhuru, marehemu alikabidhiwa fedha na ofisi ya TAKUKURU kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kibao cha “KLABU YA TAKUKURU RAFIKI SHULENI” lakini pamoja na kutumiwa fedha hizo hakuweza kutengeneza kibao hicho hadi Mwenge wa Uhuru ulipofika shuleni hapo kwa ajili ya ufunguzi wa Klabu hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi walioibiwa mali mbalimbali kufika kituo cha Polisi Rujewa, Mbeya Mjini na Chunya kwa ajili ya utambuzi wa mali zao. Aidha, linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wakamatwe na kuchukulia hatua za kisheria.
Amegive up so easily
 
Ukute kajiua kweli, na ukute hiyo pesa anayo wala hakuila....shida ni kuwa alichelewa kutengeneza hilo bango.

Msione Mwenge unapita mtaani huwa kuna rabsha nyingi kwenye maandalizi....Mwalimu alitakiwa kujisimamia na kujitetea, Hao TAKUKURU walishindwa nini kulitengeneza Hilo bango wenyewe walipeleke shuleni?

Kingine ni kuwa wakuu wa shule jitahidini kuishi vizuri na subordinates wenu, wengi mna ukoloni na mahusiano mabaya, Yani mnawachukulia subordinates Kama wanafunzi vile....Hapo ukute Mkurugenzi katishia kumtoa ukuu Kwa kuwaharibia shughuli ya Mwenge, yeye kaona bora ajiue, Yani afe na ukuu wake[emoji1787]
....eti afe na ukuu wake...daah [emoji1787][emoji1787]
 
Kuna kitu Kiko nyuma ya pazia! Mwl huwa ni mtu asiekosa solution kwa tatizo lolote!
Mi nadhani Huyu ticha hajanywa mwenyewe kwa hiari itakuwa kanywesha! Au alikuwa na shida ingine kubwa kaunganisha!
Kama mwakimu hakosi soln Kwa tatizo lolote lile kama unavyosema, alishindwaje kupata soln ili asinyweshwe sumu?

Walimu bhana[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom