pri
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 826
- 666
Hovyooooo!hivi ni lazima kuonesha upumbavu wako?Huko nyuma nilikuwa nakuona uko Smart ila kwa sasa taratibu naanza Kukuona nawe ni kama vile Unapotea na Hamnazo fulani hivi japo Nakukubali mno na sana Kimafundisho.
Mwalimu Mwakasege unajua fika kuwa Mtume Mwamposa ( Mshindani wako Kiimani na Kimahubiri na Mwanafunzi wako ) ameshawateka wana Dar es Salaam tena wa Kawe aliko lakini nawe kila ukija Kufanya Mahubiri yako Mkoani Dar es Salaam unangangania kuwa ni Kawe ( Tanganyika Packers ) tu.
Hivi Mwalimu Mwakasege kwani ukiwa unafanya Tamasha lako ( Mahubiri yako ) maeneo mengine ya Dar es Salaam kama Viwanja vya Mwembe Yanga hutoweza kupata Watu wanaokuamini?
Haya ona sasa umepanga nawe Kuanza Tamasha lako ( Mahubiri yako ) Leo Tanganyika Packers ( kama sijakosea ) na Mtume Mwamposa baada ya kuona utapiga Hela na Yeye kwa Makusudi ameweka Tamasha la Wanawake ambao ndiyo Mtaji wake na Jeshi Kubwa Kanisani Kwake hivyo kusababisha ukimbiwe na Waumini wako wengi waliopanga Kuhudhuria ( Kuja ) Kwako leo.
Mtume Mwamposa ( Mshindani wako Kiimani na Kimahubiri japo ni Mwanafunzi wako pia ) anajua mno Kucheza na Akili zako na anahakikisha ukija tu Mkoani Dar es Salaam kufanya Tamasha lako basi nae pia Wiki hiyo hiyo atafululiza na Matamasha ili mradi tu mgawane Waumini na usipate Kiwango cha Pesa ( Sadaka ) ulichokilenga kama siyo Kukikusudia.
Ukishauriwa hutaki Kusikia. Leo kama utapata Sadaka nyingi ni Shilingi Elfu Arobaini na Tano na Mia Tano Hamsini ( Tsh 45,550/= ) tu wakati Mwenzako Mtume Mwamposa kwa Nyomi la leo najua akikusanya Sadaka zote hakosi Shilingi Milioni Tano ( Tsh 5,000,000/= ) mpaka Milioni Kumi ( Tsh 10,000,000/= )
Labda baada ya huu Uzi wangu Utabadilika.