Mwalimu Mwakasege uwe unajiongeza ili kuzishinda mbinu za Mwamposa katika kugombania Waumini Tanganyika Packers Kawe

Mwalimu Mwakasege uwe unajiongeza ili kuzishinda mbinu za Mwamposa katika kugombania Waumini Tanganyika Packers Kawe

Hivi mtume kwa wakristo anatambuliwaje???

Mtume anatambulika mfungua makanisa na kazi ya Mungu maeneo tofauti tofauti. Yani mtume Ni mtu wa kutembea Sana kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na injili.
 
Ww pia hujui kitu, wote wachumia tumbo, wanakula sadaka za watu kupitia jina la Yesu, siku Yesu akirudi anaanza na Mwamposa na Mwakasege kuwapeleka motoni kabisa jehanam, sbb wanatafuta hela usiku na mchana kwa kutumia jina la Yesu, wakati Yesu hakufanya hivyo, huko ni kufanya biashara kwa jina la Yesu.

Yesu hakufanya biashara za kukusanya sadaka, yaani watu wajinga wanaangamia kwa kukosa maarifa.
Kwa taarifa yako tu, Mwakasege haandai mikutano. Yeye ni mwalikwa tu. Hata wewe waweza kuandaa mkutano wako ukamualika, ratiba yake ikiwa free atakuja
 
Huko nyuma nilikuwa nakuona uko Smart ila kwa sasa taratibu naanza Kukuona nawe ni kama vile Unapotea na Hamnazo fulani hivi japo Nakukubali mno na sana Kimafundisho.

Mwalimu Mwakasege unajua fika kuwa Mtume Mwamposa ( Mshindani wako Kiimani na Kimahubiri na Mwanafunzi wako ) ameshawateka wana Dar es Salaam tena wa Kawe aliko lakini nawe kila ukija Kufanya Mahubiri yako Mkoani Dar es Salaam unangangania kuwa ni Kawe ( Tanganyika Packers ) tu.

Hivi Mwalimu Mwakasege kwani ukiwa unafanya Tamasha lako ( Mahubiri yako ) maeneo mengine ya Dar es Salaam kama Viwanja vya Mwembe Yanga hutoweza kupata Watu wanaokuamini?

Haya ona sasa umepanga nawe Kuanza Tamasha lako ( Mahubiri yako ) Leo Tanganyika Packers ( kama sijakosea ) na Mtume Mwamposa baada ya kuona utapiga Hela na Yeye kwa Makusudi ameweka Tamasha la Wanawake ambao ndiyo Mtaji wake na Jeshi Kubwa Kanisani Kwake hivyo kusababisha ukimbiwe na Waumini wako wengi waliopanga Kuhudhuria ( Kuja ) Kwako leo.

Mtume Mwamposa ( Mshindani wako Kiimani na Kimahubiri japo ni Mwanafunzi wako pia ) anajua mno Kucheza na Akili zako na anahakikisha ukija tu Mkoani Dar es Salaam kufanya Tamasha lako basi nae pia Wiki hiyo hiyo atafululiza na Matamasha ili mradi tu mgawane Waumini na usipate Kiwango cha Pesa ( Sadaka ) ulichokilenga kama siyo Kukikusudia.

Ukishauriwa hutaki Kusikia. Leo kama utapata Sadaka nyingi ni Shilingi Elfu Arobaini na Tano na Mia Tano Hamsini ( Tsh 45,550/= ) tu wakati Mwenzako Mtume Mwamposa kwa Nyomi la leo najua akikusanya Sadaka zote hakosi Shilingi Milioni Tano ( Tsh 5,000,000/= ) mpaka Milioni Kumi ( Tsh 10,000,000/= )

Labda baada ya huu Uzi wangu Utabadilika.
Yaani nashindwa kuwaelewa hawa kondoo waaminiye hawa wachungaji, hivi mnakuwa mmerogwa au? Hawa wachungaji ni wasanii tu, hawana lolote.
 
Ila sisi wakrisyo dah[emoji2357] ,kwamba kuna ushindani wa kimahubiri tena?? Aya na point yako imelenga zaidi kwenye sadaka wala sio mafundisho, me nilidhani utafurahi kuwa wananchi wa kawe watakuwa wamepata neema ya kuhubiriwa na watumishi wawili kwa wakati mmoja aisee!
 
Achana na mambo usiyoyajua. Mwakasege ni mwalimu, Mwamposa ni mtume, huduma mbili tofauti.

Wingi wa watu huletwa na Roho Mtakatifu kutokana na anavyotaka kuwahudumia
Ila Mwakasege alipoanza kunena kwa lugha ndo nikachoka kabisa, huyu si mwalimu huyu...........akaprakachakachakapakara....uongo uongo kama tapeli Mwamposa.
 
Kwanza mwalimu mwakasege husema huwa hafanyi jambo bila kumshirikisha Mungu kwa hiyo haendi popote kama Mungu hajamwambia aende hata kiwanja hachaguichagui kwa akili zake,pili acha kumchafua mtumishi wa Mungu usije ukajiletea laana kwenye maisha yako na kizazi chako.
 
Achana na mambo usiyoyajua. Mwakasege ni mwalimu, Mwamposa ni mtume, huduma mbili tofauti.

Wingi wa watu huletwa na Roho Mtakatifu kutokana na anavyotaka kuwahudumia
Eti mtume [emoji1]

Ova
 
Sidhan kama una akili timamu aisee nimesoma andko lako ni kama unawaona mwakasege na mwamposa hawatoi huduma yoyote zaid ya kulenga sadaka tu mambo ya imani yaachen kama yalivyo hayahitaji ujuaji wa kuitana mkuu mkuu kama hayajakufka mambo ya ulimwengu wa roho nyamaza kmy potezea kbs.
 
Bora wenzako wanashindana kwenye maandiko ya Mungu kuliko we popoma unaeshindana kumiliki ID uchwara!
 
View attachment 2510825
Hakika hakukosea. [emoji1431]
Hiki kitabu nitakitafuta maana nilimsikia akielezea jinsi alivyokiandika,kwamba alikuwa kwenye ndege kurudi bongo,walipotua nchi fulani ili kubadilisha ndege mhudumu akamwambia yeye na mke wake watapanda first Class,akashangaa kidogo maana yeye alikuwa amepanda second class,ikabidi waingie,walipokaa tu huko First class kuna meza na taa, Roho mtakatifu akaanza kumpa madini,anasema aliandika kwa saa tano mfululizo mpaka akamaliza.
 
Achana na mambo usiyoyajua. Mwakasege ni mwalimu, Mwamposa ni mtume, huduma mbili tofauti.

Wingi wa watu huletwa na Roho Mtakatifu kutokana na anavyotaka kuwahudumia
Kwamba Huyo Tapeli ni Mtume? Kamtuma nani?

Mungu hakufanya huduma kwa malipo
 
Back
Top Bottom