Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

Uteuzi wa
Juliana shonza.......
Jerry Muro

Nk

Umefanya wengine wengine wengi kuehuka

Wanajitapikia tuuu hovyohovyo mitandaooni wakiamini kutapika kutawapa ulaji

Lengo na ndoto ya Annael nikubahatisha uteuzi mithili ya fisi akisubiria mkono wa binadamu kudondoka.

Ukweli ni upuuzi na ujinga kujikomba kwa upumbavu

Tusipotoshe umma kijinga kwa uchu wa madaraka.
 
Hata wakati Kikwete anaingia madarakani mlisema maneno kama hayahaya,na mliongezea kuwa Kikwete ni tumaini lililorejea,matokeo yake kila mmoja anayafahamu,kila mmoja matendo na maneno yake yatamtambulisha,Mwl.Nyerere kamaliza safari yake siku nyingi,kwani Magu hawezi kusimama kwa miguu yake mwenyewe au ni wapambe mnatafuta namna ya kumpendeza awatoe,nanyi pia simameni kwa miguu yenu wenyewe
 
Acha kumafananisha Baba wa taifa na vitu vya kijinga
 
Nakubaliana na wewe kwamba Magufuli mara kwa mara anatamka MSEMA KWELI NI MPENZI WA MUNGU. Lakini nakuhakikishia kwamba MAGUFULI SI MSEMA KWELI. mfano mmoja tu. katika bunge lililopita, ambapo wabunge kadhaa wa CCM walichachamaa kuhusu uamuzi wa serikali ya Magufuli kupoka fedha za Export Levy ambapo mfuko huo uliundwa kwa madhumuni ya kukuza zao la Korosho. ni fedha zao wenyewe wadau. katika mzozo wa Bungeni, Magufuli anamsifia Omary Mgumba kwamba NI MSEMA KWELI. lakini alichofanya Mgumba ni kutetea msimamo wa serikali. kwa hiyo kwa Magufuli, kusema kweli ni kutetea serikali. ndio maana watu wanaotetea serikali, popote walipo, mfano Jerry Muro, wanaweza kupata cheo muda wowote.Ukweli unajitegemea, siyo lazima uwe upande wa serikali au wapinzani. Kamusi ya Magufuli ndio inavyosema. Ukweli ni kuunga mkono msimamo wa serikali. Full Stop.

Lakini Nyerere, Naam, huyu alisema kweli. Nyerere alidiriki, katika kitabu cha BINADAMU NA MAENDELEO, kutamka kwamba KANISA LIPAMBANE NA SERIKALI DHALIMU. Kujiamini huku kwa Nyerere kulitokana na nini? unaona jinsi Magufuli anavyohangaika na maaskofu wanaotoa misimamo tofauti na ya Serikali? Kakobe kapekuliwa na kuhojiwa kuhusu uraia, Askofu NiweMugizi pia bado anahojiwa kuhusu uraia wake. na alikosoa msimamo wa serikali kuhusu Katiba.

Kusimamia Misingi, a man of principles, ni sifa mojawapo ya Nyerere. Ni kweli. ndio maana aliwahi kuwatimua waisraeli, wajerumani na wengine, kutokana na misimamo. lakini Magufuli kwamba ni "man of principles?" hapo nina hoja!
mfano mdogo tu. hili wimbi la wapinzani kuhamia CCM kwa kisingizio cha kukunua na sera za awamu ya Magufuli, kuna wakati Mbunge Nassari alifanikiwa kurekodi mazungumzo ya Mkuu wa Wilaya Mnyeti wakati huo, akiongea na mtu wa upinzani ambaye walikusudia kumnunua ili ajiunge na CCM na kutangaza kukunwa na utendaji wa Magufuli. aliachia sehemu ya ushahidi wake hadharani. ilikuwa ni aibu kubwa sana. Lakini Magufuli akawa na MSIMAMO WA KUMLINDA MTOA RUSHWA. Sasa kama Magufuli angekuwa anasimamia misingi, kwanza hilo zali lisingekuwepo. Lakini hata ilipogundulika, hakuchukua hatua yoyote. Misingi gani anayosimamia? mtu unapambana na rushwa, halafu chama chako kinatoa rushwa????

Ila katika mambo ya hovyo, Magufuli ana msimamo. mfano alipanga kubomoa jengo la TANESCO pale Ubungo toka enzi akiwa waziri awamu ya Kikwete wenye busara walimkatalia, kwamba huhitaji kubomoa jengo hilo ili kujenga barabara ile. alipoukwaa urais tu, akaazimia kutekeleza azma yake hiyo mbovu, hata baada ya kushauriwa kwamba inawezekana kujenga barabara bila kubomoa hilo ghorofa. hapo sawa. na aliamuru TANROADS waendelee kubomoa hata nyumba zenye STOP ORDER ya Mahakama, jambo ambalo ni kinyume na sheria na haki za binadamu.. hiyo misimao ya hovyo anayo kwa kweli, nisimkatalie.

-Falsafa ya kazi

Mwaka 1976 Mwalimu aliandika kitabu "kila mtu afanye kazi" kinachoeleza kwa undani umuhimu wa kazi katika maisha binafsi na kwa taifa. Sasa ni miaka 40 Magufuli amekuja na falsafa inayofanana ya "Hapa Kazi Tu".
Sasa hapo umeeleza vizuri wewe mwenyewe. Nyerere aliandika kitabu. alitambulisha FALSAFA. Hii HAPA KAZI TU utasema ni falsafa nayo? ina mwelekeo, ina mpangilio? na nikwambie tofauti kubwa sana ya Magufuli na Nyerere, ni MAENDELEO YA WATU. Kwa Nyerere, watu ndio msingi wa kila kitu. maendeleo yanawalenga watu. lakini Magufuli yeye ni VITU. Maendeleo kwa magufuli ni idadi ya kilometa za barabara, madaraja na kaliveti, flyovers, viwanja vya ndege. na ndiye rais ambaye bajeti ya kilimo ni ndogo kabisa. na hata hiyo kidogo hapeleki. yeye ni kujenga barabara tuuuu.

Jitihada za Nyerere zinajulikana. Hakuongelea kabisa habari ya Tanzania ya Viwanda. Yeye siku zote msisitizo ulikuwa kwenye kilimo. maana ndio UTI WA MGONGO ATI. Lakini awamu ya Tatu chini ya Benjamin Mkapa, ilibinafsisha viwanda vingi tu. inaonekana Tanzania tulikuwa na viwanda vingi sana. sasa Nyerere alivijenga bila hata kutamba. lakini leo chini ya sera ya Tanzania ya viwanda, tunaona tambo nyingi zaidi kuliko uhalisia, na Mwijage akitamba kwamba hata vyerehani vinne ni kiwanda. tunafanya Comedy kwenye mambo serious. na nyerere alikuwa na focus. Ginneries nyingi ziliwezesha processing ya pamba, na viwanda vya mafuta viki process mbegu za pamba. alikuwa anaingia kufanya processing ya korosho. hiyo ndiyo industrialisation focus tunayohitaji. ambayo itahitaji kuboresha kilimo na uzalishaji. Nyerere aliwezesha wakulima kulima, vituo vya utafiti kufanya kazi. Leo vituo vya utafiti vinaminywa hela, pesa yote inakwenda kujenga madaraja, kununua ndege, kuhamia dodoma. hapo kuna focus yoyote ambayo wewe unaiona?


Hapo kwenye madini shida ni kukurupuka. sheria zimepitishwa wangu wangu, bila hata kuhakikiwa vilivyo na wataalamu wetu na pia wawakilishi wa wananchi wetu. zililetwa kwa hati ya dharura. wala hakuna guarantee kwamba sheria mpya zitalinda kweli rasilimali zetu.
 
masahihisho. Nyerere aliwapenda watu wake .
nyerere alijenga nyumba za watumishi wa umma . huyu alisimamia zikauzwa nyingine kwa kina nanio
 
Hiv unaweza. Kumbezza mtumishi wako wa ndani halaf utegemee uwajibikaji?

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wee jamaa msumbufu! Nahc hata hujui vitu vyakufanyia iyo analytical explanation unayoing'ang'ania. Kitu kipo direct kabisa analytical explanation ya nn? Unapenda kuwachosha watu tu apa.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Unauliza aliyasema lini? We jamaa inaonekana humfuatilii huyo unaemsifia. Maana hata speach zake husikilizi. Na ndo maana unauliza ilo swali.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Mwalimu hakua na kichwa cha huyo unayemshobokea
 

Mkuu Nyerere kakukwaza nini mpaka unamfananisha na ...... basi tu naogopa uchochezi
 
Wewe mweupe kichwani utapata wapi arguments za maana? Umejikita katika kudhalilisha na kutoa hoja za kitoto.
Muda wote unaongea mambo yaleyale. Huna option nyingine. Ni kama umekaririshwa.
Huna hoja za maana wewe.
Zijibu kwanza basi hizo, anazirudiarudia kwa sababu hujazijibu!
 
Nchi maskini uchaguz kila kukicha kwann asipige stop ushamba huu
Chaguzi za kijinga, watu wanahama kijinga kwa kupewa hela na bado kina polepole wanachekelea, huu ni ujinga mpya wa karne ya 21
 
Aisee mtoa mada amechezea vitasa si mchezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…