Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

Umekubali Magufuli kashindwa kujieleza kwa staha inayofaa kwa mtukwangazi yake ya uongozi?

Serikali ya nchi yenye mbunge wa upinzani anayepigwa risasi kama target kwenye target practise utasemajeinajivunia amani?
Sijaelewa hapo unamaanisha nini.
Kwanza kabisa ninakuomba usinilishe maneno ambayo sikutamka. Mimi huwa ninasimamia msemo usemao "TUKUBALI KUTOFAUTIANA"
Kwa maana hiyo nilitaka kukuacha uendelee na kile unachoamini ili kwamba tuweze kuendelea kujadili kitu kingine.
Hata kama ningeongea na kutoa mifano mingi usingeweza kuelewa maana umeamua kuegemea upande wa kupinga.
Ndiyo maana nikaja na suala la kuhus peace index kutokana na issue yako ya kusema fujo na kadhalika,
 
"Kukubali kutofautiana" is an oxymoron, an exhibit that the person holding this thought is deranged to the point that he cannot make a decision on whether to agree or disagree.

Mimi sijaandika ninachoamini, nimeandika fact.

Magufuli katoa kauli za kishenzi ambazo hazifai kutolewa na kiongozi wa kitaifa kama yeye.

Mafano wa kauli hizi ni kuwapiga shangazi za watu fulani.

Nyerere hajawahi kutoa kauli za kishenzi zenye kiwango hiki cha ushenzi.

Magufuli nimshenzi kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea kwa rais wa Tanzania.

Mtu mshenzi wa kiwango hiki cha kukosa staha japo kwenye kauli tu, huwezi kusema kwamba anarudisha maadili serikalini.
Huwezi kumlinganisha na kiongozi ambaye alijiheshimu japo kwa kauli tu kama Nyerere.

Magufuli ni mshenzi tu.

Sasa mshenzi ataletaje maadili?

Umeshindwa kupinga hoja hii.

Kwa sababu ni ukweli.
 
Mi ndahani hizo hela zilizonunua ndege tungetafuta eneo lenye madini (virgin) tukanunua mitambo na hata wataalamu tukachimba madini wenyewe ingelipa zaidi na mapema. Siku hizi kuna kukaririshwa maneno na watu wanafuata hivyo hivyo! Hii dhana ya kuwa ndege zitaongeza watalii nina shaka nayo, sidhani kama watalii walikua wanashindwa kuja Tanzania kwa sababu hatuna ndege! This is very shallow thinking!
 
Tukiacha mengine mengi ambayo huwezi kuweka ulinganisho, la muhimu zaidi kwangu na kwa wengi, Mwalimu alituunganisha kama taifa, tukawa mfano wa kuigwa si Africa tu, bali duniani kote. Mwalimu aliipenda Tanzania na waTanzania kwa moyo safi bila ya kujitafutia sifa binafsi. Mwalimu alikuwa na MZALENDO by any definition you want to use. Mwalimu alikuwa ni mcha Mungu. Mwalimu was a gifted intellect.
 
Na mwalimu aliua ukabila kabisa, sasa hivi tunaasisi upya ukabila!
 
Mkuu nakukubali sana uwa unajibu vizuri sana
 
Jamani hata kama tunatafuta vyeo tuache unafiki wa kichawi.....eti jiwe na baba wa taifa wanawekwa kapu moja kweli???
 
Mkuu nakukubali sana uwa unajibu vizuri sana

Katika nyakati kama hizi ambazo wapiga zumari wa watawala wanataka kutuaminisha kwamba suti ya mfalme ni nzuri sana, na inaonekana kwa wale wenye busara tu, inawezekana watakaoona mfalme anatembea uchi wataogopa kusema "mbona mfalme yupo uchi?" kwa sababu wataonekana hawana busara.

Nakataa ujinga huo, ni bora nionekane mjinga kwa kuukataa ujinga kuliko kuonekana mwerevu kwa kuogopa kuonekana mjinga kunakotokana na kukemea ujinga.

Katika uongozi, kauli ina uzito sana. Inaweza kukuza uchumi, inaweza kuanzisha vita.

Sasa tutalazimishaje kiongozi asiyejua kuitawala kauli yake tu kama Magufuli ni kiongozi mzuri sana wa kulinganishwa na Nyerere, mtu aliyeweza kuongea kwa dhana za enlightenment Europe, akazichanganya na malezi na mafunzo ya Kiafrika, na kujaribu kuleta mfumo mpya duniani, watu wanaoendesha dunia wakamsikiliza kama "philosopher king" ?

Nyerere was a "philosopher king". Ukubaliane naye, usikubaliane naye, alikuwa "philosopher king".

Alikuwa na mawazo mazito, kayaandika, yamechambuliwa, alikuwa coherent.

Kama alishindwa utekelezaji kiuchumi hilo ni suala jingine.

Magufuli hajui hata anataka kwenda wapi na afikeje anakotaka kwenda, kuna mtu ana kitu comprehensive alichoandika Magufuli?

Magufuli anaweza kujieleza kwa saa nzima bila kujikanyaga na kuji contradict mwenyewe na kutishia mambo ya kijinga kama kupiga shangazi za watu?

Huyu ni mtu wa kumfananisha na Nyerere?

Msikilize Nyerere alivyokuwa anahutubia Bunge la Africa Kusini, alivyopiga "immanent critique" habari ya nationalism in Africa.

Nyerere alipiga sommersault katika hotuba kama mpiga sarakasi hodari, kama rapper ningesema ali flow kama Big Daddy Kane akaliacha beat haraka sana akarudi kwenye mstari kuonesha ana command the flow!

Mzee kwanza kaanza na African nationalism, unamsoma unasema huyu anaenda kutoa hotuba iliyo nationalistic.

Halafu hapo ndipo Guru alipokuambia "I left right and go right",akiashiria mbinu za kucheza basketball, kwamba mchezaji anaweza kukuchuza kama anakwenda kushoto, ukijipanga kumkaba kushoto, mwenzako anakwenda kulia.

Nyere alipiga fake Bunge la Afrika Kusini wabunge wakasema hiki kichwa kimekomaa kwa hoja, maana kinaichambua hoja kinayotaka kuipinga kama nzuri kwanza, halafu kinaiponda, kinakueleza upande wa pili wa hoja na kwanini huo ni mzuri zaidi.

Magufuli sijawahi kumsikia akichambua mambo with that depth at that level.

Hapo hapo akapiga U-Turn, anasagia African nationalism, unasema ayaa wee, mzee anazeekavibaya nini? Mbona kama anajipinga?

Halafu anaanza kukuelezealogically the fallacy of African nationalism, kwamba hivi vinchi tumepewa na wakoloni tu,vingine tumeviunda wenyewe maishani mwetu (Tanzania) anakuja na grand scheme sasa ya pan Afriacinst vision.

Ukimsikiliza unaona burudani, unajua kwanini huyu anaitwa Mwalimu. Hata kamakashindwa imlplementation, ana vision, inaeleweka.

Magufuli hata kuongea tu tabu.

Unaweza kuwafananisha hawa wawilikweli?

Nakuomba msikilize Nyerere hotuba ya Bunge la South Africa, halafu tafuta sehemu Magufuli anapoongea with eloquence and leadership kama hivyo utuwekee hapa.

Kauli ina matter katika uongozi.
 
Utumishi wa umma umeimarika..?? Kuna mkurugenzi kakataa kutoa fomu kwa mgombea, kisa siyo wa chama chake!
Hv kweli Nyerere angeweza kufanya huu ufisadi wa kuchezea mabilioni ya walipa kodi kununua wanasiasa na kurudia uchaguzi kila wakati? Embu acha utani ndg!
 
Kwa namna unavyoandika inaonesha kuna maslah yako yameguswa.
Tukija kwenye muktadha huu huu unaousema hapa kuhusu kuamini na facts, kwa evidences zipi unaweza kusema hizi ni tabia za kishenzi na hizi siyo za kishenzi!?
Nikisema ni definition tu unataka kuueleza umma kutokana na mambo yako binafsi nitakuwa nimekosea!?

Je, unauhakika unachokisema wewe ni right!? Je, unaweza kufafanua zaidi!?
 
Unazungumzia vitu vizito sana ambavyo elimu yetu ya sasa haiviruhusu kuvielewa.
 
Asante sana mkuu ila lumumba buku 7 awawezi kukuelewa ata siku moja wao kazi yao ni kusifia tu
 
Maslahi yangu hayajaguswa, in fact utawala huu umenifaidisha sana.

Nina wazee wangu mpaka kwenye cabinet.

Dar familia yangu tumepewa nyumba iliyokuwa ya serikali, Oysterbay. Ilikadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni tatu.

Kwa hivyo, mimi kama ningekuwa mtu wa kuangalia maslahi, ningekuwa mtu wa kushangilia utawala wa Magufuli.

Sijaangalia maslahi, naangalia kanuni.

Kuhusu ushenzi, mtu kiongozi anayetangaza kutaka kuwapiga shangazi za wapinzani wake, shangazi ambao hawajamkosea kitu, ni mshenzi.

Hajuikwamba, kiumeni, kwa ustaarabu wa leo, hatufagilii habari z akupiga wanawake.
Hatufagiliihabari za kutumianguvu, tunatumia hoja.

Zaidi, hata inapobidi kutumia nguvu, unatumia nguvu dhidi ya wapinzaniwako wa mojakwamoja, si shangazi zao ambao inawezekana hawajui lolote kuhusu ugomvi wenu.

Kwa msingi huu, Magufuli ni mshenzi,hana maadili.
 

Kutokana na majibu kama haya, ni wazi kwamba huelewi kiranga anasema nini. Au ni basi tu unajikaza kiume uendelee kuonekana unashuparia mjadara usiokuwa na kichwa au miguu uliouanzisha.
 
Safi sana Mkuu kwa Darasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…