Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Hujaelewa hata ninachoandika, ama hilo, ama unajitoaakili.Hapa ndipo ninapokuja kusema kuwa ni mtazamo wako. Huo mtazamo wako hauondoi ukweli kwamba nidhamu kwenye ofsi za umma umeongezeka. Watu wanawahi kazini wanafanya kazi zao za kuhudumia wananchi kwa kiwango.
Huu ndio ukweli ambao unaonekana lakini wewe unaukana hadharani.
Wananchi hawahitaji maneno matamu ya kubembelezwa, wananchi wanahitaji services za uhakika. Wananchi wanahitaji maji, huduma hospitalini na huduma zingine za kijamii.
Tunaposema uwajibikaji ni kuhudumia wananchi. Mimi siwezi kubadili mtazamo wako lakini facts nitazieleza. Na baada ya hapo utaelewa kwanini nchi zingine Afrika zinaiga policy za JPM.
Mtazamo wako umeuekelekeza katika negativity thoughts so ni vigumu sana kukufanya uone chochote maana tayari umejiwekea msimamo mwenyewe. Lakini kama ungekuwa flexible ungeona kitu gani tunaongelea.
Unajua kwamba mtu anayekuchukia hata ufanye mazuri kiasi gani atakuongea vibaya tu. Haya mambo yapo hata sehemu tunazoishi. So hiyo ni mitazamo tu, ya mtu binafsi haiwezi kuondoa ukweli wa mambo makubwa yanayofanywa na JPM.
Kwamba nidhamu inaongezeka si hoja niliyoipinga.
Nimepinga hojakwamba Magufulini kinara wa nidhamu.
Inawezekana Magufuli akawa hajali nidhamu (ndiyo maana ana kauli za kishenzi) na anatakakuonekana anasisitiza nidhamu ilikupata points za kisiasa na kuogopesha watu.
Mtu anayefanya ushenzi wa kigubegubekwa kauli varuvaru hawezi kuwa kinara wa nidhamu.
Anaweza kutumiasuala la nidhamu kujenga uoga miongoni mwa wafanyakazi wa serikali, lakinihilo halina maana kwamba huyu ni kinara wa nidhamu.
Angekuwa kinara wa nidhamu tungemuona hata kwa kauli zake tu.
Sina sababu ya kumchukia Magufuli, nishasema kaifaidisha sana familiayangu, sasa nimchukie mtu aliyeifaidisha familiayangu kwa sababu gani?
Mimi naongelea principles tu.
Hutakiwi kusema mtumwenye kauli mbovu kama Magufuli kwamba ni kinara wa nidhamu.
Utaonekana hujui kinara ni nini wala ndihamu inafafana vipi.