Hujaelewa hata ninachoandika, ama hilo, ama unajitoaakili.Hapa ndipo ninapokuja kusema kuwa ni mtazamo wako. Huo mtazamo wako hauondoi ukweli kwamba nidhamu kwenye ofsi za umma umeongezeka. Watu wanawahi kazini wanafanya kazi zao za kuhudumia wananchi kwa kiwango.
Huu ndio ukweli ambao unaonekana lakini wewe unaukana hadharani.
Wananchi hawahitaji maneno matamu ya kubembelezwa, wananchi wanahitaji services za uhakika. Wananchi wanahitaji maji, huduma hospitalini na huduma zingine za kijamii.
Tunaposema uwajibikaji ni kuhudumia wananchi. Mimi siwezi kubadili mtazamo wako lakini facts nitazieleza. Na baada ya hapo utaelewa kwanini nchi zingine Afrika zinaiga policy za JPM.
Mtazamo wako umeuekelekeza katika negativity thoughts so ni vigumu sana kukufanya uone chochote maana tayari umejiwekea msimamo mwenyewe. Lakini kama ungekuwa flexible ungeona kitu gani tunaongelea.
Unajua kwamba mtu anayekuchukia hata ufanye mazuri kiasi gani atakuongea vibaya tu. Haya mambo yapo hata sehemu tunazoishi. So hiyo ni mitazamo tu, ya mtu binafsi haiwezi kuondoa ukweli wa mambo makubwa yanayofanywa na JPM.
Credible katika lipi kwa suala hili nililoleta?Maswali mengi mno wakati sentensi yangu ni moja tu. Unaweza ukathibitisha kuwa Wikipedia ni credible source!?
Angalau sasa umeanza kunielewa.Hujaelewa hata ninachoandika, ama hilo, ama unajitoaakili.
Kwamba nidhamu inaongezeka si hoja niliyoipinga.
Nimepinga hojakwamba Magufulini kinara wa nidhamu.
Inawezekana Magufuli akawa hajali nidhamu (ndiyo maana ana kauli za kishenzi) na anatakakuonekana anasisitiza nidhamu ilikupata points za kisiasa na kuogopesha watu.
Mtu anayefanya ushenzi wa kigubegubekwa kauli varuvaru hawezi kuwa kinara wa nidhamu.
Anaweza kutumiasuala la nidhamu kujenga uoga miongoni mwa wafanyakazi wa serikali, lakinihilo halina maana kwamba huyu ni kinara wa nidhamu.
Angekuwa kinara wa nidhamu tungemuona hata kwa kauli zake tu.
Sina sababu ya kumchukia Magufuli, nishasema kaifaidisha sana familiayangu, sasa nimchukie mtu aliyeifaidisha familiayangu kwa sababu gani?
Mimi naongelea principles tu.
Hutakiwi kusema mtumwenye kauli mbovu kama Magufuli kwamba ni kinara wa nidhamu.
Utaonekana hujui kinara ni nini wala ndihamu inafafana vipi.
Katika nyakati kama hizi ambazo wapiga zumari wa watawala wanataka kutuaminisha kwamba suti ya mfalme ni nzuri sana, na inaonekana kwa wale wenye busara tu, inawezekana watakaoona mfalme anatembea uchi wataogopa kusema "mbona mfalme yupo uchi?" kwa sababu wataonekana hawana busara.
Nakataa ujinga huo, ni bora nionekane mjinga kwa kuukataa ujinga kuliko kuonekana mwerevu kwa kuogopa kuonekana mjinga kunakotokana na kukemea ujinga.
Katika uongozi, kauli ina uzito sana. Inaweza kukuza uchumi, inaweza kuanzisha vita.
Sasa tutalazimishaje kiongozi asiyejua kuitawala kauli yake tu kama Magufuli ni kiongozi mzuri sana wa kulinganishwa na Nyerere, mtu aliyeweza kuongea kwa dhana za enlightenment Europe, akazichanganya na malezi na mafunzo ya Kiafrika, na kujaribu kuleta mfumo mpya duniani, watu wanaoendesha dunia wakamsikiliza kama "philosopher king" ?
Nyerere was a "philosopher king". Ukubaliane naye, usikubaliane naye, alikuwa "philosopher king".
Alikuwa na mawazo mazito, kayaandika, yamechambuliwa, alikuwa coherent.
Kama alishindwa utekelezaji kiuchumi hilo ni suala jingine.
Magufuli hajui hata anataka kwenda wapi na afikeje anakotaka kwenda, kuna mtu ana kitu comprehensive alichoandika Magufuli?
Magufuli anaweza kujieleza kwa saa nzima bila kujikanyaga na kuji contradict mwenyewe na kutishia mambo ya kijinga kama kupiga shangazi za watu?
Huyu ni mtu wa kumfananisha na Nyerere?
Msikilize Nyerere alivyokuwa anahutubia Bunge la Africa Kusini, alivyopiga "immanent critique" habari ya nationalism in Africa.
Nyerere alipiga sommersault katika hotuba kama mpiga sarakasi hodari, kama rapper ningesema ali flow kama Big Daddy Kane akaliacha beat haraka sana akarudi kwenye mstari kuonesha ana command the flow!
Mzee kwanza kaanza na African nationalism, unamsoma unasema huyu anaenda kutoa hotuba iliyo nationalistic.
Halafu hapo ndipo Guru alipokuambia "I left right and go right",akiashiria mbinu za kucheza basketball, kwamba mchezaji anaweza kukuchuza kama anakwenda kushoto, ukijipanga kumkaba kushoto, mwenzako anakwenda kulia.
Nyere alipiga fake Bunge la Afrika Kusini wabunge wakasema hiki kichwa kimekomaa kwa hoja, maana kinaichambua hoja kinayotaka kuipinga kama nzuri kwanza, halafu kinaiponda, kinakueleza upande wa pili wa hoja na kwanini huo ni mzuri zaidi.
Magufuli sijawahi kumsikia akichambua mambo with that depth at that level.
Hapo hapo akapiga U-Turn, anasagia African nationalism, unasema ayaa wee, mzee anazeekavibaya nini? Mbona kama anajipinga?
Halafu anaanza kukuelezealogically the fallacy of African nationalism, kwamba hivi vinchi tumepewa na wakoloni tu,vingine tumeviunda wenyewe maishani mwetu (Tanzania) anakuja na grand scheme sasa ya pan Afriacinst vision.
Ukimsikiliza unaona burudani, unajua kwanini huyu anaitwa Mwalimu. Hata kamakashindwa imlplementation, ana vision, inaeleweka.
Magufuli hata kuongea tu tabu.
Unaweza kuwafananisha hawa wawilikweli?
Nakuomba msikilize Nyerere hotuba ya Bunge la South Africa, halafu tafuta sehemu Magufuli anapoongea with eloquence and leadership kama hivyo utuwekee hapa.
Kauli ina matter katika uongozi.
Ona sasa unakimbilia kuniambia sijui kusoma kingereza. Mimi nimekuuliza swali fupi tu uniambie na kunithibitishia kuwa wikipedia ni credible source.Credible katika lipi kwa suala hili nililoleta?
Usikariri tu kwamba Wikipedia si credible source wakati kumbe hata kusoma Kiingereza kilichoandikwa hujui!
Umesoma lipi katika hiyo Wiki ukaona Wikipedia wamekosea?
Nakwambia hivi,hutakiwi kusema mtu mshenzi mshenzi kama Magufuli ni kinara wa nidhamu serikalini.Angalau sasa umeanza kunielewa.
Sasa suala hapa unataka Magufuli afanane kabisa na mtu wa kusadikika au mtu asiyekemea wala rushwa. Mtu anayekemea rushwa na uharibifu wa mali za umma lazima ataonekana kauli zake siyo nzuri kwa baadhi ya watu.
sindano huwa inauma sana, kakini ndiyo tiba yenyewe. Ukipata kiongozi mwenye kauli tamu, mwenye kuendekeza muzaha nchi haiwezi kusogea.
Tunahitaji kusogea mbele na sio kuchekeana kwa kauli tamu tamu huku wabaya wakihujumu nchi.
Nchi inahitaji kusonga mbele zaidi ya kupeana kauli laini laini.
Kwa ni mimi nimekupa Wikipedia source au Wikipedia source ya specific subject?Ona sasa unakimbilia kuniambia sijui kusoma kingereza. Mimi nimekuuliza swali fupi tu uniambie na kunithibitishia kuwa wikipedia ni credible source.
Naweza kukupa multiple choice.
Je Wikipedia ni credible source?
A. Ndio
B. Sio
C. Sijui
Hapa ndipo wahenga husema patamu.Nakwambia hivi,hutakiwi kusema mtu mshenzi mshenzi kama Magufuli ni kinara wa nidhamu serikalini.
Ukisema hivyo utakuwa umeikosea nidhamu nidhamu.
Wikipedia any person can contribute so inaondoa credibility ya hiyo source. Je, una la kupinga mpaka hapo!? Na hakuna sehemu inaandikwa hii ni verified topic.Kwa ni mimi nimekupa Wikipedia source au Wikipedia source ya specific subject?
Na katika hiyo Wikipedia source ya specific subject, nikikwambia ni credible, na huwezi kuikosoa, utasemaje?
Unaweza kuikosoa Wiki niliyoileta?
Mimi nimekwambia Magufuli si kinara wa nidhamu, kwa sababu ni mshenzi mshenzi,ana kauli za kishenzi, hawezikufananishwa na Nyerere.
Very specific objection.
Wewe una objection gani specific to the Wiki?
Sheria ya kwanza ya kufananisha inatutaka tufananishe vinavyofananishika, wewe hujaijua hiyo sheria unafananisha visivyofananishika.Hapa ndipo wahenga husema patamu.
Iweje wewe ulete utemi wa kuona mtu anayeandika tofauti na wewe amekukosea nidhamu!?
Je, ingetokea wewe ni kiongozi si ingekuwa hatari sana!?
Back to topic. Tunaongelea utendaji wa JPM kuelekea ukombozi wa nchi kiuchumi, utendaji huu unafananishwa kabisa na utendaji wa Mwalimu Nyerere katika harakati za ukombozi wa nchi kisiasa.
Hata hapa JF kila mtu anaweza ku contribute, kwa hiyo habari zote ulizoandika ni za uongo?Wikipedia any person can contribute so inaondoa credibility ya hiyo source. Je, una la kupinga mpaka hapo!? Na hakuna sehemu inaandikwa hii ni verified topic.
Acha kukufuruLeo ninawaletea ufafanunuzi wa mambo yanayoashiria ufanano wa kiutendaji kati ya Mwl Nyerere na Ndg Magufuli Mwkt wa CCM na Rais wa Tanzania, kwa kuwa viongozi hufananishwa na hutofautishwa kwa utendaji wao katika kutoa uongozi.
-Ukweli
Mwalimu mwanzoni mwa miaka ya 1960 alipojiuzulu Uwaziri Mkuu kwenda kujenga Chama nakumuachia Serikali Mzee Kawawa, aliandika vitabu vitatu kimojawapo ni TUJIJISAHIHISHE ni kitabu kidogo chenye kurasa zisizozidi ishirini ambapo amesisitiza katika kusema kweli na neno Kweli limetajwa zaidi ya mara ishirini.
"Ukweli unatabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.."
Hayo ni baadhi ya maneno katika kitabu hicho, yanayosisitiza kusema ukweli na kuheshimu ukweli. Hii ni sawa kabisa kwa Magufuli ambaye toka awali amekuwa ni kiongozi anayesisitiza kusema ukweli na kwa sasa ni mwasisi wa msemo "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu".
-Kusimamia Misingi
CCM ina msingi wa vitu viwili, Haki na Watu. Mwalimu mwaka 1968, akitoa hotuba aliyoiita, "Lazima Chama Kiwasemee watu" na moja ya kauli zake ni, "kazi ya Chama cha Siasa kilicho imara ni lazima kiwe kama daraja la kuwaunganiaha watu na serikali walioichagua." Mwalimu alisema akiwaasa viongozi wa Chama kuwa karibu na wananchi na kuwa watetezi wa haki za wanyonge.
Hiyo tunaishuhudia tena kwa Magufuli ambapo kwa kiasi kikubwa amekuwa akiwasisitiza viongozi wa Chama kuwa sikio la wananchi na hata mageuzi ya Chama yamelenga kukifanya kuwa "Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu"
-Falsafa ya kazi
Mwaka 1976 Mwalimu aliandika kitabu "kila mtu afanye kazi" kinachoeleza kwa undani umuhimu wa kazi katika maisha binafsi na kwa taifa. Sasa ni miaka 40 Magufuli amekuja na falsafa inayofanana ya "Hapa Kazi Tu".
- Sera ya Viwanda na Kilimo
Mwalimu aliweza kuanzisha programu za kilimo ikiwemo "utekelezaji wa siasa ni kilimo" - 1974, sera ya viwanda vidogo vidogo (SIDO), vya kati ikiwemo viwanda vya nguo urafiki, Mwatex, Mutex, Mbeyatex, n.k Sawa kabisa na Magufuli ambaye ndoto yake ni Viwanda. Miezi miwili iliyopita amezindua mradi mkubwa wa kilimo awamu II utakaogusa maisha ya wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo nafuu ya kilimo.
-Udhibiti wa madini
Katika suala la madini Mwalimu alifanya utambuzi wa maeneo yenye madini, hakuruhusu uchimbaji uanze mbali na changamoto tulizokuwa tukizipitia kama Taifa, kwa kuwa Watanzania hatukuwa na elimu ya kutosha ya Madini. Magufuli amekuja amekuta mikataba kandamizi iliyoingiwa na watangulizi wake baada ya mwalimu hivyo ameifumua mikataba yote ya Madini na kufanya haki ya mtanzania kuheshimiwa na kuweza kuingia makubaliano kutoka 3% ya awali mpaka 50/50%.
- Reli, Umeme na Anga.
Mwalimu aliweza kujenga Reli ya TAZARA miaka ya 1970, kwa upande mwingine alikuwa na ndoto kubwa ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme maarufu kama Stiegler's Gorge ambao ulikwamishwa, shirika la ndege lilikuwa na ndege za AirTanzania kabla halijafa katika awamu zilizofuata. Miaka 30 sasa Magufuli amefufua shirika la ndege na mpaka sasa serikali imefanikiwa kununua ndege Saba ndogo za kati na kubwa. Ujenzi wa Reli ya kisasa unaendelea naujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler's Gorge umeanza.
Vijana wa miaka ya 1990, Nyerere tunayesimuliwa nakumsoma amerejea katika sura ya Magufuli na ni jukumu letu kumpa ushirikiano na kufanya naye kazi kuhakikisha tunatekeleza na kufikia ndoto ya TViwanda.
Na mwandishi wetu,
Said Said Nguya
Saidnguya@gmail.com
Ukiweka heading ya kipuuzi usitegemee mtu asome content! Tunafanya skimming tunakomentiSoma kwanza rafiki ndipo uweke comment.
Mbona tunarudi tena tulikotoka!? Wewe umeweka mtazamo wako. Huo ni mtazamo wako binafsi, sasa usilazimishe wengine wawe na mtazamo huo.Sheria ya kwanza ya kufananisha inatutaka tufananishe vinavyofananishika, wewe hujaijua hiyo sheria unafananisha visivyofananishika.
Umeanza kwa uongo kwamba Magufuli ni kinara wa kurudisha nidhamu serikalini.
Tumeona kwamba Magufuli kwanza kabisa hawezi kuwa kinara wa nidhamu kwa sababu hata kuongea tu, anaongea bila nidhamu na kishenzishenzi kama baharia mlevi.
Ndio maana wewe ni kati ya ninaowaheshimu sana jfHakuna mada ya kujadili mkuu Nyerere na JPM wapi na wapi mkuu? Nyerere hakuzuia mikutano ya siasa,Nyerere aliunga sera za vyama vingi ingawa baadhi ya washauri wake walimwambia akatae kwa sababu waliokubali walikuwa 20% lakni nyerere hakuwapuuza hao 20%,Nyerere aliktaaa kuishi kwenye jumba la milioni 100 aliyojengewa alitaka aishi kwenye nyumba yake ya kawaida,Nyerere hakuwahi kujengea kimada hotel,nyerere hakugawa vyeo kama njugu kwa mademu na wapiga ngenga wakumsifia,nyerere hakuiba fedha za serikali kama 1.5T ilivyopigwa,Nyerere hakufanya manunuzi ya serikali bila kushirikisha bunge,Nyerere hakuwapa nafasi wanae kwenye serikali yake ,Nyerere haku .......Mambo ni mengi sana mkuu,NDIO maana nikakwambia Weka Namba ya simu ugewe Shavu,Awamu hii wewe jitoe akili tu sifia wewe sifia siku utakuja stukia unapigiwa simu umekuwa DAS ndio maana nikakushauri weka namba ya simu.
Wamfananishe mara mbili?.Muda si mrefu MaCCM yatalifananisha jiwe na Mungu.