Mwalimu Nyerere na Dkt. Magufuli ndio wanaonekana marais bora, ila ndio marais wabovu kuliko wote

Watu unaowaongelea wawe na elimu na wawe hawawezi kurubuniwa kwa kipande cha kanga na kofia !! Otherwise tunadanganyana !!
 
Watu unaowaongelea wawe na elimu na wawe hawawezi kurubuniwa kwa kipande cha kanga na kofia !! Otherwise tunadanganyana !!
Huu ni ujinga ambao kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na Nyerere

Chama dola na serikali yenye kuhodhi kila kitu, vimepumbaza na kulemaza Sana wananchi

Na hili linaweza kubadilika Kama Marais wanaokuja watawajengea wananchi spirit ya ujasiri, spirit ya kutokuona Serikali ndio kila kitu

Kama Kuna Kijiji hakina zahanati nchi yenye mwananchi aweze kujenga zahanati binafsi na sio kukaa kuisubiria serikali
 
Uk
UkiTaka kujenga nyumba imara lazima kwanza uweke msingi imara ! China walianzishwa kwanza kuwekwa kwenye misingi imara ya kizalendo kisha baada ya kuonekana kuwa wameshafaulu ndio nyumba imara ikaanza kujengwa ndio maana China ukila Mali ya Umma wanakunyonga maana wanajua wewe sio mwenzao !! Wakikushika na madawa ya kulevya wanakunyonga maana wanajua wewe sio mwenzao !! Sisi tuliidharau ile misingi imara tukaanzisha yetu ya dili dili dili kwa Kwenda mbele !! Ndio maana Leo tuna miaka 60 ya Uhuru bado tunazungumzia madawati na maji safi !!
 
Ukinitolea mfano wa China, Mimi naweza kukutolea mfano wa nchi 50 ambazo haijafuata model ya China na zimefanikiwa muda mrefu kabla hata ya China

Halafu adui mkubwa wa nchi ni ujinga na uvivu,
hata Kama taifa lina 0 ufisadi Ila lina watu ambao ni wavivu, wasio wabunifu, wanaoililia serikali kwenye kila kitu, itakuwa imedumaa

Ila likiwa na watu wachapakazi, wabunifu na majasiri hata kukiwa na ufisadi bado litapiga hatua sababu uzalishaji itakuwa mwingi kuliko kinachoibwa

Nchi Kama Marekani miaka ya 1900 ilikuwa na ufisadi kuliko hata hapa Tanzania ya leo, lakini uzalishaji na ubinifu ilikuwa mkubwa na ika offset Ile hasara ya ufisadi

Kipindi Cha Magufuli ambapo ndio Tanzania ilikuwa ikisemwa imedhibiti ufisadi na Kenya ikitajwa Kama nchi ya kifisadi zaidi, lakini ukianagalia takwimu Kenya ilikuwa kiuchumi zaidi kipindi hicho kuliko Tanzania, sababu ni wananchi wanaofanya kazi
 
Wewe utakuwa unaishi dunia ya peke yako kama hujui kwamba matajiri ndio vitegemezi wakubwa wa serikali.

"Sera mbovu kiuchumi," ni wapi palipokuwa na sera nzuri kiuchumi paliponeemeka hapa barani Afrika? Hujui matatizo ya uchumi yaliyokuwa yanaikumba dunia nzima nyakati hizo? Unajisahaulisha tu mradi ukidhi dhana yako potofu juu ya sera za uchumi za Nyerere na kuziimba tu kama kasuku?

Haya, tuambie, China kwa sasa ambayo ina mamilionea, walianzia wapi hao mamilionea? Na hapo ulipo na akili yako unadhani serikali ya China iliwatupa mbali maskini wao kwa vile sasa wamepatikana mamilionea wengi?
 
Halafu adui mkubwa wa nchi ni ujinga na uvivu,
hata Kama taifa lina 0 ufisadi Ila lina watu ambao ni wavivu, wasio wabunifu, wanaoililia serikali kwenye kila kitu, itakuwa imedumaa
Unaonyesha wazi hujui wapi pa kuelekeza lawama zako.
Na mtu kama wewe ukiwa kiongozi ndiyo kila kitu kitaharibika kabisa, kwa sababu hujui tatizo liko wapi, kumbe tatizo ni wewe mwenyewe kama kiongozi.
 
Tanzania ni moja ya nchi za mwisho kabisa Africa kufikia uchumi wa kati

Wastani wa kipato cha mwananchi ni kidogo mno ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya, Botwasana, Namibia, South Africa
Sera mbovu,
 
Viongozi kama Nyerere na Magufuli ndio viongozi bora? Walifanya nini kukuza uchumi? Zaidi ya kupunguza kasi ya ukuaji wake
 
Viongozi kama Nyerere na Magufuli ndio viongozi bora? Walifanya nini kukuza uchumi? Zaidi ya kupunguza kasi ya ukuaji wake
Unaniuliza swali la kipuuzi unapounganisha kwa pamoja viongozi hao bila kujali mambo mengine yaliyofanyika wakati wa uongozi wao.

Wewe kuniuliza juu ya uongozi wa Mwalimu Nyerere inaonyesha wazi unaupungufu kwenye fikra zako juu ya uongozi.
 
Tanzania ni moja ya nchi za mwisho kabisa Africa kufikia uchumi wa kati

Wastani wa kipato cha mwananchi ni kidogo mno ukilinganisha na nchi nyingine kama Kenya, Botwasana, Namibia, South Africa
Sera mbovu,
Kwa hiyo mifano uliyoweka hapo ndio nchi nyingi za afrika zilizofikia uchumi wa kati? Na kwa akili yako, unadhani mwananchi wa kawaida wa Kenya anayo hali bora zaidi ya mwananchi wa Tanzania? Unajua Turkana, Baringo, Isiolo, Kilifi, na hata Kisumu zilipo? Huko hakuna wananchi ambao ni wakenya?
Wewe unadhani hayo maua yanayolimwa na wazungu na kuuzwa nje ni hela inayoingia moja kwa moja mifukoni mwa mwananchi wa Kenya?
 
Unaniuliza swali la kipuuzi unapounganisha kwa pamoja viongozi hao bila kujali mambo mengine yaliyofanyika wakati wa uongozi wao.

Wewe kuniuliza juu ya uongozi wa Mwalimu Nyerere inaonyesha wazi unaupungufu kwenye fikra zako juu ya uongozi.
Wewe ndio mpuuzi mkubwa, tena mpumbavu, mimi wa kukuuliza ndio, kwani wewe ni nani?
Unajifanya mjuaji unaulizwa unarukaruka na blah blah kibao

Nimekuita kuja kuchangia huu uzi? Si umejileta mwenyewe ukijibiwa unanata?
 
Kwani kipato cha mfanyakazi wa kawaida Kenya kama mwalimu ni kiasi gani ukilinganisha na mwalimu wa Tanzania?

Masikini wapo Kenya, China, Marekani na kila mahali, ila tunaangalia kiwango cha umasikini kipoje
 
Wengine wameshaanza kusema Ngada iko kwenye mfumo wa dunia na inawakwamua vijana !! Maana yake waachiwe tu !! Hatari sana !!
Sitashangaa kama huyu aliyeleta mada hii hapa jukwaani hayupo chini ya 'influence' ya "Ngada", maanaeke anayoyatetea siyo ya mtu mwenye akili iliyo timamu.
Kwa mfano, yeye anaona ufisadi ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya nchi!
 
Wewe ndio mpuuzi mkubwa, tena mpumbavu, mimi wa kukuuliza ndio, kwani wewe ni nani?
Unajifanya mjuaji unaulizwa unarukaruka na blah blah kibao

Nimekuita kuja kuchangia huu uzi? Si umejileta mwenyewe ukijibiwa unanata?
Unapoleta takataka hapa ni lazima uambiwe. Hii uliyoweka hapa ni takataka.
 
Kwa wavivu na wapenda vya mtelemko wanaonaglia matumbo yao tu, Kikwete na Samia ndio marais bora. Kwa wachapa kazia na wanaoangalia maslahi ya taifa kwa vizaizi vijavyo wanajua kuwa Nyerere na Magufuli walikuwa marais bora sana. Hivyo kipimo ubopra wa rais kinategemea zaidi mtu yuko upande gani wa mizani.
 
Kwani kipato cha mfanyakazi wa kawaida Kenya kama mwalimu ni kiasi gani ukilinganisha na mwalimu wa Tanzania?

Masikini wapo Kenya, China, Marekani na kila mahali, ila tunaangalia kiwango cha umasikini kipoje
Walimu wapo wangapi Kenya? Hilo kundi dogo nalo ni la kulitolea mfano?

Sasa kama Kenya walimu wanalipwa kiasi kikubwa na matumizi yao yakawa juu kuliko walimu walioko Tanzania, hiyo nayo ni habari?

Jinsi unavyowasilisha maoni yako hapa, ninashawishika kusema kuwa wewe ni mtu wa huko huko Kenya. Mara nyingi mnajivimbisha bure kwa vitu msivyokuwa navyo.
 
Akili yako kisoda akijai

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Correct.
 
Nyerere ndiye Baba wa Yote.
Mema na mabaya.
Nyerere ndiye Baba wa katiba na Chama kilichowapata Marais wote waliofuata

Hivyo ni upumbavu na ulofa kumlinganisha Mtoto na baba yake. Ni laana kubwa.

Tutamlinganisha Nyerere na Rais atakayetuletea katiba mpya mana atakua ametengeneza dira mpya ,siasa mpya na mifumo mipya ya uongozi katika Taifa hili.

Mifumo iliyopo ama imefanya vizuri au vibaya ni zao la Mwalimu.

Magufuli ni mshiriki tu wa ama kujenga mazuri au mabaya kama walivyo wengine ,ndio maana awamu zote zilizomfuata Nyerere zilikuwa na wizi na upigaji mkubwa wa kujinufaisha kila Kona.

SSH anaweza kuwa Rais wa Tofauti sana endapo ataleta katiba mpya ya Wananchi ili kazi yake iwe kuongoza na kushughulikia mafisadi Kwa matakwa ya Katiba. Yaani ukiiba ukiwa Kiongozi wa umma unajiondia Mwenyewe TU mana Tume ya maadili itakuumbua.
Kwa Sasa Waziri anaweza akamiliki Mali zenye majina ya wajukuu ambao hawajazaliwa lakini hakuna wa kumhoji mpa aliyemteua aamue kumtoa au kumwachia kirafiki au kindugu.

Kiongozi anakalia ofisi Kwa cheti feki badala ya kuchunguzwa anaambiwa chapa Kazi.

Kundi kubwa la watawala ni walioptatikana Kwa wizi wa kura. Hao hawana muda wa kujenga nchi ,wanawaza kujijenga ili wapate fedha za kuhonga wasimamizi na wakuu wa Dola ili wapite Tena 2025.

Zao la katiba mbovu haliwezi kutofautiana sana zaidi ya kulaumiana wenyewe Kwa wenyewe.
Magufuli anasifiwa Kwa sababu wabunge wa hovyo walipenya Kwa nguvu ya Dola lake. Hao kamwe hawawezi kuona ubaya wa katiba iliyojaa viraka
 
Toka afe jina lake linatajwa Asubuhi mchana Hadi usiku.
Mnazidi kumkuza kutokana na chuki na anazidi kuwakaa kichwani .
#Alishaenda tuangalie walio Active
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…