Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Watz kwa unafiki bwana hiyo serikali yenyewe iliyo mpandisha huyo mwalimu mahakamani imeruhusu viboko shuleni.
Hata hivyo ataachiwa tu hiyo ni zuga tu kuwafumba watu macho na wana harakati uchwara.
 
Binafsi nimeangalia clip hiyo, sijaona kosa lolote. Tanzania kama tumeoitisha sheria ya kutoadhibu watoto shuleni waseme
Isitoshe hapo ni Madrasa ya kidini ambayo ruhusa kuchapa, na ukimwangalia hachapi kwa lengo la kudhuru

Nabii Suleiman anasema
Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

Mithali 22:15
Well said
 
Inasikitisha sana. Huko Marekani mitoto inaua wenzao kwa silaha za wazazi wao chanzo kikiwa ni ukosefu wa maadili na sheria za hovyo. Waafrika tunaacha maadili yetu mazuri na kufuata za magharibi zilizofeli.
Hili ni tatizo la utumwa wa kifikra. Hatuwezi kuwa na watoro wasioweza kuadhibiwa.
Copral punishment ni lazima. Na kuchapa sio kuua mtoto
Nabii Suleimani a.w anasema
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Mithali 23:13
 
Sijaona kosa la huyo mwalimu. Waliompeleka mahakamani ni maadui wa maadili kwa watoto. Ila Waalimu kwa sasa wangeachana tu na ishu za kuchapa watoto kwa sababu jamii imeshakubali watoto wasiwe na maadili. Kila mtu abebe msalaba wake.
30,000,000/= sio ndogo unajua
 
Hili ni tatizo la utumwa wa kifikra. Hatuwezi kuwa na watoro wasioweza kuadhibiwa.
Copral punishment ni lazima. Na kuchapa sio kuua mtoto
Nabii Suleimani a.w anasema
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Mithali 23:13
Nipe mwanao nimshushie mvua za bakora kama huyo jamaa hapo kwenye video, Tuone kama hatakufa.
 
Mwalimu wa Madrasa, Musa Bashiru Musa (24) ambaye kipande cha picha jongefu (video) kilisambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonyesha akiwapiga fimbo za mikononi wanafunzi wake, amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma zake.

Musa ambaye ni mkazi wa Mbagala Kiburugwa, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke na kusomewa mashtaka mawili ya kuwafanyia ukatili watoto wa madrasa, kinyume cha sheria.

Mwalimu huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Jumatano, Februari 19, 2025 na kusomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Rabia Ramadhani akisaidiana na Nicas Kihemba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Vick Mwaikambo.


View: https://x.com/Shariakill/status/1892137880845222128
 
Fimbo zimefutwa kwa sasa ni vile wengi hawajui ,mimi nishawahi kupigwa vimbo thelathini shuleni enzi hizo ,tena ilikuwa sio peke yangu ni karibia darasa zima kwa kosa la kuandikwa matusi.

Wanawake wanne walizimia walikuwa wana asili ya half cast ila hawa weusi walivumilia...Kwa sasa mambo ya kuchapana ni hatari sana hat sheria za kimataifa hazitaki.
Zimefutwa shuleni na sio madrasa
 
Safi kabisa.

Haya mavaa kobazi lazima yadhibitiwe.

Dunia ipo kwenye kuwafunza watoto teknolojia, Yenyewe yapo bize kukaririsha watoto kiarabu na hekaya za vitabuni.
Sio kweli ndo maana watoto wengi hawana maadili lazima waadhibiwe
 
Back
Top Bottom