Mwalimu wangu Master Herbalist Dr. Sebi akieleza namna ya ugonjwa wa UKIMWI unasababishwa na mucus au “ute”

Mwalimu wangu Master Herbalist Dr. Sebi akieleza namna ya ugonjwa wa UKIMWI unasababishwa na mucus au “ute”

VYAKULA ANAVYO KULA BINADAMU.jpg




Vyakula Kumi (10) Ambavyo Hupaswi Kuvila


Linapokuja suala la kula. Ulimi hupenda vitu vitamu vitamu.

Mzee tumbo wala hanaga shida. Husema ameshiba. Bila ya kujali umekula nini.

Shida iko katika moyo. Kukubali kuridhika kwa kile ulichojaaliwa kukipata. Ili mkono uende kinywani.

Kula vizuri ni suala zuri. Cha kujiuliza ni je, ninachokula ni chema kiafya? Kina madhara gani mwilini? Kinanifanya nijisikieje? Je nakunya vizuri?

Leo nita — share vyakula kumi. Ambavyo hupaswi kula. Hata ukishauriwa na Bwana Daktari. Navyo ni pamoja na:

Nafaka Zilizokobolewa
Tukianza na mchele uliokobolewa. Mchele huu haufai kiafya. Kwa sababu ukoboaji unafanya virutubishi kuondolewa. Pia nyuzi nyuzi huondolewa. Mchele huu mweupe unaweza kukufanya upate matatizo ya mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia ulaji wa mchele huu haukupi lishe yeyote zaidi ya kujaza tumbo. Badala yake unapaswa kula mchele wa kahawia. Mchele huu una madini mengi na vitamini kwa ajili ya afya yako.

Pia sembe haifai kwa afya yako. Kama mchele. Ukoboaji wa mahindi kupitiliza unayafanya yapoteze madini na vitamini. Pamoja na wanga. Ambavyo ni vitu muhimu kwa kuutia mwili nguvu na afya. Badala yake unga wa dona ndio unafaa kiafya. Kwa sababu mahindi yanasagwa yakiwa na ganda lake. Pia kiini hakiondolewi ambacho ndio ‘target’ ya panya mharibifu.

Bila kusahau ngano iliyokobolewa pia haifai. Waweza kusema mbona unga huu unaongezewa vitamini na madini kiwandani? Chakula bora hakipatikani kiwandani. Wala hakihitaji kuongezewa virutubishi.

Mkate Mweupe
Mkate huu ni zao la ngano iliyokobolewa. Hivo haufai kabisa kiafya kama tulivyoona kuwa, ngano iliyokobolewa imeondolewa virutubishi. Badala yake kula mkate wa kahawia. Unaotokana na ngano isiyokobolewa.

Juisi za Matunda
Ndiyo. Juisi za matunda. Hapa sizungumzii juisi zile za kiwandani. Ambazo zimewekwa ladha tu ya matunda lakini hazina uhalisia wowote. Nazungumzia juisi ile unayoitengeneza nyumbani. Inasemekana kuwa juisi hiyo ina sukari vijiko kumi sawa na chupa ya soda. Haifai kiafya. Unapotengeneza juisi kwa kusaga matunda una haribu nyuzi nyuzi zilizokatika matunda. Hivyo ikiwa una matatizo ya mmeng’enyo wa chakula. Ni afadhali ule matunda kama yalivyo. Badala ya kunywa juisi yake.

Soda
Kama nilivyoeleza hapo juu. Soda ina vijiko kumi vya sukari. Sukari inapozidi mwilini, kongosho inashindwa kupambana na sukari hii. Hivyo kusababisha ugonjwa wa kisukari.

Rangi inayoongezwa kenye soda inaaminika kusababisha saratani ya mapafu na ini.

Vile vile soda kwa watoto wandogo huongeza hatari ya kunenepa kupindukia.

Pia soda inakufanya uishiwe maji mwilini.

Badala yake kunywa maji mengi. Ikiwa hupendi ladha ya maji. Yachanganye na vipande vya limao kwa manufaa zaidi.

Chipsi
Chakula cha fasta au siyo. Chakula pendwa cha akina dada. Lakini hata wanaume! Wengi wetu tunakula chipsi. Hii ni kutokana na uvivu wa kupika au sababu zingine.

Hupaswi kula chipsi kwa sababu zina mafuta mengi. Vyakula vilivokaangizwa vina mchango mkubwa katika kusababisha kutopata choo. Au kupata choo kama cha mbuzi.

Tambi
Tambi zinatengenezwa kwa ngano iliyokobolewa. Kwa hiyo haina virutubisho vyovyote. Licha ya kuongezewa viungo kama vitamini, mafuta na madini. Hivi vyote ni takataka ambazo hazifai kuingia mwilini.

Mafuta ya Kupikia ya Kiwandani
Imekuwa kibiashara sana siku hizi. Baada ya kuona kuwa watu wanapata ufahamu zaidi kuhusu vyakula. Utaona kibandiko ‘Hayana Lehemu’. Au ‘Mafuta Asili’. Mamlaka za chakula na dawa huweza kutoa ruhusa ya wazalishaji kuweka vibandiko hivyo ikiwa tu wamekidhi viwango fulani. Hii haimaanishi kuwa ni kweli mafuta hayo ya kupikia hayana lehemu. Badala yake kula mafuta ya alizeti, karanga n.k. Yaliyochujwa kwa mashine za mtaani. Na kuuzwa yakiwa ‘pure’ bila kuchanganywa na kitu kingine chochote.

Maandazi
Unapopika chakula kwa joto jingi kupita kiasi. Chakula hicho kinapoteza virutubishi na kugeuka ‘garbage’ ama ‘junk’. Maandazi huivia mafuta yenye joto kali sana. Pia kwa kuwa yanaivia mafuta, hii ina maana kwamba maandazi yana mafuta mengi. Ambayo huweza kusababisha matatizo ya mmeng’enyo wa chakula pamoja na unene. Pia hayana virutubisho vya asili kwa kuwa yanatengenezwa kwa ngano iliyokobolewa. Ingawa kuna maandazi ya ngano isiyokobolewa, lakini kitendo cha kuyapika kwa mafuta yenye joto kupita kiasi. Kunayafanya nayo pia yakose lishe bora kiafya.

Chumvi Ya Mezani
Utaambiwa imeongezwa madini ya joto. Lakini chumvi hii ya mezani katika uasili wake siyo nyeupe kama unavyoiona. Inachimbwa na ku bleach iwa ili iwe nyeupe. Kupikwa kwa joto la hali ya juu sana. Kunaifanya isifae kiafya. Madini ya iodineyanayopatikana katika chumvi asili hayatoshi kuzuia ugonjwa wa rovu. Ndio maana huongezewa potassium-iodide’ ili kukukinga na ugonjwa huo. Ikumbukwe kwamba madini yanayoongezwa kwenye chumvi asili sio asili. Bali yametengenezwa kiwandani na hivyo moja kwa moja. Haya hayafai kuingia mwilini mwako. Badala yake tumia chumvi asili ya mawe. Na kula vyakula vyenye madini ya ‘iodine’ kwa wingi. Kama vile maziwa na mayai.

Pombe
Matumizi yaliyokithiri ya pombe yanaweza kusababisha matatizo ya ini, ugonjwa wa moyo.Na saratani. Pia pombe huweza kusababisha unene aka ‘beer belly’ kwa mtumiaji aliyekithiri. Matatizo ya pombe ni mengi, mengi sana. Ulevi kupindukia ni tishio kwa uchumi wa mtumiaji.

Hivyo ni baadhi tu ya vyakula ambavyo hupaswi kuvila. Kutokana na madhara yanayoletwa na vyakula hivyo kiafya. Ni vema binafsi kila mtu akajihoji anajisikiaje baada ya kutumia chakula fulani. Huenda chakula fulani kikawa kibaya kwa mtu huyu. Lakini kikawa bora kwa mtu mwingine. Pia ni vema kila mtu akawa muwazi kwa tafiti mbali mbali zinazokuwa zimefanywa na wataalamu wa afya.
 
Nimesikia dr sebi ana ongelea kuhusu fonio kwa kiswahil zinaitwaje
Fonio ni neno kwa nyasi mbili zilizopandwa katika jenasi ya Digitaria ambayo ni mazao mashuhuri katika sehemu za Afrika Magharibi. [1] Ni mtama wenye nafaka ndogo. [1]

Fonio ni chakula chenye lishe na ladha nzuri. [1] [2] Inatumiwa haswa katika nchi za Afrika Magharibi, ambapo pia inalimwa. [1] [2] Soko la fonio la kimataifa lilikuwa tani 673,000 mnamo 2016. [3] Jina fonio (lililokopwa na Kiingereza kutoka Kifaransa) limetoka kwa Wolof foño. [4]

Mnamo Desemba 2018, Tume ya Ulaya iliidhinisha biashara ya fonio kama chakula cha riwaya katika Jumuiya ya Ulaya, baada ya kuwasilishwa na kampuni ya Italia Obà Food kutengeneza na kuuza bidhaa mpya za chakula.

Hizo hapo chini nafaka za Foniao.
 

Attachments

  • WALI WA FONIO.jpg
    WALI WA FONIO.jpg
    160.5 KB · Views: 42
  • FONIO.png
    FONIO.png
    89.9 KB · Views: 42
  • FONIO GRAIN.png
    FONIO GRAIN.png
    139 KB · Views: 45

DR SEBI ON BLOOD CLOT DR SEBI AZUNGUMZIA TIBA YA KUGANDA DAMU KATIKA MISHIPA YA DAMU .DAWA YAKE NI LILY -OF- THE- VALLEY​

A blood clot is a clump of blood that has changed from a liquid to a gel-like or semisolid state. Clotting is a necessary process that can prevent you from losing too much blood in certain instances, such as when you’re injured or cut.


HOW TO GROW LILY-OF-THE-VALLEY.jpg





 
Dr. Mimi mpaka leo sielewi mambo ya hospital na uwa nauliza kwa nini HIV haipimwi kwa microscope ili tuone mwonekano wa kirusi?

Pia Dr. nina shida ya kupata choo kama cha mbuzi na inaweza kunichukua siku 3 mpaka 4 kupata choo hivi hapa tatizo ni nini?
 
Dr. Mimi mpaka leo sielewi mambo ya hospital na uwa nauliza kwa nini HIV haipimwi kwa microscope ili tuone mwonekano wa kirusi?

Pia Dr. nina shida ya kupata choo kama cha mbuzi na inaweza kunichukua siku 3 mpaka 4 kupata choo hivi hapa tatizo ni nini?
Mkuu,

Usipate tabu sana ni dalili kuwa wewe unageuka mbuzi! Usijali,wala usiogope!

Hapo sehemu uliyopo kama unaweza kupata papai na ndizi mbivu(kama si mgonjwa wa kisukari) basi tumia vitu hivyo kabla ya kula chakula chengine chochote unapoamka. Lakini kwanza anza na maji moto, kunywa vikombe viwili vya maji moto, yasikuunguze lakini. baada ya dakika 10 kula ndizi mbivu moja,ile iliyovurugika kidogo sio ile ngumu, na papai. Papai bivu, kama utapata avocado (parachichi) ongezea, halafu nenda jogging kidogo kama 30mins utoke jasho, kama utakwenda mbali ukumbuke kuchukua mfuko wa plastiki akiba!
Natumai tatizo lako litatatuka,mkuu! Anza kesho. Hakuna kirusi cha HIV ndio maana hawapimi kw aMikroscope waongo wazungı.
 
Mkuu,

Usipate tabu sana ni dalili kuwa wewe unageuka mbuzi! Usijali,wala usiogope!

Hapo sehemu uliyopo kama unaweza kupata papai na ndizi mbivu(kama si mgonjwa wa kisukari) basi tumia vitu hivyo kabla ya kula chakula chengine chochote unapoamka. Lakini kwanza anza na maji moto, kunywa vikombe viwili vya maji moto, yasikuunguze lakini. baada ya dakika 10 kula ndizi mbivu moja,ile iliyovurugika kidogo sio ile ngumu, na papai. Papai bivu, kama utapata avocado (parachichi) ongezea, halafu nenda jogging kidogo kama 30mins utoke jasho, kama utakwenda mbali ukumbuke kuchukua mfuko wa plastiki akiba!
Natumai tatizo lako litatatuka,mkuu! Anza kesho. Hakuna kirusi cha HIV ndio maana hawapimi kw aMikroscope waongo wazungı.
Ahsante doctor.
 
Dr. samahani sasa kinachopimwa mpaka mtu anagundulika ana virus wa HIV ni nini na kuambiwa mgonjwa ni nini
Naomba ufafanuzi wako Dr.
 
Dr. samahani sasa kinachopimwa mpaka mtu anagundulika ana virus wa HIV ni nini na kuambiwa mgonjwa ni nini
Naomba ufafanuzi wako Dr.

Kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na jinsi mtu anavyoweza kuambukizwa HIV​


Disemba mosi ni siku ya kimataifa ya UKIMWI Duniani


Maelezo ya picha,
Disemba mosi ni siku ya kimataifa ya UKIMWI Duniani

Suala la maambukizi ya virusi vya HIV vinavyosababisa ugonjwa wa Ukimwi bado linaendelea kuwakosesha usingizi wataalamu wa afya kote duniani.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) ugonjwa huo umewaangamiza zaidi ya watu milioni 35 kufikia sasa.
Mwaka jana pekee, karibu watu milioni moja walifariki kutokana na magonjwa yanayohusishwa na virusi vya HIV.

Kuna karibu watu milioni 37 ambao wanaishi na virusi hivyo - 70% kati yao wanapatikana barani Afrika - huku watu milioni 1.8 wakiambukizwa umpya mwaka 2017.
Tangu ugonjwa wa Ukimwi ulipogunduliwa miaka ya 1980, kumekuwa na gumzo kuhusiana na jinsi virusi vyake vinavyoweza kusambazwa.
Je maisha ya waathiriwa wa ugonjwa huo katika jamii yamekuaje?
Leo Ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi Duniani, tunaangazia baadhi ya dhana potofu zinazosababisha kunyanyapaliwa kwa waathiriwa.
Dhana: Naweza kuambukizwa virusi vya HIV kwa kutangamana na watu waliyoathirika
Uchunguzi wa damu ni muhimu ili kubaini kama una virusi vya HIV

Maelezo ya picha,
Uchunguzi wa damu ni muhimu ili kubaini kama una virusi vya HIV
Dhana hizi zimesababisha unyanyapaa dhidi ya waathiriwa wa ugonjwa wa UKIMWI kwa muda mrefu.
Licha ya kuendeshwa kwa kampeini ya mwaka 2016 ya kuhamasisha watu nchini Uingereza kuhusiana na suala hilo 20% ya watu nchini humo wanaamini HIV inaweza kusambazwa kupitia mate au kumgusa mtu aliyeambukizwa virusi hivyo.
Huwezi kuambukizwa virusi vya HIV kupitia:
  • Kwa kuvuta hewa moja
  • Kukumbatiana, kubusiana, au kusalimiana
  • Kutumia pamoja vyombo vya kula chakula
  • Kutumia maji pamoja
  • Kutumia pamoja vitu vya kibinasi
  • Kutumia pamoja vifaa vya mazoezi
  • Kugusa kiti cha msalani, komeo la mlango na kadhalika
Mwaka 1991, Princess Diana wa Wales alikutana na waathiriwa wa Ukimwi mjini London katika juhudi za kukabiliana na dhana kuhusu njia za maambukizi ya virusi vya HIV

Maelezo ya picha,
Mwaka 1991, Princess Diana wa Wales alikutana na waathiriwa wa Ukimwi mjini London katika juhudi za kukabiliana na dhana kuhusu njia za maambukizi ya virusi vya HIV
Virusi vya HIV huambukizwa kupitia damu, kunyonyesha au kufanya ngono bila kinga na mtu aliye na virusi hivyo.
Dhana: Dawa za kienyeji zinaweza kuzuia maambukizi ya HIV
Huu si ukweli hata kidogo . Dawa za kienyeji, kuoga baada ya kufanya tendo la ndoa au kufanya ngono ya mdomo haina athari yoyote dhidi ya HIV.
Utamaduni wa utakaso ambao ulipata umaarufu katika mataifa ya jangwa la sahara , na maeneo ya India na Thailand, umetajwa kuwa hatari sana.

Umesababisha wasichana kubakwa na watoto wadogo kunajisiwa hali ambayo inawaeka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV.
Chimbuko la utamaduni huo linaaminiwa kuwa barani Ulaya katika karne ya 16 ambapo watu walianza kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende.
Utamaduni huo hata vyo haukuwahi kutibu magonjwa hayo pia.
HIV haiambukizwi kwa kumgusa mtu aliyeathiriwa au kwa kuumwa na mbu

Maelezo ya picha,
HIV haiambukizwi kwa kumgusa mtu aliyeathiriwa au kwa kuumwa na mbu

Dhana: Mbu wanaweza kusambaza virusi vya HIV
Japo maambukizi hupitia damu, tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mtu hawezi kupata maambukizi kutoka kwa wadudu wanaofyonza damu kwa sababu hizi mbili.
1) Mbu hamuongezei mtu damu mwilini kabla ya kumuuma mtu.
2) Virusi vya HIV huishi ndani yao kwa kwa muda mchache.
Kwa hivyo hata mtu akiishi katika eneo lililo na mbu wengi, maambukizi ya HIV hayahusiani kwa vyovyote na mbu hao.
Dhana: Siwezi kupata virusi vya HIVkwa kufanya ngono ya mdomo
Ni kweli ngono ya mdomo huenda si hatari sana ikilinganishwa na aina nyingine ya ngono.
Viwango vya maambukizi ni chini ya nne katika visa 10,000.
Mpira wa kondomu uliyovalishwa kwa ndizi

Maelezo ya picha,
Mipira ya kondomu husaidia kumkinga mtu dhidi ya virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa
Lakini mtu anaweza kupata maambukizi ya virusi vya kufanya ngono ya mdomo na mwanamume au mwanamke aliye na virusi hivyo.
Ndio maana madaktari wanapendekeza matumizi ya mpiria wa kondomu wakati wa kufanya gono ya mdomo.

Dhana: siwezi kuambukizwa virusi vya HIV nikivaa mpira wa kondomu
Mipira ya Kondomu inaweza kupasuka, kutoka au kuvuja wakati wa tendo la ndoa hali ambayo huenda ikawaeka katika hatari ya maambukizi ya virusi wapenzi wote wawili
Hii ndio maana kufanikiwa kwa kampeini dhidi ya UKIMWI hakukomei katika muktadha wa kuwaambia watu kutumia kinga pekee, bali bia kuna haja ya wale waliyeambukizwa virusi vya HIV kupata matibabu.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani WHO, mmoja kati ya kila watu wanne ana virusi vya HIV na mtu huyo hana habari - hii inamaanisha watu milioni 9.4 - wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Dhana: Kama huna dalili huna virusi vya
Mtu anaweza kuwa na virusi vya ukimwi na asiwe na habari.
Hata hivyo huenda akapatikana na magonjwa kama vile homa inayofanana na influenza-ikiwa ni pamoja na kuumwa na kichwa,kushikwa na homa, harara mwilini au kuumwa na koo katika wiki chache za kwanza baada ya kuambukizwa viini vinavyosababisha ugonjwa wa UKIMWI.
Muuguzi akimhudumia mgonjwa

Maelezo ya picha,
Mmoja kati ya kila watu wanne ana virusi vya HIV na mtu huyo hana habari
Dalili zingine kama vile kupungua uzani, kuharisha na kukohoa hujitokeza kadiri kinga ya mwili inavyoendelea kupungua.
Muathiriwa asipopata matibabu huenda akapatikana na magonjwa kama vile kifua kikuu, homa ya utandu wa ubongo miongoni mwa zingine

Dhana: Mtu aliyepatikana na virusi vya HIV atafariki akiwa na umri mdogo
Watu wanaojua hali yao ya HIV na kuzingatia matibabu na lishe bora huishi kwa muda mrefu.
Shirika la UNAids linasema 47% ya watu wote wanaoishi na virusi vya HIV huwa wamedhibiti kiwango cha virusi hivyo mwilini kwa kutumia dawa.
Hii inamaanisha watu hao hawawezi kusambaza virusi hivyo hata wakijamiana na mtu ambaye hana virusi hivyo.
mama na mtoto

Hata hivyo wakisitisha matibabu viwango vya virusi vinaongezeka na vinaweza kuonekana katika damu yake.
Kwa mujibu wa WHO, watu milioni 21.7 waliyo na virusi vya HIV wamekuwa wakitumia dawa za kukabiliana na virusi hivyo mwaka 2017.
Idadi hiyo imeongezeka kutoka watu milioni 8 mwaka 2010 - hii inamaanisha 78% ya watu waliyo na virusi vya HIV wanajua hali yao.

Dhana: Kunamama waliyoathirika watawaambukiza watoto wao
Suala hilo lina mjadala lakini uwezekano wa akina mama ambao wamedhibiti kabisa kiwango cha virusi vya HIV katika miili yao wanaweza kuwanyonyesha watoto wao bila kuwaambukiza virusi hivyo. chanzo. Kwanini huwezi kuambukizwa Ukimwi kupitia mate? - BBC News Swahili
 

Uhariri wa Vinasaba: Wachina 'wameunda' binadamu asiyeweza kuambukizwa Ukimwi?​


embryo


Mwanasayansi kutoka Uchina ambaye amedai kuwa amesaidia kuzalisha watoto wa kwanza ambao chembe zao za jeni zilihaririwa kabla ya kuzaliwa na kwamba hawawezi kuambukizwa Ukimwi, ameshutumiwa vikali na madai yake kutiliwa shaka.
Prof He Jiankui anadai kwamba wasichana hao pacha, waliozaliwa wiki chache zilizopita, vinasaba vyao (DNA) vilifanyiwa ukarabati wakiwa bado ni vinitete kuwawezesha kutoambukizwa Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU).
Madai yao aliyoyatoa kwenye kanda ya video iliyosambazwa na shirika la habari la Associated Press hayajapigwa darubini na yamewaghadhabisha wanasayansi wengine.
Wamesema wazo hilo lenyewe ni la kuogofya.
Kazi kama hizo za kisayansi, za kuhariri jeni za binadamu, zimepigwa marufuku katika mataifa mengi.

Vizazi vijavyo​

Wanasayansi wanaamini kwamba uhariri wa jeni unaweza kuwaepushia watu magonjwa ya urithi yanayotokana na vinasaba, kwa kufuta chembe za jeni zinazosababisha magonjwa hayo au hata kuzifanyia ukarabati mtoto akiwa bado ni kiinitete.

Lakini wataalamu wana wasiwasi kwamba kuhaririwa huko kwa jeni kunaweza kusababisha madhara makubwa sio tu kwa mtoto mwenyewe bali pia vizazi vya baadaye ambavyo vitayarithi marekebisho yaliyofanywa na wanasayansi kwenye vinasaba.
Katika mataifa mengi, ikiwemo Uingereza, kuna sheria zinazoharamisha kuhaririwa kwa jeni hata katika mchakato wa kuwasaidia binadamu kutungisha mimba.
Foetal ultrasound scan

Wanasayansi wanaweza kufanya utafiti kuhusu uhariri wa jeni kwa kutumia viinitete vilivyotupwa baada ya mwanamke kutungishwa mimba kwenye maabara, shughuli inayofahamika kama IVF, lakini hilo huruhusiwa tu kwa sharti kwamba viinitete hivyo vitaharibiwa baada ya utafiti na visitumiwe kuzalisha mtoto.
'Watoto wa maabara'
Lakini Prof He, aliyesomea Stanford nchini Marekani na anayefanyia kazi yake katika maabara moja katika jiji la Shenzhen kusini mwa China anasema alitumia vifaa vya kuhariri jeni 'kuwaunda' watoto hao wawili pacha waliopewa majina "Lulu" na "Nana".
Kwenye video, amedai kwamba alifanikiwa kuondoa jeni kwa jina CCR5 kwenye viinitete vya na kuwawezesha watoto hao kuwa na kinga ya kudumu dhidi ya Ukimwi hata wakikumbana na virusi hivyo.
Anasema kazi yake imeangazia kuwaunda watoto ambao hawaugui maradhi mbalimbali na si kuwaunda watoto wa maabara wa kupendeza, wenye macho ya kuvutia au wenye kiwango cha juu cha werevu.
"Ninaelewa kwamba kazi yangu itazua utata - lakini ninaamini kwamba familia zinaihitaji teknolojia hii na niko tayari kushutumiwa mradi tu niwe nawasaidia," anasema kwenye video hiyo.
'Kuweza kutibiwa'
Hata hivyo, mashirika kadha, ikiwemo hospitali iliyohusishwa na madai hayo imekana kuhusika.
Chuo Kikuu cha Kusini cha Sayansi na Teknolojia mjini Shenzhen kimesema hakikuwa na ufahamu kuhusu mradi huo wa profesa huyo na sasa kitaanzisha uchunguzi.
Image of the human body

Na wanasayansi wengine wanasema iwapo taarifa hizo ni za kweli, basi Prof He atakuwa amevuka mipaka, kwa kufanyia majaribio viinitete vyenye afya katika utafiti wake bila idhini wala msingi.
Prof Robert Winston, mtaalamu wa masuala ya uzazi, amesema: "Hii ni ripoti ya uongo, ni utovu wa maadili katika sayansi na ni kukosa uwajibikaji."
"Kama ni kweli, bado itakuwa ni utovu wa maadili kisayansi."

Dkt Dusko Ilic, mtaalamu katika seli za viinitete katika chuo kikuu cha King's College London, amesema: "Ikiwa hili linaweza kukubalika kimaadili, basi mtazamo wao wa maadili ni tofati sana na maeneo mengine ya dunia."
Anasema kwamba siku hizi Ukimwi ni ugonjwa unaoweza kutibiwa na kudhibitiwa na iwapo ni ugonjwa unaoweza kudhibitiwa kwa dawa, basi hakuna hatari yoyote ya mzazi kumrithisha mtoto.

Hatari zilizopo​

Prof Julian Savulescu, mtaalamu wa maadili katika Chuo Kikuu cha Oxford amesema: "Kama ni kweli, basi majaribio hayo yanaogofya. Viinitete hivyo vilikuwa na afya - havikuwa na magonjwa yoyote."
Human embryo development

CHANZO CHA PICHA,KATHY NIAKAN
Maelezo ya picha,
The embryo divides and develops from a single fertilised egg (top left) to a blastocyst (bottom right)
"Uhariri wa jeni wenyewe bado ni jambo linalofanyiwa majaribio na unahusishwa na matokeo mengine ambayo wakati mwingine huwa hayajatarajiwa, ya kubadilika kwa maumbile. Unaweza kusababisha matatizo ya kinasaba mapema au baadaye katika maisha ya mtoto, au hata kusababisha saratani."
"Majaribio haya yanawaweka watoto waliokuwa katika afya nzuri kwenye hatari za uhariri wa jeni bila kuwa na manufaa yoyote kwao."
Wanasyaansi wanasema uhariri wa jeni unaweza kukubalika siku za baadaye, lakini sheria zaidi na umakinifu unahitajika kabla ya kuruhusiwa.
chanzo. Wachina 'wameunda' binadamu asiyeweza kuambukizwa Ukimwi? - BBC News Swahili
 
Mmmh...
Ila kuna uzi hapa jukwaani unaelezea ni namna gani mlonge unaweza kutibu maradhi mbalimbali,mmoja wa wachangiaji katika huo uzi ni wewe mwenyewe, mbona umebadili mawazo yako ghafla..?
Au kipindi hicho ulikua bado haujamsoma Dr Sebi..?
Hili swali ni zuri
 
Dr Sebi:
Mucus is the cause of all disease.
This was the question posed to me in court, that why were we making these claims and why were we so successful and what was going on is that disease was never identified to us. If it was identified the question would not be asked now and then we all, all of us that are sick would be enjoying health.

Well, disease is the accumulation of mucus, breaking down the mucus membrane and that mucus covering groups of cells in your body, like for instance we have the mucus membrane in the body to protect us from the onslaught of bacteria as they are called, as they are called but this mucus membrane is for protection but now we eat acid foods and the acid foods break down the mucus membrane and thus cause it to flow with the blood covering other groups of cells now, cells that belongs to organs, depriving them of oxygen.

If the mucus goes to your nostrils they call it sinusitis, if the mucus goes to your bronchial tubes is bronchitis, if the mucus goes to the lungs is pneumonia.

They didn’t make any claims, they didn’t do anything, so naturally if one out of a flock of people that has not shown anything or stood up for their right if they had accomplished something. Well he was just part of the pack, and I wasn’t in disagreement with the attorney general because he did his job but it was his mistake by assuming that I was a part of the pack. I am not part of any pack, never has been, never could be.





Download
720
Dk Sebi:
Kamasi ni sababu ya magonjwa yote.
Hili ndilo swali nililoulizwa mahakamani, kwamba kwa nini tunatoa madai haya na kwa nini tulifanikiwa sana na kinachoendelea ni kwamba ugonjwa huo haukutambuliwa kwetu. Ikiwa ingetambuliwa swali lisingeulizwa sasa na basi sisi sote, sisi wote ambao ni wagonjwa tungekuwa tunafurahia afya.

Kweli, ugonjwa ni mkusanyiko wa kamasi, kuvunja utando wa kamasi na ute unaofunika vikundi vya seli katika mwili wako, kama kwa mfano tuna utando wa kamasi mwilini ili kutulinda dhidi ya shambulio la bakteria kama wanavyoitwa, wanaitwa lakini utando huu wa kamasi ni kwa ajili ya ulinzi lakini sasa tunakula vyakula vya asidi na vyakula vya asidi huvunja utando wa kamasi na hivyo kusababisha mtiririko wa damu unaofunika makundi mengine ya seli sasa, seli ambazo ni za viungo, na kuwanyima. oksijeni.

Kamasi ikienda kwenye pua yako wanaiita sinusitis, kamasi ikienda kwenye mirija ya bronchial ni bronchitis, kamasi ikienda kwenye mapafu ni nimonia.

Hawakutoa madai yoyote, hawakufanya chochote, hivyo kwa kawaida ikiwa mmoja kati ya kundi la watu ambao hawajaonyesha chochote au walisimama kwa haki yao ikiwa walikuwa wamekamilisha jambo fulani. Kweli, alikuwa sehemu tu ya pakiti, na sikuwa na maelewano na mwanasheria mkuu kwa sababu alifanya kazi yake lakini lilikuwa kosa lake kwa kudhani kuwa mimi ni sehemu ya pakiti. Mimi si sehemu ya pakiti yoyote, haijawahi kuwa, haiwezi kuwa.
 
One of the greatest contributions and losses of the last 3 generations was Dr Sebi. You can recognize who truly loved him by what they say and do. By who supported him, quoted him, visited him and got along with him.
_
To this day much of his message and knowledge is still being uncovered and understood. This is due to our reluctance to truly embrace nature the way he did.
He will forever be missed and we vow to carry on his message and the healing modality he built up, fought for and won for us all. The AfricanBioMineralBalance
RIP GOOD BROTHER
❤
🌱
🌿
🍃
👇
🤲
😭


Mmoja wa michango na hasara kubwa zaidi ya vizazi 3 vilivyopita alikuwa Dk Sebi. Unaweza kutambua ni nani aliyempenda kikweli kwa yale wanayosema na kufanya. Ni nani aliyemuunga mkono, akamnukuu, akamtembelea na kupatana naye.
_
Hadi leo hii sehemu kubwa ya ujumbe na ujuzi wake bado unafichuliwa na kueleweka. Hii ni kutokana na kusita kwetu kukumbatia asili jinsi alivyofanya.

Atakumbukwa milele na tunaapa kuendeleza ujumbe wake na njia ya uponyaji aliyoijenga, kupigania na kushinda kwa ajili yetu sote. Kaa Pepopni kwa amani Mwalimu wangu Doctor Sebi.
 

Attachments

  • DR.SEBI.jpg
    DR.SEBI.jpg
    40.9 KB · Views: 39
Back
Top Bottom