Mwamba alivyojimaliza mwenyewe baada ya kugundua kuwa watoto aliezaa na mkewe sio wa kwake

Aloo dunia ina mengi!

Mwamba alianza kwa kunyanyua vyuma, mwili ukawa jumba na mtaani akawa anatisha. Vijana wakamuogopa na vichuchu vikampenda. Kazi alikuwa nayo nzuri tu, hivyo kila mchuchu alieingia chumbani kwake alihitaji aishi nae.

Anyway jamaa kwa vile umri umesogea, ikabidi ateue mchuchu mmoja kati ya wengi aliolala nao akaowa. Harusi ilifana mambo yakaenda vyema, na baada ya miezi kadhaa mchuchu ukadaka kiumbe. Imeenda hadi miezi 9 akajifungua babe boy. Mwamba akaongeza mapenzi kwa binti hasa baada ya kuona mkewe kamzalia kidume cha kusimamia mali zake na familia yake hapo baadae.

Mungu akajaalia jamaa akalenga tena binti akadaka kiumbe na baada ya miezi 9 akatoka babe girl. Furaha ya mwamba ikawa ni zaidi ya hii ninayoisimulia hapa.

Watoto walikuwa wazuri wa rangi na sura. Walionekana zaidi kufanana na mama kwa 80% , maana mama alikuwa mzuri kisha mweupe pee.

Wakapanga wazae kizungu, hivyo hawakutaka kuongeza mtoto wa tatu wala wa nne. Watoto wakalelewa kisasa kwa kutumia maziwa ya kopo ili yale ya mama yabaki kutumiwa na baba (watu wazima wanaelewa)

Baada ya miaka kadhaa yule boy akiwa darasa la tatu katika shule moja ya bei na yenye hadhi ya watoto wa wakubwa na wa kishua, na girl akiwa darasa la kwanza.

Mapenzi yakiwa motomoto huku mwamba akiwa ashamjengea mkewe jumba la kifahari (kwa sasa linaishi wazazi wa mkewe) kama asante ya kumzalia watoto wale aliowapenda kwa moyo wake wote. Ghafla babe boy akaanza kuumwa, kwa vile pesa ipo basi mtoto akapelekwa katika hospital bora kupata matibabu. Bila kutarajia wakaona hali inazidi kuwa mbaya, mtoto hali, hanywi mwili ukaanza kuishiwa nguvu na maji mwilini.
Mwamba akamhamisha his son kwa hospital nyingine yenye ubora zaidi. Hali ikaendelea na mtoto akaanza kupungukiwa damu. Hivyo ikashauriwa inabidi mtoto aongezewe damu kisha ndio aendelee na matibabu. Baba akasema yupo tayari kutoa damu kwa ajili ya kidume chake hicho kimoja cha mbegu.

Ikahitajika vipimo mbali mbali vya damu ili kuona kama magroup yao ya damu yanaendana, na pia baba Hana magonjwa nk (wale waliowahi kuchangia damu hospital wananielewa zaidi).

Baada ya vipimo vya kina ikaonekana kuwa group la baba sio lake hivyo anahitajika baba mzazi original ndo aje atoe damu. Mwamba akashtuka na kuwambia madaktari kuwa yeye ndio baba halali wa mtoto huyo na kwamba mtoto hana baba mungine yeyote zaidi yake yeye. Madaktari wakaendelea kusisitiza kwamba vipimo vinaonesha kuwa yeye na huyo mtoto hawana uhusiano wowote, hivyo damu yake pia haiwezi kuwa na msaada wowote kwa mtoto.

Mwamba na mkewe wakapandwa ghadhabu na kuamua kumhamisha mtoto wao katika hospital nyingine. Pia kule wakakuta tatizo la ukosefu wa damu ni kubwa hivyo inabidi tu aongezewe damu. Baba akasema atamtolea damu mwanae. Baada ya vipimo na huku nako wakakuta hola. Yani hakuna uhusiano wowote kati ya mwamba na mtoto. Hapo jamaa akaanza kuona ukweli wa zile taarifa za damu kwa hospital zote mbili. Alichofanya akakurupuka bila kumwambia mkewe kuwa anakwenda wapi. Hadi nyumbani na kukachukua kale kabinti kake walikokuwa wamekaacha na dada wa kazi hadi katika hospital nyingine kupima damu. Vipimo pia vikaonesha kuwa na huyu hawaendani kwa lolote wala chochote.

Mwamba akawasha gari hadi hospital na kumwambia mkewe ambae alikuwa ashakubali kuchangia dam kwamba waende nyumban mara moja. Mke akiwa na hofu wakaenda hivyo hivyo hadi home. Na jamaa kumtaka mkewe amweleze ukweli kuhusu watoto.

Mke alijaribu kuficha ficha ila baada ya jamaa kumtolea bunduki na kumwambia kwamba kama haongei ukweli atampasua kichwa, ikabidi amwambie ukweli kuwa kuna dogo fulan ambae walikuwa nae kwenye uhusiano toka udogoni mwake yani enzi za kimama mama, shule wakajikuta wameandikishwa darasa moja maana walikuwa majirani ila kijana alikuwa anamshinda binti mwaka mmoja tu.

Hivyo pamoja na kwamba aliolewa lkn bado alishindwa kuishi bila kupata penzi la yule kijana. Cha kushangaza kijana alikuwa anatwanga kitambo, ila watoto wameingia pindi tu baada ya binti kuolewa na huyo mumewe.

Mwamba baada ya kupata hizo taarifa hakutaka kumdhuru yule binti, alichofanya akajifanya amemsamehe na kumuomba kuwahi hospital kumtolea mtoto damu.

Ile binti anatoka, jamaa akaamua kujipiga risasi tano kichwani. Mke alipofika alikuta mfanyakazi analia, ile kuingia ndani anakuta maiti ya mumewe ikiwa sakafuni.

Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi.
Risasi tano kichwani😂😂😂 atakua alipigwa
 
Kaka risasi kichwani kwa kujipiga hivi unaifahamu risasi lakini? Kama alipigwa upo sawa
 
hadith yako nzuri na inafundisha.ila hapo kwenye kujipiga risasi tano za kichwa tuache kidogo.RISASI YA KICHWA UWA MOJA TU.UKIONGEZA YA PILI WEWE MWANAUME
 
Hii chai kabisa lakin nowdays trending ni watoto kuwa na mababa wawili had watatu na wote wanahudumia mtoto mmoja
 
Acha story
 
Mijitu inakurupuka hata kupima uongo na ukweli haijui
Risasi 5
Mimba ziliingia baada ya yy kuolewa [emoji28]
 
Ya kutunga!
Kuna kipengele umekikosea...Kwamba mgonjwa(mtoto) anaongezewa dam aliyochangia babake?? [emoji1]..hii hua inatokea kwenye emergency life saving situation tu na WHO iko against hii kitu. Kawaida Dam inayochangiwa na ndugu wa mgonjwa ama wazazi sio dam anayowekewa mgonjwa coz kuna vipimo vingi lazma vifanyike kujiridhisha kua dam n salama.
NB; mtoto sio lazma afanane group la dam na babaake. Kuna vipimo maalum vya kuangalia Vinasaba.
Naomba kuwasilisha.
 
Ila kwenye group la damu la mtoto sio lazima lifanane na baba au mama, genetics ya form four hiyo.
 
That's why baba kujua DNA ya watoto lazima iwe haki yake coz wanawake wana privilege ya kujua kila wanayemzaa mwanaye; wanaume hawajui. Hizi sheria za kubana kupata DNA za kipuuzi na haiwahusu serikali; wanaume ni haki yao kujua.
 
Ahsante kwa chai.

Kwanza, si lazima kundi la damu la mtoto lifanane na kundi la damu la mzazi. Labda endapo tu wazazi walikuwa na kundi moja la damu. Mtoto anaweza kuwa na kundi la tofauti kabisa na makundi ya wazazi wake wote.

Pili, kwenye uchangiaji wa damu si lazima anyetoa damu awe sawa na kundi la damu la anayepokea. Unaweza ukatoa, kisha mgonjwa akawekewa damu yake pasipokusubiri mlolongo mrefu wa kupima. Itatumika tu kama fidia.

Tatu, huwezi kujipiga risasi tano kichwani. Risasi moja tu ya kisawasawa, huwezi tena hata kushikilia bunduki.

Tunashukuru kwa story yako.
Mpuuzi sana huyu mleta mada
 
Aloo dunia ina mengi!

Mwamba alianza kwa kunyanyua vyuma, mwili ukawa jumba na mtaani akawa anatisha. Vijana wakamuogopa na vichuchu vikampenda. Kazi alikuwa nayo nzuri tu, hivyo kila mchuchu alieingia chumbani kwake alihitaji aishi nae.

Anyway jamaa kwa vile umri umesogea, ikabidi ateue mchuchu mmoja kati ya wengi aliolala nao akaowa. Harusi ilifana mambo yakaenda vyema, na baada ya miezi kadhaa mchuchu ukadaka kiumbe. Imeenda hadi miezi 9 akajifungua babe boy. Mwamba akaongeza mapenzi kwa binti hasa baada ya kuona mkewe kamzalia kidume cha kusimamia mali zake na familia yake hapo baadae.

Mungu akajaalia jamaa akalenga tena binti akadaka kiumbe na baada ya miezi 9 akatoka babe girl. Furaha ya mwamba ikawa ni zaidi ya hii ninayoisimulia hapa.

Watoto walikuwa wazuri wa rangi na sura. Walionekana zaidi kufanana na mama kwa 80% , maana mama alikuwa mzuri kisha mweupe pee.

Wakapanga wazae kizungu, hivyo hawakutaka kuongeza mtoto wa tatu wala wa nne. Watoto wakalelewa kisasa kwa kutumia maziwa ya kopo ili yale ya mama yabaki kutumiwa na baba (watu wazima wanaelewa)

Baada ya miaka kadhaa yule boy akiwa darasa la tatu katika shule moja ya bei na yenye hadhi ya watoto wa wakubwa na wa kishua, na girl akiwa darasa la kwanza.

Mapenzi yakiwa motomoto huku mwamba akiwa ashamjengea mkewe jumba la kifahari (kwa sasa linaishi wazazi wa mkewe) kama asante ya kumzalia watoto wale aliowapenda kwa moyo wake wote. Ghafla babe boy akaanza kuumwa, kwa vile pesa ipo basi mtoto akapelekwa katika hospital bora kupata matibabu. Bila kutarajia wakaona hali inazidi kuwa mbaya, mtoto hali, hanywi mwili ukaanza kuishiwa nguvu na maji mwilini.
Mwamba akamhamisha his son kwa hospital nyingine yenye ubora zaidi. Hali ikaendelea na mtoto akaanza kupungukiwa damu. Hivyo ikashauriwa inabidi mtoto aongezewe damu kisha ndio aendelee na matibabu. Baba akasema yupo tayari kutoa damu kwa ajili ya kidume chake hicho kimoja cha mbegu.

Ikahitajika vipimo mbali mbali vya damu ili kuona kama magroup yao ya damu yanaendana, na pia baba Hana magonjwa nk (wale waliowahi kuchangia damu hospital wananielewa zaidi).

Baada ya vipimo vya kina ikaonekana kuwa group la baba sio lake hivyo anahitajika baba mzazi original ndo aje atoe damu. Mwamba akashtuka na kuwambia madaktari kuwa yeye ndio baba halali wa mtoto huyo na kwamba mtoto hana baba mungine yeyote zaidi yake yeye. Madaktari wakaendelea kusisitiza kwamba vipimo vinaonesha kuwa yeye na huyo mtoto hawana uhusiano wowote, hivyo damu yake pia haiwezi kuwa na msaada wowote kwa mtoto.

Mwamba na mkewe wakapandwa ghadhabu na kuamua kumhamisha mtoto wao katika hospital nyingine. Pia kule wakakuta tatizo la ukosefu wa damu ni kubwa hivyo inabidi tu aongezewe damu. Baba akasema atamtolea damu mwanae. Baada ya vipimo na huku nako wakakuta hola. Yani hakuna uhusiano wowote kati ya mwamba na mtoto. Hapo jamaa akaanza kuona ukweli wa zile taarifa za damu kwa hospital zote mbili. Alichofanya akakurupuka bila kumwambia mkewe kuwa anakwenda wapi. Hadi nyumbani na kukachukua kale kabinti kake walikokuwa wamekaacha na dada wa kazi hadi katika hospital nyingine kupima damu. Vipimo pia vikaonesha kuwa na huyu hawaendani kwa lolote wala chochote.

Mwamba akawasha gari hadi hospital na kumwambia mkewe ambae alikuwa ashakubali kuchangia dam kwamba waende nyumban mara moja. Mke akiwa na hofu wakaenda hivyo hivyo hadi home. Na jamaa kumtaka mkewe amweleze ukweli kuhusu watoto.

Mke alijaribu kuficha ficha ila baada ya jamaa kumtolea bunduki na kumwambia kwamba kama haongei ukweli atampasua kichwa, ikabidi amwambie ukweli kuwa kuna dogo fulan ambae walikuwa nae kwenye uhusiano toka udogoni mwake yani enzi za kimama mama, shule wakajikuta wameandikishwa darasa moja maana walikuwa majirani ila kijana alikuwa anamshinda binti mwaka mmoja tu.

Hivyo pamoja na kwamba aliolewa lkn bado alishindwa kuishi bila kupata penzi la yule kijana. Cha kushangaza kijana alikuwa anatwanga kitambo, ila watoto wameingia pindi tu baada ya binti kuolewa na huyo mumewe.

Mwamba baada ya kupata hizo taarifa hakutaka kumdhuru yule binti, alichofanya akajifanya amemsamehe na kumuomba kuwahi hospital kumtolea mtoto damu.

Ile binti anatoka, jamaa akaamua kujipiga risasi tano kichwani. Mke alipofika alikuta mfanyakazi analia, ile kuingia ndani anakuta maiti ya mumewe ikiwa sakafuni.

Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi.
Risasi tano kichwan inaweze
 
humu kuna watu wanajua kusoma na kuandika tu ila kichwani ni weupe sana

kundi la damu lina mahusiano gani na mzazi ingekuwa hivyo tungekuwa tunapimwa damu na sio vinasaba

yaani mpangilio wa paragrafu unaweza sema jamaa ni msomi sana kumbe mpumbavu

hata damu ujawah kutoa, hosp kuna akiba ya damu sio ukitoa mtu anawekewa hapo hapo pumbavu ww
 
Back
Top Bottom