Mwambe hili linakuondolea sifa ya kuwa mwenyekiti/kiongozi CHADEMA

Mwambe hili linakuondolea sifa ya kuwa mwenyekiti/kiongozi CHADEMA

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,815
Reaction score
103,955
Jana ulitoa kauli ambayo haitegemewi kutoka kwenye kinywa cha mtu anayewania kuwa Mwenyekiti, eti: Ruzuku itawekwa wazi na si kama ilivyo sasa ambapo ni siri ya viongozi wachache! Eti utajenga Jengo la ofisi ya chama na blah blah nyingi.

Sawa ni haki yako kutoa mawazo yako, bila kuingiliwa, lakini unaangalia unayatolea wapi na muda gani. Kama hayo ungeliyasema ndani ya chama, sawa kabisa.

Katika kipindi ambacho kuna mtu mwenye nguvu zote anaapa kuua upinzani, ni muda wa kuepuka any kind of migogoro ndani ya chama.

Wewe ndiyo kwanza unazua migogoro ukijua fika kuwa wakati wa chaguzi ndio muda wa mifarakanao katika taasisi kama hizi.

Unataka wana CHADEMA wakuelewe vipi? Una agenda gani kama sio kuisambaratisha CHADEMA?

Rais Magufuli alikusifia sana wakati fulani.

Hakika Mwambe hufai, ni Pandikizi.

Angalia CCM ulipotoka, Mwenyekiti wao anafanya mangapi ambayo hakuna ndani ya chama chao anayehoji (sisemi CHADEMA muige watu kufungwa midomo, hapana), lakini unaangalia ni muda gani unatoa malalamko kama hayo, hata kama kutafuta kura.

Nilitegemea uyaseme siku ya kuomba kura, sio kwenye mitandao ya kijamii kuwabeza wenzako kuwa ni "wezi"

Mwambe ni pandikizi, mkirogwa mkampa hata kura moja, CHADEMA mmekwisha, kama CUF na vyama vingine vya mifukoni!
 
Huyo ni ccm mole in Chadema. Hawezi kuwa m/kiti wa chama kama Chadema.

Ccm wamechemsha wangemuundia chama chake kama wanavyofanyaga but this strategy will not do, it's dead on arrival..!!!
 
Nipo pamoja na Mwambe japo siipendi na sihitaji kusikia habari za Ccm

Mwambe kaongea ukweli, Chadema tukubali tumefeli kutokuandaa mtu wa kumrithi Mbowe

Mbowe hata kama anagombea ilitakiwa awepo na mgombea mwingine mwanachadema asilia ili kama watu hawamuhitaji Mbowe waangukie kwa huyo mwanachadema OG

sasa hivi wasiomtaka mbowe hawana option zaidi ya mwambe tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma kitabu cha Dr Slaa ""nyuma ya pazia ",chadema iliyosalitiwa 2015"" ndipo utajua kuwa Mbowe ana kamati kuu nyengine tofauti na kamati kuu ya chadema..Dr Slaa anasema alipigwa na bumbuazi 2010 alipoambiwa eti kamati kuu imefanya kazi yake na kumchagua Dr slaa agombee uraisi wakati hakuna kikao chochote kilichokaa kumpitisha yeye kuwa mgombea urais
 
Jana ulitoa kauli ambayo haitegemewi kutoka kwenye kinywa cha mtu anayewania kuwa Mwenyekiti, eti: Ruzuku itawekwa wazi na si kama ilivyo sasa ambapo ni siri ya viongozi wachache! Eti utajenga Jengo la ofisi ya chama na blah blah nyingi.
!
Kwani kasema uongo? Kwani Ruzuku inawekwa wazi? Kwani jengo.la Ofisi lipo? Mwambe kasema ukweli
 
Ukisoma kitabu cha Dr Slaa ""nyuma ya pazia ",chadema iliyosalitiwa 2015"" ndipo utajua kuwa Mbowe ana kamati kuu nyengine tofauti na kamati kuu ya chadema..Dr Slaa anasema alipigwa na bumbuazi 2010 alipoambiwa eti kamati kuu imefanya kazi yake na kumchagua Dr slaa agombee uraisi wakati hakuna kikao chochote kilichokaa kumpitisha yeye kuwa mgombea urais
Lakini pamoja na bumbuwazi akasimama kupeperusha bendera!! Interesting...
 
Yaani mtu kuhoji kuhusu ruzuku ni pandikizi? Mtu kusema ataboresha office ni pandikizi? Mnaridhika ni kile kibanda cha kuku pale ufipa? Hivi mbowe kawapa nini? Mnataka atawale miaka mingapi?

Sent using Jamii Forums mobile app

JK. kwa ufupi anazo kichwani na atakumbukwa saana sasa hivi na hata akiwa RIP....
1..Za kuambiwa changanya na zako
2..Unajimwambafy
3..Wanazoza
na mengine mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom