Mwambe hili linakuondolea sifa ya kuwa mwenyekiti/kiongozi CHADEMA

Mwambe hili linakuondolea sifa ya kuwa mwenyekiti/kiongozi CHADEMA

Mwambe hana sifa ya msingi kupata uwenyekiti!!! YEYE ANATOKEA KUSINI MWA TANZANIA, KAMWE CDM HAITAPATA KIONGOZI KUTOKA MIKOA YA KUSINI. CDM NI FURSA YETU WACHAGA

Sent using Jamii Forums mobile app
Umewahi kuugua ukichaa?

Bob Makani alikuwa mchaga? Mashinji ni mchaga? Dr Slaa alikuwa mchaga?

Au unataka kusema wachaga hawana haki ya kuwa vipngozi wa chama? Kama huko CCM kuna sera ya kuwazuia wachaga wasiwe viongozi wa juu wa chama, vyama vingine havina huo ubaguzi. Ndiyo maana unaona ndani ya CHADEMA, mchaga ameweza kushika mpaka nafasi ya juu kabisa, si kwa sababu ya uchaga wake bali kwa sifa na maamuzi ya wanachama.
 
Nafikiri Mwambe amekosa ile sifa ya kawaida ya mtu makini.

Kwa fikra za Mwambe, CHADEMA itakuwa imara sana kwa kuwa na majengo mazuri ya ofisi? Mbona CCM walipora majengo mengi yaliyojengwa na wanachi wote lakini bado kimekuwa chama cha hovyo?

Alitakiwa aeleze wazi, hela ya chama kwa sasa inafanya kazi gani ili tulinganishe umuhimu wa kile pesa hiyo inachofanya na kama ikitumika kujenga ofisi.

Siku zote nguvu ya chama cha siasa ni kuwapata wananchama wengi. Nijuavyo, kwa sasa pesa ya chama imeelekezwa zaidi kwenye programs za kukijenga chama kwenye ngazi ya msingi. Wakufunzi wa chama wamekuwa wakihamia vijijini kukiimarisha chama, hasa kupata wananchama wapya na viongozi.

Ukiwa na wanachama wengi, wenye uelewa na commitment, ni wanachama ndio watakaojenga ofisi za chama katika maeneo yao. Bahati Mbaya Mwambe halijui.
 
Bams,
Kwanza uchaga, pili ukaskazini.

chukua faida za kuwa mwana chadema ulinganishe kati ya kaskazini na maeneo mengine ya nchi. Utagundua kuwa wachaga na kaskazini wamefaidi uwepo wa chadema kuliko pande nyingine za nchi
 
Jana ulitoa kauli ambayo haitegemewi kutoka kwenye kinywa cha mtu anayewania kuwa Mwenyekiti, eti: Ruzuku itawekwa wazi na si kama ilivyo sasa ambapo ni siri ya viongozi wachache! Eti utajenga Jengo la ofisi ya chama na blah blah nyingi.

Sawa ni haki yako kutoa mawazo yako, bila kuingiliwa, lakini unaangalia unayatolea wapi na muda gani. Kama hayo ungeliyasema ndani ya chama, sawa kabisa.

Katika kipindi ambacho kuna mtu mwenye nguvu zote anaapa kuua upinzani, ni muda wa kuepuka any kind of migogoro ndani ya chama.

Wewe ndiyo kwanza unazua migogoro ukijua fika kuwa wakati wa chaguzi ndio muda wa mifarakanao katika taasisi kama hizi.

Unataka wana CHADEMA wakuelewe vipi? Una agenda gani kama sio kuisambaratisha CHADEMA?

Rais Magufuli alikusifia sana wakati fulani.

Hakika Mwambe hufai, ni Pandikizi.

Angalia CCM ulipotoka, Mwenyekiti wao anafanya mangapi ambayo hakuna ndani ya chama chao anayehoji (sisemi CHADEMA muige watu kufungwa midomo, hapana), lakini unaangalia ni muda gani unatoa malalamko kama hayo, hata kama kutafuta kura.

Nilitegemea uyaseme siku ya kuomba kura, sio kwenye mitandao ya kijamii kuwabeza wenzako kuwa ni "wezi"

Mwambe ni pandikizi, mkirogwa mkampa hata kura moja, CHADEMA mmekwisha, kama CUF na vyama vingine vya mifukoni!
Ilitakiwa Mwambe amalizie vizuri statement yake kwamba ruzuku ya chama inaliwa na Mbowe ! Angeeleweka zaidi.
 
Haya haya mnayoyasema kuhusu CCM na Serikali yake ndo hamyataki yasemwe kuhusu CHADEMA. Wakina membe na wengine wakiisema CCM mnawaona mashujaa na majasiri hamuoni kama wanaleta migogoro ndani ya chama. Ushabiki ni mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Membe kasema nini kuhusu chama chake in a negative way?
 
KAMA MH. MWAMBE ALIZUNGUMZIA SUALA LA RUZUKU NA OFISI ZA CHADEMA WANACHADEMA WANAHAKI YA KUMPA KURA KM KWELI WANANIA YAKUJENGA CHAMA. jambo hili nimeliandika katika andiko na comment zangu hum JF. Siku 4zilizopita nikasema chadema nikibubu cha mbowee nanikathibitisha kwakuhoji rudhuku ya chama ambayo ameifanya kuwa niyake nahakuna wakuhoji wakati nipesa yetu ya walipakodi waTZ , nikahoji angarau ofice tu za chama hata ile yamakao makuu haina hadhi, mda huo anakodi ndege kwenda kuomba maridhiano kwenye sherehe yaanj ni ajabu kweli, namda huo anakagenge kawatu wachache ambao wengi wao niwachaga wenzake nabaadhi yawatu toka mikoa mingine ambao wapo pale km mandondocha nakuwafanya wanachama zaidi ya 2ml. Anaojisifia kuwa wapumbavu! Nasubiri kampeni za 2020 mungu atufikishe tutahitaji majibu ya maswari haya pamoja na maswari mengine mangi mtujibu. Najua mmepanga kuanza maboma ya ofice mwaka 2020 lakini hayatakuwa majibu yakujibu makusanyo yapesa miaka yte hyo namda huo tunachangia matibabu ya lisu. Mwambe umetusaidia kuchokonoa mada. Safi sana ila najua hawatakupa hata ukishinda ila umetupa nguvu yakuhoji
Usiwe jinga la kufuata mkumbo. CCM ina ofisi zipi za jasho lake? Una ushahidi kuwa Mbowe anakula hela za ruzuku au ndio praise team
 
Yaani mtu kuhoji kuhusu ruzuku ni pandikizi? Mtu kusema ataboresha office ni pandikizi? Mnaridhika ni kile kibanda cha kuku pale ufipa? Hivi mbowe kawapa nini? Mnataka atawale miaka mingapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaan hawa manyumbu ni wanyama wa kuhurumiwa tuu hawajui wanataka nini. badala ya kufanya maaamuzi yaliyosahihi na kwa muda sahihi wanamshambulia mtu sahihi ambaye atawavusha ksalama mto mara wasiliwe na mamba. Sasa ngoja tuone kesho siyo mbali.
 
Kitaturu,
Mwambe ni pandikizi. Hata kama una hoja, unaangalia mazingira ya wapi useme dukuduku lako. Si vema kunza kupandikiza migogoro wakati huu wa Magufuli. Ni hatari kubwa kwa ustawi wa CDM.
Nadhani wajumbe wa CDM wanamfahamu huyu CCM na pia wanamfahamu Mbowe!
 
Kitendo cha kuambiwa kuwa yuko kimwili Chadema lakini Kiroho yupo CCM tena tukaambiwa na mwenye nguvu HAFAI HAFAI ipo siku atarudi CCM huyo
Alisema Bwana Mkubwa kuwa Kmwili yuko CDM , rohoni yuko CCM, eti damu yake ni CCM
 
Wanaokuja na sera ya kuindoa Chadema chumbani wanapingwa kwa nguvu zote

Sent using Jamii Forums mobile app
hana lolote la chmbani, huyu ni pandikizi. Mfano wewe nyumbani ni CDM, uko huko kwa vile ulipishana nao siyo kuwa damu yako ni CCM, NEVER! Unadhani wewe kesho utakuwa hapo kama wadhifa ulionao, walikupokea kuikomoa CDM, siyo kuwa wanakupenda, labda kama.............omba sana Mungu!
 
Daniel Agger,

..TL alikuwa anaelekea kuwa mtu mwenye ushawishi kuliko yoyote yule ktk upinzani.

..ila akapigwa risasi ktk eneo la serikali, na lenye walinzi 24/7.

..kwa maoni yangu Sept 7 2017 ulitunyima waTz kiongozi mwenye ushawishi wa kuwa-challenge Mbowe na Magufuli ktk nafasi zao.

NB.

..aliyeondoa WALINZI wa eneo aliposhambuliwa TL anawafahamu waliopanga unyama ule.
 
Du. Chadema mnakwama wapi. Mna andika bila hata Aibu. Nyie kila siku mnashabikia Membe nk je MEMBE NI PANDIKIZI LA CHADEMA.
 
Retired,
Tatizo la Mwambe ni Mwana Chadema wa kuja. Hajaijua misingi ya kidemokrasia ndani ya Chadema ya kwamba ni "mwiko" kumsema vibaya Mwenyekiti Mbowe. Na bahati mbaya huyu Mwambe hajifunzi kwa Chacha Wangwe, Zitto Kabwe na Mzee Sumaye! Agghghg!
Hebu tuwaulize akina Kinana, Makamba (junior na senior), Membe, Nape, Ngeleja na wengine wengi kama ni ruksa kumsema ‘vibaya’ au hatu kumkisoa kwa haki mwenyekiti wa CCM Magufuli!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Umewahi kuugua ukichaa?

Bob Makani alikuwa mchaga? Mashinji ni mchaga? Dr Slaa alikuwa mchaga?

Au unataka kusema wachaga hawana haki ya kuwa vipngozi wa chama? Kama huko CCM kuna sera ya kuwazuia wachaga wasiwe viongozi wa juu wa chama, vyama vingine havina huo ubaguzi. Ndiyo maana unaona ndani ya CHADEMA, mchaga ameweza kushika mpaka nafasi ya juu kabisa, si kwa sababu ya uchaga wake bali kwa sifa na maamuzi ya wanachama.
Nazidi kuamini kweli wachaga hawapendwi nchi hii. Kama siyo hivyo basi hayo ndiyo maneno yanayoonekana kuwa na uzito wa kuivunja Chadema, maana kila chama chenye nguvu hutafutiwa maneno ya kukivumisha ubaya mpaka pale kinapotoweka.
 
Back
Top Bottom