Mzuvendi,
Nakuwekea hapo chini post ambayo niliiweka hapa siku ziizopita.
Nadhani kuna ndani yake kitu cha kujifunza:
Umuhimu wa
Abdul Sykes ulianza Burma akiwa katika 6th Battalion ya KAR
wakati wa Vita Kuu ya Pili (1938 - 1945).
Hapo ndipo alipowaeleza askari wenzake umuhimu wa kuunda chama cha siasa
kuwaondoa Waingereza Tanganyika.
Wakati huo
Abdul alikuwa na umri wa kiasi cha miaka 23 hivi.
Angalia hiyo picha yake hapo chini akiwa Burma:
Ukipitia Tanganyika Intelligence Gazette kuanzia 1950 hizi ni taarifa
za kikachero za Waingereza zikiandikwa na Special Branch utaona
habari za
Abdul akiwa Dar es Salaam na mikoani alikokuwa akipita
kuongea na viongozi wa TAA kuhusu hali ya baadae ya Tanganyika.
Moja ya taarifa hizi ambazo mimi ninayo ni ni safari ya
Abdul Sykes
ya Kanda ya Ziwa aliyofanya mwaka wa 1952 akiwa Katibu na Kaimu
Rais wa TAA kukutana na
Paul Bomani na kisha kuelekea Uganda.
Lakini kabla ya hapa mwaka wa 1950
Abdul Sykes alifanya mkutano
na
Jomo Kenyatta na kundi lake la kina
Paul Ngei, Kungu Karumba,
Bildad Kaggia na wengine Nairobi agenda kuu ikiwa kuunganisha nguvu
za Waafrika wa Tanganyika na Kenya kupambana na Waingereza.
Huu ulikuwa wakati wa Mau Mau.
Nimeeleza habari hizi kwa kirefu kwenye kitabu chake.
Mimi sikulaumu kuwa wewe hujui historia hii.
Utaijuaje ikiwa haikupatapo kuandikwa hadi nilipoiandika na kitabu kuchapwa
Uingereza mwaka wa 1998?
Tatizo lako ndugu yangu
Nguruvi3 ni kuwa unataka kuleta ubishi katika jambo
ambalo wewe huna ujuzi nalo.
Katiba iliyoandikwa na wazee wangu mwaka wa 1950 ipo.
Abdul Sykes kaieleza katika taarifa yake kwa wanachama wa TAA (Angalia:
Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January,
1951
Sykes' Papers).
Cranford Pratt katika kitabu chake ''Critical Phase in Tanzania,'' kaieleza na
kaisifia (Angalia: Cranford Pratt,
The Critical Phase in Tanzania 1945-1968,
Cambridge University Press, London, 1976, uk. 29-31.)
''Document'' hii hutoweza kuiona popote pale kwa sababu hata Tanzania National
Archives (TNA) imenyofolewa jalada liko tupu.
Hata kwenye maktaba yake ya ''microfilm,'' pia imeondoshwa.
Halikadhalika katika Maktaba ya CCM Dodoma jalada pia liko tupu.
Nimepata kuandika kuhusu, ''Lost Documents,'' naitafuta hii paper nikiipata nitaileta
barzani In Shaa Allah.
Leo sishangai kwako wewe kunitaka mimi nikupe ushahidi wa katiba iliyoandikwa
na wazee wangu mwaka wa 1950.
Wakati tunahariri mswada wa kitabu kulikuwa na ubishani mkubwa kati yangu na
wachapaji kwa kuwa neno nililoandika ni kuwa nyaraka hii ya katiba ''imeibiwa.''
Mhariri hakupenda neno hili na akasema niseme, ''imepotea,'' au ''haionekani.''
Isiwe ''imeibiwa.''
Nguruvi3,
Nimekupa ushahidi wa katiba iliyoandikwa na wazee wangu waliokuwa katika
TAA Political Subcommittee.
Document hii ilijadiliwa katika mkutano mkuu wa TAA 1954 mkutano uliounda
TANU na mwaka wa 1955
Nyerere alisoma yaliyokuwa katika ''document,'' hii
UNO mbele ya Kamati ya Udhamini.
Ikiwa hujaridhika na haya niliyokueleza mimi nipo hapa In Shaa Allah nasubiri.
Bahati mbaya unachoshwa na kusoma vitabu.