Mwami Theresa Ntare VI wa Heru - Chifu wa kwanza mwanamke

Ni kweli sijui mengi juu ya uhuru wa Tanganyika zaidi ya kile nilichofundishwa Primary na siwezi kuja kudai kwamba najua mengi. Watanzania wengi (keyword Tanzania) hatujui mengi jinsi ya uhuru wa nchi hizi mbili ulivyopatikana sababu moja ni jinsi tulivyofundishwa. Tumefundishwa kipolitics zaidi kwamba tunajua yale yanayosifia na yanayotukuza upande mmoja bila kujali pande nyingine. Uhuru wa Tanganyika kwa asilimia kubwa tulifundishwa uanzilishaji wa TAA then TANU na Nyerere, Nyerere, Nyerere, Nyerere up to independence. Ndio maana nasema kipolitics. Wangetufundisha vitu vyote hata vile vilivyokuwa negative from Team TAA/TANU/Nyerere katika post zangu unaweza kuona nimesema focus nyingi ilikuwa kwa Nyerere bila kujali mchango wa wengine. Hawa kina Sykes na wengine hawajapewa focus ya mchango wao ndio maana wengi hatuwajui. Nina uhakika wewe pia kuna mengi (harakati za uhuru) ambayo hujawahi kuyasikia huyajui na hutoyajua.
Nimeuliza awali je palikuwa na vyama vyingine zaidi ya TAA/TANU vilivyoshiriki katika harakati? Kuna watu ambao walikuwa na mawazo tofauti na kina Nyerere katika harakati hizi? Je unayajua haya Mr. Mohamed? Kama unayajua naomba utuletee. Tusiendelee kudanganywa kwamba watanganyika wote walikuwa wanakubaliana na lengo moja na msimamo mmoja. Hata katika hii story ya Mwami Thereza Ntare amesema hata Enzi zake palikuwa na vibaraka. Napenda kujua kama challenges hizi zilikuwamo ndani ya TANU. Napenda kujua watu Nyerere aliokwaruzana nao katika harakati. Vyote hivi ni part ya historia ya uhuru. Haya ndo nayasema as Informative. Tusikubali kuambiwa yale yanayopendeza tu wakati palikuwa na mengine yaliyo negative. Fikiria (hypothetical) hivi endapo CCM isambaratike kesho, keshokutwa baada ya miaka 50 wakija kuandika historia ya CCM wataandika yale mazuri tu ya CCM haya mabovu, maovu yafanywayo na CCM na watu wake hutayasikia. Hii pia inaweza kusemwa juu ya vyama vyingine pia not just CCM only.
 
Our system of education wasn't designed to produced thinkers. And what's worse is our independence didn't entail individual liberty which guarantee your right to question authority and be critical.
Yeah hilo ndilo tatizo. Ndio maana wengi tunapishana kuelewa humu. Elimu imedizainiwa kukwambia ukariri unachofundishwa sio ku-analyze na ku-question unachofundishwa.
 
Rubaman,
Yote ninayoyajua nimeandika katika kitabu cha Abdul Sykes.

Mengine nimayaandika katika papers nilizotoa katika mikutano
mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Na mengine mengi yamo katika www. mohammedsaid.com
na katika mitandao tofauti ya kijamii.

Ngoja In Shaa Allah niingie Maktaba nikutafutie kitu fulani
umekigusa hapo
juu.
 

Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia
mbele ya haki

By Gagnija

Alikuwa kipenzi cha wa-Tanganyika. Picha uliyoiweka ni ya Zanzibar kwenye
mazishi ya Karume aliyeuwawa kwa risasi, ulitegemea aende huko kama anakwenda
harusini? Labda kama alivyosema Jaji Werema, sisi wengine mambo ya huko hatuyajui
na hayatuhusu. Tuwaachie wenyewe.

Turudi kwenye mada, wale wazee waliompokea Nyerere Dar walisukumwa na kitu gani
hasa hadi kumchagua kuwaongoza mtu toka kijijini bara asiyejua hata kula chapati?

Gagnija,
Nakuomba upunguze hamaki.

Maswali unayouliza ni mazuri na yanaweza kunogesha sana mnakasha huu
ukawa wenye tija na vilevile kustarehesha wasikilizaji na wachangiaji ila
kwa sharti kuwa tuondoe hamaki zetu.

Tujiepushe na lugha, kwa kutumia lugha ya Bunge la Tanzania, tujiepushe
na lugha za ''maudhi.''

Vyakula kama chapati huendana na utamaduni wa watu.
Mie binafsi nikipata tabu sana na wenzangu tukisafiri.

Wanataka tukale chakula kwenye baa na wanaagiza pombe, ugali na nyama
ya kuchoma.

Nikitaabika sana la kwanza huo ugali na kisha kula chakula baa.

Lakini ndiyo maisha kila mtu ana mazoea aliyotokanayo kwao kwa hiyo kwa
sasa tuachane na hayo masuala ya ''chapati.''

Turudi kwenye mada.
Ukweli ni kuwa TAA ilikuwa imefika mahali haiendei mbele wala hairudi nyuma.

Walikuwa hawajaitisha ''delegates conference'' kwa miaka 4 toka ule uchaguzi
wa 1950 uliomtia madarakani Abdul Sykes na Dk. Vedasto Kyaruzi.

Lakini katika hii miaka 4 TAA ilikuwa imefanya mambo makubwa katika uwanja
wa siasa kiasi cha serikali kutoa onyo kupitia Government Circular No. 5 na 6
ya 1953.

Sasa haya ninayoeleza hapa chini ni katika mazungumzo yangu na Tewa Said
Tewa tulikyokuwa tukifanya mara kwa mara.

Tewa anasema Abdul ndiye aliyekuwa akizuia kuitishwa kwa hiyo ''delegates
conference,'' na mimi natumia neno lilelile alilokuwa akipenda kutumia Mzee
Tewa, ''delegates conference.''

Nilimuuliza Mzee Tewa, ''Vipi mtu mmoja anaweza kuzuia msiitishe mkutano
kwa miaka 4?''

Jibu alonipa lilikuwa, ‘’TAA ilikuwa haina fedha zake yenyewe na sisi katika
masuala ya fedha tukimtegemea sana Abdul.''

Katika majibu haya mimi nikafanya, ''deduction,'' kutoka taarifa nyingine
ambazo nilizokuwanazo kuhusu siasa katika kipindi kile.

Kipindi hiki cha 1950 - 1953 ndicho kipindi ambacho Abdul alikuwa na vikao
visivyokwisha nyumbani kwake na Chief David Kidaha Makwaia wa Shinyanga
kuhusu yeye kujitoa kwa Waingereza na kuja kuongoza TAA ili waunde TANU.

Wakati ule Chief Kidaha alikuwa katika Legico.

Mzee Tewa hili la kumleta Chief Kidaha TAA akilijua na alinieleza lakini yeye
hakuunganisha kama moja ya sababu ya Abdul kuchelewesha kuitisha kwa
wakati ''delegates conference,'' kwa kumsubiri Chief Kidaha.

Kwa nini Abdul alihangaika sana na Chief Kidaha?
Hili swali ni mojawapo ya maswali ambayo mie binafsi yakinitaabisha sana.

Jibu nililipata katika Nyaraka za Sykes.

Katika nyaraka hizi nimmesoma Dk. Wilbard Mwanjisi akiandika mwaka 1951
akisema maneno hayo hapo chini katika italics:

The conflict between TAGSA and the government was not to end there.
In his inaugural speech to TAGSA members upon his election as president,
Dr Mwanjisi attacked the British and called them ‘uncivilised’, emphasizing
in his speech the fact that human intelligence has nothing to do with race
or skin pigmentation; and that all human beings were born equal and therefore
subject to the same limitations.

Dr Mwanjisi called upon the government to allow civil servants to take part
in politics with the following words:

‘’In recent session of the Legico, Honorable Chief Kidaha Makwaia, advised
the Government to consider the question of allowing civil servants to take
part in open politics, I completely and fully support that young chief, the
greatest African politician of our day in this territory. There are many great
brains of his calibre but sorry, they are being wasted just because they are
civil servants.’’ [1] (
‘Doctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December,

1951. Sykes' Papers).

Chief Kidaha alipowakatalia TAA ndiyo sasa 1952 hapo akatokea Nyerere na
kisomo cha hali ya juu pamoja na Hamza Mwapachu kumueleza Abdul bila
kuuma maneno kuwa yeye anamjua vyema Nyerere na anaweza akakisaidia
chama pakubwa.

Kwa ufahamu wangu hali ilikuwa hivi na ndivyo Nyerere alivyoingia TAA pale
Makao Makuu ya TAA, New Street.

Ilikuwa baada ya hapa na Nyerere kuchukua uongozi kama rais wa TAA 1953
ndipo sasa alipojulishwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kwa wazee wengine.

Tatizo linalowakumba wengi ni huku kutojua hali halisi ya siasa za wakati ule
na ‘’advantage,’’ kubwa niliyokuwanayo mie dhidi ya wengi hapa jamvini ni
kuwa mimi ninazo taarifa ambazo hata hawa viongozi wa leo katika CCM
hawana na waliokuwanazo weshatangulia mbele ya haki

Bila ya taarifa hizi mtu atakuwa anapigiapigia pembeni tu hana mbele wala
nyuma.

Kilichojenga TANU si ule mkutano wa Julai 7, 1954.
Historia ya TANU ilijengwa kabla ya saba saba.

Kwa kumalizia na katika mojawapo ya maswali ambayo sijapata majibu hadi
hii leo ni kuwa Dk. Mwanjisi na Chief Kidaha walikuja kuwa maadui wakubwa
na Nyerere baada ya uhuru na wote wawili wakakimbia nchi na kwenda kuishi
Kenya.
 
Nini kilisababisha Dr Mwanjisi na Chief Kidaha wawe maadui wakubwa wa Nyerere baada ya uhuru mpaka wakimbilie Kenya?
Karibu ndugu Mohamed Said.
 
Nini kilisababisha Dr Mwanjisi na Chief Kidaha wawe maadui wakubwa wa Nyerere baada ya uhuru mpaka wakimbilie Kenya?
Karibu ndugu Mohamed Said.
Gwamahala,
Hili somo linataka utafiti zaidi kuweza kupata majibu.
 
Gwamahala,
Hili somo linataka utafiti zaidi kuweza kupata majibu.
Inasadikika kuwa Nyerere alikuwa hapatani sana na independent thinkers, kwasababu alipenda sana fikra zake zidumu. Watu dizaini ya Kawawa aliwapenda sana.
 
Inasadikika kuwa Nyerere alikuwa hapatani sana na independent thinkers, kwasababu alipenda sana fikra zake zidumu. Watu dizaini ya Kawawa aliwapenda sana.
Gwamahala,
Ahsante kwa taarifa hii.
 
Sahihi,hats Mzee wangu alinisimilia vivi hivi!alipofariki,alisema kwenye kaburi lake upande wa kichwani,ulipandwa mti uitwao" umurinzi!"sikimbuki vizuri kama jinahili ni sahihi!
 
Zito Kabwe siyo Mwami wa Heru kwani kwao Mwandiga hapastahili kuwa na Mwami? Tafadhali sana, usiwatukane Wanyaheru(Buha) kwa kuwavika sifa bandia wanasiasa. Wanyaheru ndiyo Waha halisi na HERU JUU ndiyo BUHA, wengine wote ni RUNDI
huu ni uongo. inawezekaje kijiji kimoja tu ndio kiwe na waha katika mkoa mzima wa kigoma, waliobakia wawe warundi?
Huu ni uongo mkubwa kabisa
 

Unakuta mtu anajiita chief tu mtaani hapa. Hajui hata historia ya uchief.
 
Mimi mwenyewe nimejaribu kuitafuta historia ya huyu mama ila sijafanikiwa, tusubili wenye kuifahamwatujuze
Mkuu nakusudia kuandika Historian ya Hawa mashujaa wetu.Lakini Kuna ufinyu wa Taarifa sahihi zinazowahusu.Nilitaka kuanza na Mwanamalundi lakini historian yake ina mkangayiko Sana.
 
Mkuu nakusudia kuandika Historian ya Hawa mashujaa wetu.Lakini Kuna ufinyu wa Taarifa sahihi zinazowahusu.Nilitaka kuanza na Mwanamalundi lakini historian yake ina mkangayiko Sana.
Njoo Bujola utapata msaada unaohitaji.
 
Unanikumbusha heru-ushingo, hili eneo hatari sana kwa ujambazi na ulozi kadiri ya masimulizi ya wenyeji.
 
Uso wake nao pia unaongea kitu kingine kizuri cha ziada kuhusu yeye; atakuwa alikuwa ni mama bora sana nyumbani hasa kwenye familia yake
 
HAPO zamani za kale jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake, ni wanawake wachache tu wanapatikana katika kurasa muhimu za Historia ya Tanzania. Kama vile Bibi Titi Mohamed, Binti Namabengo na Mkomanile au Nkomanile (Mwanamke shujaa wa vita vya majimaji).

Mjadala mkubwa umeibuka mitandaoni baada ya Rais Samia Suluhu Hassan mwamba wa Tanzania huyu kusimikwa kuwa mkuu wa machifu wote Tanzania huku machifu wa Kisukuma wakimpa jina la HANGANYA maana yake, ‘NYOTA INAYONG’AA’, mitandaoni wanadai haijawahi kutokea chifu akawa mwanamke.

Sasa kwa taarifa yako nikwambie tu kwamba, Theresa Ntare ni mwanamke shupavu ambaye alikuwa ni Mtawala (Chifu) kutoka katika kabila la Waha jamii ya Kitusi, Ukanda wa Kasulu sehemu za Heru juu. Huyu ni mwami Theresa Ntare VI, Malkia wa Heru kuanzia April 16, 1946 mpaka November 9, 1962. Mwanamama huyu aliweza kuwa Kiongozi wa Jamii ya Heru huko Kasulu.

Unapajua Heru?
Heru ni eneo ambalo lipo katika wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma. Eneo la Heru limegawanyika katika sehemu mbili (Heru juu na Heru chini). Heru Chini inaundwa na vijiji vya Nyansha, Mgandazi, Ntare, Bugaga, Nyumbigwa, Nkundutsi, Zeze na vijiji vyote vya maeneo ya Kasulu ya chini. Heru juu inaundwa na vijiji vya Munyegera,Heru na Buha pamoja na vijiji vya ukanda wote wa juu kuelekea Buhigwe.

Kihistoria Wanyaheru (Buha) ndio hasa Waha asilia na Kiha cha Heru (Buha) kina tofauti ya kimatamshi na jamii zingine za Waha. NGOMA ZA BWAMI ambazo ni maarufu kwenye kabila la Waha zinaelezwa kushamiri eneo la Heru zaidi kuliko maeneo mengine.


Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika. Sina details nyingi za huyu mama, WanaJF kama kuna anayefahamu zaidi kuhusu huyu mama shupavu basi atupe historia yake.

Alipata nafasi ya kwenda kusoma Ulaya enzi ukoloni nafasi maalum za watoto wa machifu. Alihitimu mafunzo ya ya sheria akawa msaada mkubwa sana wa kisheria wakati wa kudai uhuru, hasa kwenye mikataba ya kimataifa.

Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni mkuu wa machifu akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958. Makabidhiano yalifanyikia Shule ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.

Mengi hayajulikani katika historia ya utoto wa Mwami Theresa Ntare, lakini inaaminika alikuwa mtoto wa kike pekee wa Chifu Ntare. Inaelezwa kwamba Mwami Theresa Ntare alitawazwa uchifu baada baba yake Mwami Ntare kukosa mtoto wa kiume.

Baada kutawazwa uchifu ilibidi atafutiwe mchumba kutoka ukoo wa Chifu Lusimbi wa Kalinzi hivyo akawa ameolewa na kijana wa Kitutsi kutoka Kalinzi akiitwa George Shinganya.

Kulingana na mila za Kiha, Mwami haolewi. Akiolewa inabidi ahame milki yake ya uchifu ili akawe mke wa huyo mwoaji. Hivyo basi, Mwami Ntare hakuolewa na George Shinganya. Bali familia ya Mwami ndiyo iliyolipa mahari kwa familia ya Shinganya. Hivyo, Jina la Shinganya likaondolewa na akaitwa George Ntare.

Baadaye ndoa ya Ntare na George ilivunjika na Mwami akaoana na Mwami Louis Dantes Ngua wa Ufipa (Huyu ana asili ya uchifu wa Ufipa). Kuna nadharia zinazoeleza pia kuwa Mwami Theresa Ntare alipata pia kuwa mke wa Chifu Makwaia wa Usukuma. Lakini hakuna ushahidi wowote juu ya hilo.

Wakati wa zama hizo jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake hasa katika masuala ya Uongozi. Hilo halikumfanya Mwanamama Ntare asiweze kuongoza vizuri na kishupavu jamii yake ya Waha wa Heru huko Kasulu.


Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni Mkuu wa machifu wote Tanganyika akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958. Makabidhiano yalifanyika shule ya sekondari ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.

Mwani Theresa Ntare aliheshimika kama Chifu wa Kasulu yote na sio tu Heru alisimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru.

Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja ya wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika.

Aliendelea kuwa Mbunge mpaka miaka ya 1980, lakini kabla ya hapo aliachia uchifu Disemba 9, 1962, Katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam nchini Tanganyika. Hapo alikaribishwa kama Malkia wa Heru kwa Ngoma Maalum kutoka Ngome ya Malkia wa Heru kwa heshima kubwa.



Inaelezwa alifariki miaka ya 1990 na mara ya mwisho alikuwa akiishi maeneo ya karibu na barabara inayoelekea Munyegera – Kati ya ilipo shule ya msingi na Kahaga Dispensary (kulikuwa na soko hapo kati miaka ya 1985).

Kwa sasa Mwami wa Heru ni Costa Shinganya au Ntare ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mwani Theresa Ntare. Kuna wanaosema Mbunge wa Kigoma mjini, ndugu Zitto Ruyagwa Kabwe ndiye hasa Mwami wa Waha wote. Lakini hili ieleweke yeye amepewa heshima tu ya Mwami Mpole aliyejulikana kama Ruyagwa.

Huyu ndiye Mwami Theresa Ntare VI, Malkia wa Heru kuanzia 16 Aprili, 1946 mpaka 9 Novemba, 1962. Matukio mawili yaliyowatokea yeye na Baba wa Taifa ni: Walizaliwa mwaka mmoja 1922,wamefariki mwaka mmoja 1999.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…