Mwamposa ajitetea kuwakamua waumini 'sadaka ya kujimaliza', atoa ufafanuzi mujarabu

Mwamposa ajitetea kuwakamua waumini 'sadaka ya kujimaliza', atoa ufafanuzi mujarabu

Mambo ya kiimani ni mapana sana na yana siri ambazo wapo wanaozijua na wapo wasiozijua huwa sipendi kuhoji sana watumishi wanaonda mienendo tofauti nachofanya nikutafuta napopaamini, na kumuomba Mungu pia kunionyesha kweli, tusinyoshee vidole watumishi hata kama wapo katika njia potosha wewe hama kanisa basi mtafute Mungu wa kweli alipo na ukimtafuta utampata
Huo upana na siri ndipo utapeli unapo jifichia.
 
Mganga sio mtumishi wa bwana ila Mwamposa ni mtumishi wa mungu pindi anapofanya cha tofauti lazima tujiulize Mara mbili mbili usi mfananishe Mtume mwamposa na mganga
[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Jana nilikutana na mfuasi wa Mwamposa akawa anatamba kwamba yeye ni msomi ana digrii ya uchumi lakini hawezi kumuacha Mwamposa. Anasema kwamba zamani alikuwa anaenda sana kwa waganga lakini baada ya kuingia kanisani kwa Mpwamposa ile roho ya kwenda kwa waganga imekata. Hivyo, hawezi kumuacha mtume kwa kuwa kamtoa kwa waganga na ataendelea kumtolea sadaka bila kuchoka ijapokuwa bado hajapata kazi.
NI SUALA LA MUDA TU,
WATAOKOLEWA NA MUDA NA SIO MTUME WALA NABII.
KUNA MUDA FAHAMU ZITARUDI, AKILI ITARUDI INGAWA MUDA UTAKUA UMEKWENDA
 
Mimi kuna ndugu yangu nilimsaidia issue flani ivi akaenda kumshukuruku mwamposa kwa maombi yake kujibiwa , namwangaliaga tu ata sielewi kichwa chake kipoje.
Hao watu (hasa wanawake) wakishaenda kwa Mpwamposa kuna kitu anawatilia kichwani, sio bure! Kuna jamaa yangu mmoja yupo huko miaka 2 sasa, ukimuona ni zaidi ya CHIZI. Utamhurumia sana.
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mtume Boneface Mwamposa (Bulldozer) amefafanua kwa ufasaha maana ya "sadaka ya kujimaliza" inayotolewa na waumini wa kanisa lake baada ya kupokea shutuma mbalimbali kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akiwakamua waumini hela zote hadi wanakosa nauli ya kurudia majumbani kwao.

Ufafanuzi uliotoka ni kwamba kutoa sadaka ya kujimaliza sio kutoa fedha zote ambazo mtu amekwenda nazo kanisani. La hasha! Maana ya sadaka ya kujimaliza ni kutoa fedha zako zote ulizonazo benki na kuziwasilisha kwa mtume kama sadaka. Kwa mfano, kama una akaunti 5 kwenye benki tofauti, komba pesa zote zilizomo kwenye akaunti hizo umtolee Mungu wako. Hii ndio maana halisi ya sadaka ya kujimaliza. Yaani unajimaliza kabisa na kuanza upya!

Mtume amesema hayo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkesha wa mwaka mpya unaoenda kwa kaulimbiu ya "vuka na chako" utakaofanyika kanisani kwake katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

MAONI YANGU
Binafsi nimewahi kusimuliwa na muumini mmoja aliyetoa sadaka fedha zote alizokuwa nazo hadi nauli lakini wakati anaondoka kwa miguu kuelekea kwake Gongolamboto akitokea Kawe, mtume akamfanyia muujiza akaokota noti ya Tsh 5000 akaitumia kama nauli, yeye na wanawe wawili aliokuwa ameandamana nao.

Nsamini sasa ufafanuzi umewekwa wazi kwani waumini na wananchi walikuwa hasa hawafahamu maana ya sadaka ya kujimaliza.

Nawasilisha.

Pia soma > Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini
Wajinga ndio waliwao, yani ukaushe account yake ukajaze kwenye account ya mwenzako? Mbeya Mbalizi amejenga hotel ya hatarii, kanunua kijiji na mtaa mzima, hivi serikali haiwezi kuingilia utapeli huu kwa kivuli cha jina la Yesu?
 
Kwa kuwa wanajipeleka wenyewe sidhani kama serikali inaweza kuthubutu kuingilia kati jambo kama hili.
 
Hao watu (hasa wanawake) wakishaenda kwa Mpwamposa kuna kitu anawatilia kichwani, sio bure! Kuna jamaa yangu mmoja yupo huko miaka 2 sasa, ukimuona ni zaidi ya CHIZI. Utamhurumia sana.
Hatari sana
 
Screenshot_20230505_075141_WhatsApp.jpg
 
Ani hawa watu sijui hata wanalishwaga nini!! Wakukute sasa unamuongelea vibaya huyo Mwamposa wao uone watakavyokuonea huruma watakwambia una mapepo😂😂😂
 
Ani hawa watu sijui hata wanalishwaga nini!! Wakukute sasa unamuongelea vibaya huyo Mwamposa wao uone watakavyokuonea huruma watakwambia una mapepo😂😂😂
Kweli kabisa. Yaani wao wanajiona wako sahihi 101%.
 
Ila ndugu zangu wakristo mjitafakari
 
Mimi kuna ndugu yangu nilimsaidia issue flani ivi akaenda kumshukuruku mwamposa kwa maombi yake kujibiwa , namwangaliaga tu ata sielewi kichwa chake kipoje.
Walalahoi wengi hasa wanawake wanatapeliwa sana na Mwamposa. 99% ya wafuasi wake ni wanawake. Sijui hawa viumbe wanakwama wapi hadi wakubali kutapeliwa kirahisi hivyo.
 
Back
Top Bottom