Mwamposa Buldoza anazo nguvu za kweli

Mwamposa Buldoza anazo nguvu za kweli

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
1,842
Reaction score
6,087
Apostle kuna miujiza huku, nini kimetokea mkaka alikua hatembei miaka 30 baada ya maombi ameanza kutembea,

halleluyaaaaaaaaa, nani mtenda miujiza yeeeeeesu.

Nilikua nikisikia hivyo nabadilisha channel nilijua ni uongo tu.

Juzijuzi hapa kuna issue ilitokea ikanifanya nianze kumfatilia mwamposa buldozer, ndugu yangu hapa mtoto wake alikua anauguaugua yuko dhohofu akaamua kuanza kufatilia mwamposa vipindi vyake.

Akawa anafatilia maelekezo mfano unachukua maji unayaombea kwa imani (maji yoyote hata ya nyumbani kisimani au bombani), kitu cha ajabu kikatokea mtoto akatoa haja kubwa mbegu ya fenesi kuubwa, baada ya mda mtoto akaanza kupata nafuu.

Ikabidi prakatuba etumba etumba nianze kufanya research juu ya huyu mwamposa, aisee kiukweli hata Kama anatumia uchawi Mimi sijui, lakini matendo anayoyafanya yeye na wewe endapo ukipractise kwa miezi 6 utaanza kuona utofauti maishani mwako kwanini

Jamaa anazo ibada mbili, j.2 asubuhi na jioni, usiku pia kuna operation komboa familia kuanzia saa 4, usiku saa 8 jamaa yupo live, asubuhi saa 2 jamaa yuko live yaani ni maombi tu alafu ni kila siku hiyo ndio daily routine yake.

Hivi niwaulize sisi wengi daily routine zetu asubuhi hatusali tunaingia job, jioni tunapitia bar usiku tunasali kidogo au hatusali kabisa, mtoto wako anapata mapepo huwezi hata kumuombea maana ukianza kuomba pepo anaweza kukupiga makofi na kukucheka.

Siwazi saana kuhusu njia zake za maji na mafuta kwenye kupiga hela lakini nikichojifunza anakutengenezea wewe kua na imani kwamba endapo nikitumia haya maji basi nitapona....kwenye biblia kuna mifano mingiii Sana kuhusu manabii waliotumia vitu mbalimbali kwenye uponyaji

Anachofanya mwamposa ni kwamba ali-invest mda wake kumtafuta Mungu akapata hii power then kwa sababu yeye ni mjanja mjanja anatumia nguvu alizo nazo kupiga hela.
sawasawa na wewe unalima mashamba mwisho wa siku upate faida kwa investment uliyofanya.

Tunachokoswa sisi naona ni Imani, Imani yako ndio inakuponya sio mwamposa mwamposa yuko kati tu pale kuiboost imani yako maana ukisikia tu mafundisho yake Unapata nguvu ya kiroho.

Mwamposa haponyi anaeponya ni Mungu anachotaka kwako ni imani tu

Siku moja alitoa siri akasema ombeni sala ya baba yetu ulie mbinguni Mara 5 asubuhi, mchana na usiku na saa 8 usiku ukiweza kuamka Kama dozi vile kwa imani, utaanza kubadilika Kiroho.

Wengi wetu hatukumbuki Mara ya mwisho kuomba sala ya baba yetu, anaweza kua anapiga hela Sana kwenye sadaka lakini Mimi naona acha awapige tu maana yeye kagundua siri ambayo wengi hawaijuiii.

Kundi kubwa la watu wanaotoka usukumani wengine hata kiswahili Hawajuii wanaenda kushuhudia awezi kuwapanga wote wale but wengi imani zao ndio zimewaponya narudia Mwamposa ni catalyst tu amegundua ukweli ulipo ni IMANI TU NDIO UFUNGUO WA UPONYAJI, MTU KWENDA KWA MWAMPOSA ANAJUA ANAENDA KUPONA ameshahamini tayar, kumbe mwamposa haponyi ila imani ya wenye matatizo ndio inawaponya.

Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.
 
Kwa7babu nyinyi ni "WASHIRIKINA" "USHENZI WENU" umechupa mipaka mnacho kifanya hapa kawe Kila j.pili ni kufanya biashara zenu. MAFUTA na MAJI YA CANADIAN.
Mimi ni msabato bro, nilichoandika ni research fupi niliyoifanya, naweww ungekuja na yakwako ya kishirikina na uchawi, labda Kama unataka ligi
 
Ni kama hii michezo ya bahati nasibu wanaoshinda ni kidogo sana kuliko walioliwa, kuna watu tunawajua wao ni hodari sana wa kwenda huko wanajua ratiba zote na za kanisani kwa Mwamposa na wana imani kweli na miujiza ya Mwamposa ila wanaishia kusimulia shuhuda za wengine tu wao hadi leo hawana ushuhuda wao binafsi toka waanze kwenda huko kwa Mwamposa.
 
Back
Top Bottom