Mwamposa Buldoza anazo nguvu za kweli

Mwamposa Buldoza anazo nguvu za kweli

Kama issue ni imani sasa kwa Mwamposa anaenda kufanya nini? Kwanini asikae huko nyumbani na kuomba kwa imani ya kweli kabisa na kutegemea kupona?
Rejea nikichoandika watu hawana imani wanaenda kwa mwamposa kupata uponyaji so jamaaa ataendea kuwapiga tu maana siri ya uponyaji hawaijui
 
"Kundi kubwa la watu wanaotoka usukumani wengine hata kiswahili Hawajuii wanaenda kushuhudia"


Umemaanisha nini hapa kuleta dharau kwa kabila la watu tena kabila kubwa luliko la kwako shenzi wewe!!!
Sawa nimetolea mfano Mimi mwenyewe ni mnyatunzu Wa bariadi tena msukuma halisi
 
Ndugu Mungu hawezi kuja ukamuona ila uja kupitia watu wake,Mimi nina imani sana Mungu wa Elisha na Yakobo,Mungu wa baba yetu Ibrahim yuko pamoja na Nabii Mwamposa,naomba Mungu wake anisaidie niachane kabisa na kamnyoso
 
Nakupendekezea msikilize mchungaji Mbaga
Screenshot_20220826-191238.png

Ninayo collection ya mahubiri ya mchungaji mbaga zaidi ya 50, nimesubscribe mahubiri tv mmoja kati ya wahubiri ninaowapenda mnoo kwa imani yangu.
 
Unamaanisha asisome biblia?
Nabii ni mtu anaekuja na prophecy ya mambo yajayo hasomi popote ila anatamka yanaandikwa anayotamka , ukisoma history ya nabii isaya alikuwa uchi mwaka mzima anatamka unabii mpaka wa kuja kwa Yesu , Sasa Leo hii nabii anasoma unabii wa isaya alafu na yeye anajiita nabii ata kutembea na boxa mtaani hawezi
 
Nabii ni mtu anaekuja na prophecy ya mambo yajayo hasomi popote ila anatamka yanaandikwa anayotamka , ukisoma history ya nabii isaya alikuwa uchi mwaka mzima anatamka unabii mpaka wa kuja kwa Yesu , Sasa Leo hii nabii anasoma unabii wa isaya alafu na yeye anajiita nabii ata kutembea na boxa mtaani hawezi
Mimi Mkuu unabii wa mwamposa au manabii wengine sijui wamepatia wapi, lakini ni janja janja tu za kupatia pesa tu....kwa imani yangu nabii wa mwisho ni mama Helen g white, hawa wengine inaweza kua majina wanajiita tu
 
umesoma uzi wote?

Nimesoma uzi wote na napenda kukuthibitishia kwamba dhumuni kuu la uzi huu ni kumtukuza mtu na sio MUNGU.

Nimeona vijana wake wakishuka nyuki kuhoji utimamu wangu, nawathibitishia kwamba nina akili kuliko vile wanavyoweza kufikiri.

Kama wewe ni Mkristo unayeamini kuwa MUNGU yupo na hujaona shida kuanzia katika kichwa cha uzi basi acha kumuabudu MUNGU na ufanye mambo mengine.

Soma kichwa cha uzi na uniambie kuna tofauti gani na zile sms za "Ninae babu yangu ni mganga wa Sumbawanga na ana nguvu hakuna linalomshinda"


 
Back
Top Bottom